RUSTEM PASHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2016
- 4,707
- 11,365
Pombe Magufuli nakushauri usisahau kuwaeleza wananchi kuwa Tanzania ya viwanda kama umeifanikisha, maana 2015 ulipigiwa kura na watu wengi kwa namna ulivyonadi sera zako, hasa iliyonivutia mimi mpaka nikakupa kura ni Tanzania kuigeuza nchi ya viwanda.
Sasa hivi sisikii ukinadi umeifanikisha vipi nchi yetu kuwa ya viwanda, kunaviwanda vipya vingapi, kama viwanda vipya vimeongezeka naamini navijana wengi watakuwa wameajiriwa huko, waeleze watanzania namna ulivyoigeuza nchi yetu kuwa ya viwanda. Maana kwa sasa tangu kampeni zianze sijasikia hata kwa bahati mbaya ukizungumzia unahitaji nchi ya viwanda.
Pia ningekushauri ujikite kwenye hoja mara nyingi, ueleze wananchi ni namna gani ndege 11 zilivyobadili uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, Watanzania niwatu wakarimu na niwaelewa naamini watakuelewa ukiwambia nimamna gani umepunguzwa umasikini wao.
Mwisho tunahitaji Nchi ya Viwanda, Tanzania ya Magufuli tunahitaji nchi ya viwanda kwelikweli.