Ushauri Mwigulu kuwa makini sana kwenye mawasiliano

Ushauri Mwigulu kuwa makini sana kwenye mawasiliano

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Bashe ndiye waziri anayeongoza kwa kuwa na mawasiliano mazuri lakini Mwigulu mwana Ilboru mwenzangu nampa nafasi ya mwisho. Mwigulu ndugu yangu hii serikali ni ya viongozi wapole na wataratibu sana hasa Raisi Samia na Makamu wake.

Makamu wake ambaye alikuwa waziri kama wewe na nafasi hiyo hajawahi kuonyesha dharau ya waziwazi hata kama unasema una PhD.

Sisi ambao tunajua kuhusu PhD tunajua huwezi kupata PhD bila kusaidiwa wakati ukiwa waziri huo ndiyo ukweli hivyo acha mara moja kutumia eti kwasababu una PHD lkuona wabunge wengine au wadau wengine kama vile umewazidi.

Lakini ushauri wangu unaenda mbali zaidi hili la kijigamba gamba pasipo ulazima linaonyesha utoto wako ambao unaweza hata kukuzuia nafasi na vyeo vikubwa zaidi huko mbele. Jifunze kutoka kwa Raisi na makuamu wake jinsi ya kwenda juu hasa kwenye jamii ya Watanzania.

Lakini kama unavyojua wahitimu wa Ilboru hatuna utamaduni wa kujigamba kitoto kitoto hivyo hata kama tunamafanikio makubwa.

Sijapenda hili na jirekebishe haraka kwa manufaa yako, ya serikali na jamii kwa ujumla. Haya ni mawazo yangu kwako ya wazi.

Najua kabisa utanipata. Ongea wakati hauna hasira.
 
Huyu jamaa babu wa babu yake atakuwa ni mhaya.
 
Ni kweli kabisa rais Samia ni mnyenyekevu sana. Natamani sana niwe kama yeye.

Lakini baadhi ya wasaidizi wake Wana kiburi.
 
Ukipayuka sana hata hekima na busara hukukimbia, maana aliongea mpaka akasahau kaongea nini.
 
Ana psychiatric problem
Ego inamsumbua
Hiyo piechidii aliitafuta ili aringishie wenzake mjengon
Mbona kuna ma profesa wapo kimya??
 
Mwigulu ndiyo mwenye nchi. Mtamfanya nn enyi wadanganyika??

Aliwaambia asiyetaka kulipa tozo ahamie Burundi, hamjataka kwenda.

Na Sasa amewachana laivu wabunge vilaza waliopitishwa kwa nguvu ya dikteta Magufuli kuwa hawana sifa ya kujadili uchumi, bali wajadili uganga wa kienyeji tu.
 
Back
Top Bottom