Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ina maana alikuwa "hajajitambua". Unaweza ukamuonya mtu asikuelewe. Baadaye akatafakari akaelewa. Kuna stages za kukubali jambo. Mara ya kwanza huwa kwa kawaida ni denial. Understanding inakuja baadaye na hapo ndipo mtu huanza kujirudi. Si unaona hata Nyerere? Kwani katika utawala wake uliwahi kusikia akisema "nimekosea"? Lakini wakati ameshang'atuka ndiyo tulisikia akisema "hata mimi nimefanya makosa mengi". Hapo ndipo alitambua na hii ilikuja baada ya kutafakari na pengine hata kulinganisha wengine wanafanya nini. Kwa hiyo, hata kwa Mbowe, kama kauli yake ni genuine ni vizuri tukaona kwamba amefanya vizuri kutambua na tunaweza kuendelea kumsaidia ili awe mwangalifu zaidi. Kwenye siasa kuna approaches nyingi sana za kuendesha siasa. Kuna baadhi ya approaches zinatumika kama watu hawana uelewa mzuri wa mambo na nyingine kama wana uelewa mzuri wa mambo ingawa wanasiasa wengi wanawachukulia wananachi kama hawaelewi kitu, bali ni wao tu wanaoelewa.
 
Nani kakwambia "haki hupewa"? Haki ni "inalienable" unakuwa nayo hata kabla ya kuzaliwa. Ni jukumu lako kuidai kila mara unapoona inakandamizwa au unanyang'anywa/porwa. Kuna legal maxim inayosema: "He who sleeps over his rights loses them". Maana yake ikiwa kwamba "usipodai haki zako" (pale zinapokandamizwa/porwa) utazipoteza.
 
Sijawahi kuweka imani kwa kiongozi Bali imani yangu ipo kwenye Chama Cha CHADEMA

Kwani Chadema ni nini?

Chadema ni chama cha kisiasa kilichoundwa na sera/katiba + viongozi + wanachama...

Ukikitoa kimoja, huna chama
 
Ukiweka pembeni hili la maridhiano, Lisu, Heche, Ruge na wengine unaopendekeza wapewe uongozi wa chadema ni sehemu ya team ambayo imekuwa ikizidiwa akili na CCM. Kwanini husipendekeze wote hawa waachie ngazi kama hoja yako ni kukisafisha Chama?
 

1. Hili la "kesi" ulilileta wewe. Katika kujiridhisha, ukalitolea ufafanuzi. Nikakwambia kama ndivyo halina shida, tukalifunga.

La 'kesi' ni issue closed natumai umelileta tena hapa katika kujiridhisha tu kuwa limekwisha.[

2. Kuwa simple au difficult, misifa na kujipamba binafsi ulikoandika? Hili ni la kushangaza. Suala siyo kwa tathmini binafsi.

"Ndiyo maana mahakamani kuna hakimu, mwendesha mashtaka, mshitakiwa, mashahidi, nk. Watu tofauti hao."

Si busara sana kujifagilia mwenyewe. Nyani haoni kundule.

Muhimu ni kujiridhisha kubakia kwenye hoja. Hoja hujibiwa kwa hoja; moja moja, bila kuacha au kuruka moja.

Kwamba unadhani kuna anayependa au hata kuwa na muda wa kubishana? Busara ni kuwa ukiona mtu kaamua kutumia muda wake kujadili jambo, kuheshimiana, uungwana, nk haviwezi kuwa na mbadala.

"Hatujuani, humu naweza kuwa mtu yeyote kama ilivyo kwako pia."

3. Kwamba nakimbilia kujibu, sikusomi na yote uliyosema hapo? Usinisemee mimi tafadhali. Wewe si supernatural kuyajua hayo huko uliko. Huna ushahidi huo kwenye lolote.

Kwa wazi nimeweka maswali kila ilipobidi na pua namba za aya kuwezesha kurejea popote nilipoandika kirahisi. Upo ushahidi mwingi kukumbusha kuwa hujibu maswali yangu yoyote:

"Kwamba bila shaka husomi, huchukui muda kuelewa, nk; bali unakimbilia kujibu.

Au labda ndiyo sababu unadhani nami nafanya hivyo?
 
Kwani Chadema ni nini?

Chadema ni chama cha kisiasa kilichoundwa na sera/katiba + viongozi + wanachama...

Ukikitoa kimoja, huna chama

Tatizo ni kuwa kwenye msafara wa mamba tunajua kuwa kenge nao huwa wako kazini.
 
- Sasa kama hata maneno nayotumia hapa kwa nia njema kwako yanageuka tatizo, sijui nitumie maneno gani mengine, mimi kusema simple, nimemaanisha simple kama ilivyo, sihitaji kujipamba hapa mimi sio bwana harusi wa JF!.

- Kutofautiana mawazo kwangu sio tatizo, ndio maana nikakwambia umekurupuka kujibu, kwasababu kama ungenisoma mwanzo kabisa nilipoandika neno "kesi" kwenye tafsiri yake nilikwambia nimemaanisha kutofautiana mawazo.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ukiweka pembeni hili la maridhiano, Lisu, Heche, Ruge na wengine unaopendekeza wapewe uongozi wa chadema ni sehemu ya team ambayo imekuwa ikizidiwa akili na CCM. Kwanini husipendekeze wote hawa waachie ngazi kama hoja yako ni kukisafisha Chama?

