Ushauri: Msaada kuhusu tabia ya wizi iliyokubuhu kwa kijana wangu

Nenda polisi kaongee nao, ili baadae uende na mtoto wampige mjwara mzito
 
Pole Sana atabadilika tu Kuna wakt nilikuwa na tabia za hvyo vya udokoz udokoz Ila iliisha automatically Bila kujua na Wala sipendi na siwapendi wezi kbsa
 
Ndiyo maana nasema ajalibu kwa kila namna kumrekebisha tabia ikiwa ni pamoja na kufanyiwa maombi. Kamwe lawama hataziepuka. Akimrudisha atalaumiwa kuwa hataki kusaidia au kuishi na ndugu. Akipatwa na matatizo kutokana na tabia yake atalaumiwa kuwa ameshindwa kumsimamia. Hivyo lawama haziepukiki.
 
Hana shida, ni tatizo la kiroho zaidi. Dozi iliyopo kanisani kwenu bado haimtoshi. Jaribu kumpeleka kwenye makanisa ya Walokole akaombewe. Popote pale. Kwa kuanzia, unaweza ukampeleka kwa Bull dozer Mwamposa au kwa Nabii Suguye
Usipofanya hivyo inabidi ukae standby siku moja kufikishwa Polisi ukiwa una kesi, wewe kama mtuhumiwa! Mpeleke kwa Walokole. Mimi ni mmoja wao, naelewa ninachokueleza hapa
 
Mkuu swali ni je akiiba pesa anafanya nayo nini?Ukiweza kujua matumizi yake ya pesa unaweza jua uanze kumsaidia vipi.
 
Pole Sana atabadilika tu Kuna wakt nilikuwa na tabia za hvyo vya udokoz udokoz Ila iliisha automatically Bila kujua na Wala sipendi na siwapendi wezi kbsa
Kubeba laptop, simu nafikiri dogo, kahama kwenye udokozi kawa wa next level!
Kuchukua buku buku 2 ni tofauti na kudondoka na simu za watu unaziuza bei chee!
Yaani kapitiliza!
 
Ana baba ake muondoe angekua wako ningekushauri kitu ila huyo utapata lawama
 
Nimeongea na dogo hapa sasa hivi nimemwambia nimrudishe kwa baba amekataa kabisa analia anadai nimsamehe harudii tena lakini alishaomba msamaha mara nyingi Sana

naumia Sana nampenda huyu ni damu yangu kabisa.
Huruma inakuponza mrudisheeee utajutaa kanafiki hakoo
 
Ameen ameen afadhali bora lawama kuliko fedheha
 
Tupe mbinuaana bado tunazaa hatujui tutabeba nini matumboni
 
Pole sana
 
Mkuu swali ni je akiiba pesa anafanya nayo nini?Ukiweza kujua matumizi yake ya pesa unaweza jua uanze kumsaidia vipi.
Alisema huwa anaenda kula chips sijui soda na vitu vingine.
Ilihali nyumbani nilikuwa nampa vyote.
 
Tayari nilishampeleka kwao
 
Alisema huwa anaenda kula chips sijui soda na vitu vingine.
Ilihali nyumbani nilikuwa nampa vyote.
Good sasa kwa kuanza,mwambie akitaka chipsi akwambie au uwe na tabia ya kutoka nae na kwenda sehemu ya chipsi unamnunulia mnakula mnashiba then akija nyumbani unampa tena chakula.Mfanye awe rafiki yako kwa kuanza ili ufahamu kama ana tatizo la kleptomaniac au ni tattizo la malezi huko kwa ndugu yako kwani kwa assessment yangu mpaka ndugu yako amemleta kwako kuna shida kwenye mji wake. so do what you can.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…