Upara sio ugonjwa so hauwezi kuwa na dawa. Ni maumbile. Kama vile walivyo watu wafupi, watu weusi, weupe, wenye nywele kama kachumbali, kipilipili, wenye sura ya duara, wenye sura ndefu, wenye matiti makubwa kama begi, wenye matiti madogo.
Haya ni maumbile. Kinachokusumbua ni kulazimisha ufanane na watu wengine ili uvutie sasa sijui kwa faida gani.
Hapa ndipo ule msemo wa jikubali unapokuja kutumika. Yaani kabla haujataka kulazimisha ufanane na mtu jitazame wewe upoje ili kama kuna features mnafanana unaweza mcopy ila kama haifananii kwa asilimia 100% then tafuta mtu unayefanania nae ambaye anapendeza then copy style yake.
Unaweza kubakia na upara wako na nywele za ubavuni au unaweza nyoa upara kabisa kama unakichwa kizuri cha kunyoa na ukaenda vizuri na aina fulani za mavazi.
So kaa upya ujidesign muonekano wako. Achana na kujiwazia kuwa una dosari inayotakiwa matibabu.