1. Hili la "kesi" ulilileta wewe. Katika kujiridhisha, ukalitolea ufafanuzi. Nikakwambia kama ndivyo halina shida, tukalifunga.
La 'kesi' ni issue closed natumai umelileta tena hapa katika kujiridhisha tu kuwa limekwisha.[
2. Kuwa simple au difficult, misifa na kujipamba binafsi ulikoandika? Hili ni la kushangaza. Suala siyo kwa tathmini binafsi.
"Ndiyo maana mahakamani kuna hakimu, mwendesha mashtaka, mshitakiwa, mashahidi, nk. Watu tofauti hao."
Si busara sana kujifagilia mwenyewe. Nyani haoni kundule.
Muhimu ni kujiridhisha kubakia kwenye hoja. Hoja hujibiwa kwa hoja; moja moja, bila kuacha au kuruka moja.
Kwamba unadhani kuna anayependa au hata kuwa na muda wa kubishana? Busara ni kuwa ukiona mtu kaamua kutumia muda wake kujadili jambo, kuheshimiana, uungwana, nk haviwezi kuwa na mbadala.
"Hatujuani, humu naweza kuwa mtu yeyote kama ilivyo kwako pia."
3. Kwamba nakimbilia kujibu, sikusomi na yote uliyosema hapo? Usinisemee mimi tafadhali. Wewe si supernatural kuyajua hayo huko uliko. Huna ushahidi huo kwenye lolote.
Kwa wazi nimeweka maswali kila ilipobidi na pua namba za aya kuwezesha kurejea popote nilipoandika kirahisi. Upo ushahidi mwingi kukumbusha kuwa hujibu maswali yangu yoyote:
"Kwamba bila shaka husomi, huchukui muda kuelewa, nk; bali unakimbilia kujibu.
Au labda ndiyo sababu unadhani nami nafanya hivyo?