Ushauri na Mbinu Mbalimbali Kuhusu Uendeshaji wa Biashara ya Kuosha Magari (Car Wash)

Nataka kuanza biashara ya car wash but nlitaka kujua
1. Kodi ya eneo la biashara
2. Malipo ya wafanyi kazi yapo VP
3. Bei unacharge VP
4. Faida kwa siku inaweza simama ngapi

UZOEFU WANGU: VIFAA NA RASILIMALI WATU

Namiliki Car Wash huku kunduchi karibia na Eneo la Jeshi.

--Kodi ya Eneo--150,000 tshs. Na hii ilishuka kutoka 500,000 tshs wakati nafungua. Kwasababu mzunguko wa biashara ulikuwa mdogo. Bei mara nyingi ni maelewano.

--Malipo ya wafanyakazi? Na walip kwa gari. Gari tunaosha tshs 10,000. Ya kwao asimilia 30. Hesabu inatoka baada ya siku kuisha

--Bei--tunatoa huduma ya kuosha gari ''FULL'' au ''KUOSHA BODI'' na tunafanya service ya magari pia. Gharama zake?
KUOSHA FULL--10,000/=
KUOSHA BODI--5,000/=
CAR SERVICE---10,000/=
KUOSHA CARPET--10,000 mpaka 30,000

--Faida inategemeana na:
---Huduma unazopanga kutoa
---Mauzo ya vifaa vya spea--Engine Oil, Oil filter, Oil Coolants, Brake fluid, Air Filter
---Mzunguko wa wateja
---''Marketing''
---Ufanisi wa kazi...Ukiosha gari vizuri wateja watarudi
---Usalama wa mali za wateja. Kuna wafanyakazi ni wadokozi. Wakiiba hela wateja wanazoacha kwenye gari wateja hawarudi tena

Ni mchanganyiko wa vitu hapo juu vinavyochangia hela utakayotengeneza.

Gharama utakazotumia?
--Unahitaji mashine ya ''compressor'' au ''presha''
--Unahitaji ''gun'' zile mashine zinatoa maji
--Unahitaji ''vacuum cleaner'' kwa ajili ya kutoa vumbi ndani ya gari
--Unahitaji mashine ya upepo
--Unahitaji ''polish'' kwa ajili ya kung'arisha dashboard na sehemu za ndani ya gari
--Unahitaji tenki la maji
--Bili za dawasco
--Kodi TRA
--Umeme
--Kodi ya Eneo
--Usafi--ufagio, na dustbin
--Usimamizi wa hali ya juu
 

Bingwa nimetokea kuheshimu sana post yako. All the Best. Ni nadra sana mtu kufunguka hivi. Watu chuki na wivu sana hata msipofahamiana.
 
Mkuu bonge ya point, but kuna uzi huku unahusu car wash, mods wangeuunganisha na huu hakika watu wangepata madini

Sent from my TECNO CA6 using JamiiForums mobile app
 
Oyaa [emoji23] [emoji23] naenda kusevu kwenye Email yangu hii.
 
Habari wadau,

Nimefanikiwa kupata capital na ninataka kufungua car wash sites mbili ninahitaji kujua yafuatayo:
1. Vifaa vya kutumia (capital equipments)
2. Sehemu ya kuvipata kwa bei nafuu na ubora unaoridhisha.
3. Je biashara inalipa kwa hapa Dar es Salaam?
 

Kila la kheri boss wangu!
 
Nina 17millions
Sehemu nzuri wilaya ya Ilala na Kinondoni. Ukipata maeneo ya Mlimani City kwendea mpaka mwenge itakuwa vizuri pia, maaeneo ya New Bagamoyo Road itapendeza na maeneo mengine inabidi uka survey sana.

Mtaji mkubwa unaweza kufosi strategic area kama hizo.

Kwa msaada wowote nicheki Free Anytime nitakusapoti.
 
Asilimia kubwa ya maeneo yenye bar zinazojaza....atapiga pesa sana
 
Car Wash is just a hustle, it ain't a sustainable business idea.

Successful people strive to build businesses and never rely just on hustles.

Mfano: Usitegemee Car Wash inaweza kuwa Conglomerate hata siku moja.

It's a hand to mouth business.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…