1. Ninasimama na Economist kwa sababu zilizopo humu:

Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

2. Huu ni uzi wa Oct. 18, ukionya mapema mno kwenye mambo haya haya bila kuchoka, hadi mtandaoni.
 

1. Wapi nimesema nina tatizo na neno lolote?

2. Nimesema tuache kujifagilia na kushutumiana.

3. Hapo #2, hilo ni jukumu la watazamaji au wasikilizaji (third party).

4. Hapo #3, tofautisha third party na mashabiki.

Nikazie hapa kuna swali moja kwako la kujibu, na hoja moja ya kuthibitisha "hapana kujifagilia au kushutumu."
 

1. Kumbe umerudi kwenda ku edit tena baada ya miye kujibu?



2. Kwamba ghafla baada ya kujibu umerudi ku edit kuongeza aya ya kwanza ambayo haikuwapo?

3. Huo siyo ustaarabu.

4. Thibitisha umeongezea aya Ili kama ni nia yako kujadiliana kistaarabu niijibu hiyo pia kwanza.

5. Ku edit baada ya kujibiwa ni uhuni!
 
Nime edit kuongeza aya ya pili, jamaa hunisomi kwa makini na kunielewa, sasa natumai hata nawe umejiona.

Soma paragraph ya kwanza sehemu zote mbili uone kama zimetofautiana hata neno moja! ndio maana juu kule nilikwambia unakimbilia kujibu bila kusoma na kuelewa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
1. Ninasimama na Economist kwa sababu zilizopo humu:

Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

2. Huu ni uzi wa Oct. 18, ukionya mapema mno kwenye mambo haya haya bila kuchoka, hadi mtandaoni.
Unapo ongea neno "ujasiri" unamaanisha nini? Kwamba hao unaowaita majasiri watachukuwa bunduki wakaing'oe CCM madarakani au watatumia mbinu hizihizi za majukwaani na ushawishi kukubalika kwa wananchi? Akili na mikakati ndiyo njia pekee iliyopo kuikabili CCM na siyo fujo. Wao wanatumia vyombo vya dola kugandamiza upinzani.
 

1. Kwamba unakubali ilikuwa paragraph moja; ambayo kwanza ilikuwa hii:



2. Kwamba ume edit baadaye na sasa ziko mbili ambazo ni hIzi:



3. Na bado unasema mbili hizo zimefanana neno Kwa neno kila mahali?

4. Hebu zirejee uzipitie kisha ulete mrejesho.
 
Namaanisha soma paragraph ya kwanza, sehemu zote mbili, ili uone kama zinatofauti ya neno hata moja.

Simply siku edit kubadilisha nilichoandika mwanzo kama unavyodhani, nili edit kuongeza paragraph ya pili pekee.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Wana CCM watakupinga kwasaba Mbowe ni mtu muhimu sana kwa utawala wa CCM kwenye kulaghai wafuasi wake ili mambo yaende.

fikiria mwenyekiti wa chama angekua Lisu au Heche rasimu ya katiba ya Warioba wangeitilia mkazo na kingeeleweka.
Lisu mwenyewe kaka sio wa kumuamini sana ki vile, wakilambishwa asali hamna anaesalia.
 
Ile ya kumpa uenyekiti Lowasa na kumfanya mgombea ilikua ni karata ya CCM. CCM walijua wakimkata huku ataenda kule na atagombea. Itakua rahisi Kwa wao kupepea na kuchukua umaarufu Kwa wananchi zaidi maana Kila mwananchi anafahamu ni namna Gani Chadema walimnanga Lowasa Leo wamempokea Tena Kwa kumfanya mgombea.

Mbowe apumzike tu maana chama kitamfia mkonni.
 
Uchambuzi wako ni dhaifu sana. Uamuzi wa kumchukuwa Lowassa ilikuwa ni siasa za matukio ambao kwa mtu yoyote mwenye weledi ktk siasa angeufanya. Jifunze hata kwa wenzetu pale Kenya, Ruto, Kenyatta na Odinga hawajawai kuwa na vyama vya kudumu lakini wao wamedumu ktk siasa muda wote.

Kwa wagombea Urais ndani ya Ukawa kwa wakati huo (Dr. Slaa na na prof. Limpumba) waliokuwa wakipigana vikumbo vya kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera, kati yao hawa hakukuwa na mtu potential kumzidi Lowassa kwa wakati huo. CCM yenyewe ilimuogopa na iliofia sana alipohamia Chadema. Pamoja na kuhujumiwa kwenye zoezi la kupiga na kuhesabu kura lakini wote ni mashahidi wa idadi ya wabunge walioingia bungeni kutokana na ujio wa Lowassa ndani ya Chadema.
 

Bila Lowasa upinzani ungepata wabunge zaidi na heshima yao ingebaki palepale, sasa hivi unashangilia wabunge ambao wote walikuja kuunga mkono juhudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…