Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Ni wazi kuwa Lissu amekuwa mwanaharakati wa kutetea haki za wananchi kwa miaka mingi, pia ni wazi kuwa kwa sasa yeye ndiye mwanasiasa pekee wa upinzani mwenye uwezo wa kumtikisa Magufuli.
Lakini kuna mambo machache ningependa kumshauri ayazingatie atakavyoendelea na kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
1. Aache kumshambulia Magufuli binafsi
Naamini kuna watu wengi tu wamemshauri juu ya hili, ni muhimu sana kulizingatia hili. Ni vema kuielekezea mashambulizi serikali kwa ujumla na chama cha CCM badala ya kumshambulia Magufuli.
Hata Magufuli akitaka kurusha vijembe upande wa pili mara nyingi hua hataji majina ya watu. Anaepusha mgongano wa hoja kugeuka kuwa ugomvi binafsi.
2. Ajikite kwenye matatizo yanayowagusa wananchi wengi
Japo kiubinadamu ni ngumu sana kufanya hili ukizingatia yeye binafsi alivyoteswa na kulengwa moja kwa moja na utawala huu lakini ajitahidi kuachana na 'personal vendetta' dhidi ya serikali akiwa jukwaani.
Watu hawakuchagui ili ukatimize hasira zako bali ili ukatatue changamoto zao. Kuna mengi ya kuongelea kila sehemu, watumishi, wakulima, wafanya biashara, wahitimu wa vyuo n.k
Lakini pia kuna ukatili wa polisi na kuminywa kwa demokrasia na uhuru, bila kusahau sheria na kanuni za kishenzi za awamu ya 5.
3. Ajizuei kutumia lugha kali
Najua Lissu ni bingwa wa kutibua nyongo za wapinzani wake, namshauri sasa kwakua anawania ofisi ya juu kabisa hapa nchini basi ajitahidi kuongea kama rais mtarajiwa. Lugha za kejeli na kukashifu hazifai kutolewa na kiongozi mkuu wa nchi.
Ni hayo tu machache, natumaini ujumbe umefika.