GE2025 Ushauri Mpina: Kagombee kupitia chama chochote, utapita maana wananchi wako upande wako kwa 100%

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wananchi wanaweza kumpigia kura nyingi tu, ila anayetangaza matokeo asimtangaze yeye mshindi.
Mfumo wetu wa uchaguzi ni mbovu sana .
Kwa mfumo huu ni kheri kusiwe na zoezi la upigaji kura kwani ni zoezi la kisanii,ulaghai na kitapeli.
Uchaguzi wa 2020 walipitishwa Kwa nguvu wabunge wa CCM pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa Kwa Tanzania nzima..
Uchaguzi wa nchi hii upo chini ya RAISI yaani huyu ndiyo anachagua yupi aingie bungeni na yupi apigwe chini
 
Ndugu Retired umesahau kama kuna tofauti kati ya kupata kura nyingi na kutangazwa mshindi?​
 
Kwa hiyo upo uwezekano wa kugombea kupitia chama kingine nje ya Ccm na kuweza kushinda pasipo reforms ?
 
Afadhali mara mia magufuri alikuwa anachagua vichwa na wasomi sbb alijiamini
 
Kwa tume ipi? Kama wamemuamuli kumzuia watamzuia hata huko kwenye tume ya kutangaza matokeo. Ila mpina hakuna wa kumshinda kisesa
 
tatizo wewe haupo jimboni kwake,huyu jamaa watu wengi hawamtaki,ni mbunge mpuuzi sana hana lolote ambalo amefanya kwenye jimbo lake
 
Huyu mzanzibari anatuharibia sana nchi yetu Kwa kalazimisha kupitisha wabunge vilaza wasiojua kitu chochote zaidi ya kusema ndiyooooo hata kwenye upuuzi
 
Utaenda kumpitisha na kumtangaza???
 
Kwani yuko peke yake nchi nzima?

Wagombea ni wengi na hicho kiti sio chake milele. Wacha na wengine wapate nafasi.
 
Tatizo mfumo, hata sasa wananchi wanamkubali 100% japo ni mbogamboga ila shida mfumo ndugu.
 
Poleni sana
 
Pole sana nyumbu, hufahamu chochote kuhusu kisesa lakini uchadema chakavu unakusumbua.
 
Mpina anasumbuliwa na hulka ya asili ya kisukuma, uwezo mdogo wa kujishusha huku akiongea kwa kudhania muda wote anayo haki ya msingi ya kuweka wazi maoni yake.

Mbele ya Rais huwezi kusema 'tunakudai' wakati umezungukwa na ushahidi wa namna Rais huyo alivyofanya kazi nyingi za kuonekana katika majimbo yanayokuzunguka, huwezi kutumia lugha za kumshusha Rais mbele ya hadhara halafu wasaidizi wake wasishughulike na wewe.

Akienda huko upinzani atakutana na siasa tofauti na hizi za CCM huyu ni kada wa chama huko kwenye vyama vingine atakosa 'ukuta' wa kumlinda ambao upo ndani ya CCM.

Kwa kifupi atamalizika mapema kisiasa akienda huko kwa hoja za jazba za kisiasa. Mrema alipotea baada ya uchaguzi wa 1995 kumalizika.
 
Asiende kwengine kokote aendelee kuchapa makalio yao hapohapo mpaka somo lieleweke

Mwisho wake utakuwa bora kuliko mwanzo wake
 
Kama nimzalendo kweli awasemee watu wake kupitia NRNE huwezi kusema unasaidia kusukuma gari bovu wewe mwenyewe ukiwa umelipanda ndani nilazima ushuke uchague upande wa Haki

No reform No Election
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…