USHAURI: Mdogo wangu amekataa shule, nataka nimtafutie fani ya ufundi asiwe mzigo mbeleni

USHAURI: Mdogo wangu amekataa shule, nataka nimtafutie fani ya ufundi asiwe mzigo mbeleni

Hii ndiyo pointi sasa

KIjana aulizwe kwanza anataka kufanya kipi. Achague vitatu.

Halafu mzazi ndio achague sasa amsapoti katika kipi.

Lazima tutambue kwamba watu wengine nao wana maamuzi yao
Muulize yeye mwenyewe kua anataka kufanya nini kwenye maisha yake? Unaweza kumpeleka sehemu kisha huko napo asiweke bidii,

Kama hajui anataka nini
 
Watu kama hao wanahitajika sana, katika uzalishaji wa viwandani hasa zile kazi za kutumia nguvu.
Unaweza pia kumpeleka kwenye karakana ya uchomeleaji, gereji, useremala n.k. au kwenye mafunzo ya ulinzi; kwa ujumla zile kazi za kutumia nguvu tu.
 
Wanaandika Mzee wewe udereva umesoma wapi? Lazima uchukue notice
Notisi zipi za kabla kuwasha gari ucheki ,oil na maji na Mafuta na upepo kwenye matairi na kuchora alama za barabarani au Wakati Kwa macho tu waweza zikariri Kuna Nini kikubwa kwenye course ya udereva kinachohitaji Hadi uwe na daftari la kuandika kubadili gia mlimani,kupaki au kuovertake ? Kipi Cha kuandika notisi Kwa course ya udereva?
 
Kwanza nikupongeze kwa yafuatayo
1.upendo wako wa hali ya juu
2.akili njema ya kujua kuzuia mizigo ijayo

Pili nije kwa mada kaka huyo bado kwa umri wake mdogo usimkatie tamaa huyu tukikushauri vyema ww ndo badae itakuwa tegemezi kwake .
Naomba unijibu haya ndipo nikushauri juu ya mdogo wetu
1.kaa nae muulize anapendelea maishani afanye shughuli gani ya kulea familia yake.mtajie bajeti yako familia mwambie na yy atakuwa nayo si muda na atalipia yy je amejipangaje
2.je analewa.anavuta sigara? Ni wa ngapi kuzsliwa
3.ana kipaji chochote cha kuzaliwa

4.nidhamu yake kwenye hela yake ikoje

5.ni lazima aishi mwanza au huko?
6.unabajet kiasi gani kumsaidia?
 
Notisi zipi za kabla kuwasha gari ucheki ,oil na maji na Mafuta na upepo kwenye matairi na kuchora alama za barabarani au Wakati Kwa macho tu waweza zikariri Kuna Nini kikubwa kwenye course ya udereva kinachohitaji Hadi uwe na daftari la kuandika kubadili gia mlimani,kupaki au kuovertake ? Kipi Cha kuandika notisi Kwa course ya udereva?
Basi utapewa kitini
 
Watu kama hao wanahitajika sana, katika uzalishaji wa viwandani hasa zile kazi za kutumia nguvu.
Unaweza pia kumpeleka kwenye karakana ya uchomeleaji, gereji, useremala n.k. au kwenye mafunzo ya ulinzi; kwa ujumla zile kazi za kutumia nguvu tu.
Sahihi pia Kuna kazi kama vibarua wa ujenzi kama wabeba nzege au mizigo masokoni nk ,wasukuma mikokoteni,waosha magari na bodaboda,makondakta ,wapiga debe ,watembeza mitumba mitaani,wauza magenge,mama nitilie ,baba nitilie nk kama shule hataki kazi ziko nyingi za hao wagoma shule mtu hutakiwi kuumiza kichwa
 
Naombeni ushauri kuhusu mdogo wangu wa kiume ambaye hajamaliza hata shule ya msingi na sasa amekuwa mzigo, kwani mawazo ya kusoma hana. Nataka nimtafutie fani (ufundi) ili mbeleni asijekuwa mzigo, kumbuka ni miaka 18+.

Naombeni ushauri wa fani inayoweza kumfaa na labda pia kama mnajua chuo cha veta kinachotoa fani husika.

Location yake ni Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Musoma au Geita.

Nawasilisha
Mtafutie shamba,mpe jembe.
Km unataka mali utazipata shambani.
Mimi ninawaza tu pale mtoto wa shule ya msingi anawezaje na kufanikisha kuacha shule?

Lazima mzazi au mlezi atakuwa kawezesha hilo jambo kufanikiwa.
 
Mtoto anakataaje shule kimasihara!!

Weka Bakora, elimu at least ya form 4 ni muhimu.
 
Back
Top Bottom