Ushauri: Mtendaji Kata na Mratibu Elimu Kata ya Kifuru(DSM). Kuhusu uzio Shule ya Msingi Kifuru, wafichieni aibu hawa Watoto na walimu wao

Ushauri: Mtendaji Kata na Mratibu Elimu Kata ya Kifuru(DSM). Kuhusu uzio Shule ya Msingi Kifuru, wafichieni aibu hawa Watoto na walimu wao

Google Diggers

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2015
Posts
944
Reaction score
1,138
Ni ushauri tu. Na Kawaida unaweza ukauchukua na au ukauacha.

Nilipita kuelekea Mbezi nikitokea tabata. Baada ya eneo la Kinyerezi jijini DSM, utakutana na Shule ya Sekondari Kisungu, Hawa wameficha japo kwa uchache eneo dogo tu aidha Watu wasifanye njia, ama macho ya wapita njia na kadhalika...wameweka uzio wa mabati. Kwa kuwa hii ni shule na masuala ya kitaalamu yanaendelea humo wamejiongeza.


Ukisogea kilometa moja hivi au zaidi utakutana na Shule ya Msingi Kifuru. Kituo cha daladala kinakuonesha kuwa kuna shule hapa na walimu wamekaa nje na wanafunz wanasoma aidha watoto Hawa wanakaa chini Kwa hiyo wanakuwa wamebeba mifuko ya sandarusi kwa ajili ya kukalia kama kiti na meza

Wakati haya yanaendelea na walimu wanaendelea na kazi kama kawaida wote tunajua wanaendelea na malezi ya watoto.

Mimi binafsi yangu sikupendelea sana muonekano, kukaa chini watoto sio taswira nzur, lakini pia kuona kinachafanywa na walimu si afya kabisa. Kwa sbab mnawapa nafasi MIDIA kuwaumbua wkt wa kutekeleza kazi.

Ukiwa kama unarudi nyuma Kuna petrol station inajengwa, huyu muwekezaji anamabati anayatumia Kuziba sheli yake isionekane wkati wa ujenzi, ni taratibu za ujenzi. Lkn huyu mnaweza mkamuomba baada ya zoez la ujenzi kukamilika awasaidie yale mabati muweke uzio hapo stend ya daladala Ili mtenganishe masuala ya kijamii, wapita njia na Shule.

Wekeni geti la mabati hayohayo itasaidia usalama wa Watoto pia.


Yule bana si ajabu akawasaidia kuweka msingi na kuipandisha walau koz kadhaa za tofali itategemea mtakavyomuandikia kiupole na unyenyekekevu.

Mwisho jengeni tabia ya kuwatumia watu, wawekezaji wanaowazunguka kuchangia maendeleo ya elimu Kwa watoto.

wafichieni aibu hawa Watoto na walimu wao​


Mungu ibariki Tanzania. Ili kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom