Lethergo
JF-Expert Member
- Aug 7, 2023
- 6,534
- 11,421
Wakuu!
Huu ni ushauri wa kuilinda pesa yako na sio simulizi za 'Chuma Ulete'.
Pesa ina nguvu, hapa nitazungumza na wale wote wanaotaka kuimiliki pesa. Pesa ninayoizungumzia zaidi hapa ni pesa ya Sarafu (Coin) ambayo inatumika katika maluweluwe mengi sana.
Pesa ya Karatasi au Noti sitoizungumzia sana ila nitaigusia kidogo tu kuielezea.
Nimejifunza kwamba wapo watu hutumia Pesa kupata Pesa na hutumia Pesa kuletea watu wengine mabalaa, mazonge, nuksi na mikosi.
Nakumbuka nikiwa mtoto mdogo nilikua napenda sana kuokota Sarafu njiani (Coin). Yaan ile asubuhi nikiwa naelekea Shuleni njiani nilikua nabahatika kuokota Sarafu za sina tofauti yaan shillings 5, 10, 20, 50, 100, kwa kweli kwa kua nilikua sijui na sikuwahi kukatazwa nilikua naziokota zile Sarafu na kuzitumia.
Kisha kesho nawaza naweza nikaokota zingine nikijihisi mwenye bahati sana. Kumbe sikujua nyuma ya pazia nini kinaendelea kwenye hizi Sarafu (Coins) zinazotupwa na kuzagaa.
Sasa hata hapo na kuendelea kukua nimekua nikiokota Sarafu mpaka za Nchi za kigeni km Rupees za India, pesa za Indonesia, Japan, nk nikawa nazihifadhi sababu sina pa kuzipeleka bila kujua hizo Sarafu (Coins) zilikua na maana gani. Ila baada ya kujua sikuhizi mimi siokoti Sarafu yoyote.
Tuendelee.....
Baada ya kukaa muda mrefu na kujiuliza maswali mengi kuhusu fedha niliwahi kupata safari moja kwenda Mkoa mmoja wa Kanda Ya Ziwa (sitoutaja) nikitokea Dar.
Nikiwa kwenye ule Mkoa kuna kitu nilikiona ila kutokana na imani yangu ya Dini niliyonayo sikuona km ni shida kwangu nikawa nafanya kitu ambacho nilitakiwa nisifanye bila kujua.
Ilikua hivi.....
Mara nyingi nikiwa kwenye matembezi yangu, kwa kua mimi napenda sana kutembea kwa mguu kuliko kitu chochote hususani nyakati za jioni na asubuhi, naweza kutembea umbali mrefu kwa mguu bila kuugua wala kupatwa na shida yoyote ya kiafya.
Sasa basi siku moja nikiwa kwenye matembezi yangu km kawaida nikakutana na Bibi mmoja mimi simjui na yeye hanijui, Bibi yule akakaanza kunichangamkia km vile tumewahi kuishi pamoja au km vile ananifahamu muda mrefu nilipotea sasa nimerudi sio kawaida, katika maongezi yangu na yule Bibi akatupia neno 'Nipe hela ya mafuta basi leo sina hela Baba yangu', nikashtuka kidogo kwa mshangao na yeye akawa km ananishangaa ila kwa kua siku hio nilikua na hela lakini sikua na mategemeo kwamba nitakutana na mtu akaniomba msaada wa Pesa (napenda kuishi ndani ya budget yangu), mimi ukiwa na shida sikupi kile nilichokiwekea malengo nakupa kile ambacho ni extra yaan hakina cha kufanyia.
Basi Bibi nikamkatalia kua leo sina kitu lakini nikamwambia labda siku nyingine.
Ikapita km wiki moja nikaja tena nikakutana tena na Bibi yule yule njia panda ile ile akaanza tena story zile zile na maongezi yetu yakawa ni yale yale akagusia anataka hela ya mafuta na mkononi ana kamfuko cha mboga ila hela ya mafuta akasema hana, kwa jinsi alivyochangamka yaan tunaongea tunacheka kabisa, siku hio kiukweli nilikua sijabeba chochote mfukoni nikamwambia Bibi leo sina kabisa tuangalie siku nyingine. Baada ya hapo nikatembea na Yesu (Biblia) yaan nikaondoka nikamwacha Bibi aakinishangaa huku anatabasamu.
Hio ikapita nikakaa km wiki 2 mbele tena sasa siku hio ndio nikawa nina hela nyingi angalau mpaka extra yaan kuna hela za budget zangu na kuna zingine nje ya budget zinaelea tu hazina cha kufanyia ndio nikatembea nazo katika hizo hela mimi napenda kutembea nazo ni Sarafu yaan Coin ninazopatiwa chenji siwezi kuzitupa.
Basi katika tembea tembea mara paap Bibi yule yule njia panda ile ile kanisimimamisha sasa hii inakua mara ya 3 nasimamishwa na Bibi yule yule mwenye bashasha nyingi zile zile na uchangamfu ule ule uliotukuka na story zetu ni zile zile na mazungumzo yetu ni yale yale kwamba 'Naomba hela ya mafuta nimeishiwa hela Baba yangu'.
Bahati nzuri siku hio nilikua na Sarafu nyingi mfukoni nikavuta Sarafu moja ya 500 nikampa Bibi nikimwambia hii hapa Bibi nimekuahidi sana leo nimekupatia. Bibi akaachia tabasamu moja la furaha sana akinitazama bila kunimaliza. Sababu nilikua nimechoka kuahidi kila ninapokutana nae kwamba leo sina tuangalie siku nyingine ikawa hivyo.
Lakini kabla sijaenda kwenye maelezo ya msingi wa uzi huu nitagusia jambo lililotokea miezi 2 hivi kabla sijaenda Mkoa huo tajwa hapo juu.
Nikiwa Dar, kuna siku moja nilienda Posta kwenye mishe zangu kuna barua nilikua nimeenda kutuma siku hio mafuta (Pesa) yalikua ya kutosha (tukutane sheli), watu wa viti virefu watakua wamenielewa.
Nikiwa bado nipo Posta nilikutana na mtu mmoja kijana mtanashati maeneo ya Mnazi Mmoja, amevaa kwa kupendeza sana alikua kijana alivalia suruali ya khaki na shati la dark blue huku chini mguuni ana moka nyeusi, akanisogelea akaniambia kwa utulivu kabisa 'brother nina shida kuna sehemu nafika nimepungukiwa nauli km 600 hivi naomba unisaidie'.
Mimi sababu mafuta (Pesa) nilikua nayo na nakumbuka nilipata Chenji kwenye gari la mwanzo wakati wa kuja Posta, sikuweza kukosa 600 ya kumpa, kweli nikaingia mfukoni nikampa 600. Jamaa akashukuru kidogo akapotea na njia sikumuona tena.
Turudi kwenye Mkoa nilioenda nikiwa huko km kawaida yangu ya kupiga misele yaani kutembea kufanya utalii wa ndani nikaingia barabara moja nayo ni njia panda hapo nikamkuta binti mmoja yupo na katoto akawa amenisimamisha 'kaka samahani' mimi nikajibu 'bila samahani' basi akawa analalamika kale katoto kanaumwa kamekosa hela ya dawa na hela anayoitaka ni 200 tu apate walau panadol au paracetamols sio hela kubwa mimi kwa kua mafuta (Pesa) nilikua nayo ya ziada (extra) haina cha kufanyia, nikatoa 200 tatu jumla 6000 nikampa nikatembea na njia.
Sasa katika kujifunza hapa na pale nikaja kuambiwa Bwana wewe hela unayoombwa na mtu njiani popote pale unapokua popote pale unapoenda, mtu ambae anakuja kwa kukuchangamkia tu humjui hakujui hamjawahi kua marafiki na hamfahamiani hio maana yake umeingiliwa au umevamiwa kwenye himaya yako ya Pesa unahitaji ulinzi.
Hapa ili unielewe naomba utulie vizuri maana kuna ile namna umekutana na mtu tu akakuomba Pesa unayo ila kuna kitu ndani kinakukataza usitoe ukasema hapana huyu simpi ukamwambia sina ukapita hivi, hii maana yake wewe ulinzi wako upo imara na haingiliki ila ikitokea umetingishwa kidogo huyo umeingia mfukoni umetoa wewe ulinzi wako mdogo jichunguze.
Tuendelee....
Nikaambiwa Bwana hela unayompa mtu njiani ambae amekuomba hio hela iwe 100, 200, 500 hizo Sarafu ukiombwa ukampa basi jua huyo mtu anaenda kufanyia mambo yake ambayo wewe huyajui ila sio ya wema yaani ni mambo ya gizani.
Na baada ya kumpa hio hela wewe mambo yako km yalikua yamenyooka basi yarakuendea kombo utaona hela yako inakupotea tu yaani unapoteza hela zinakokwenda haujui mwisho unabakia hauna hela umeishiwa.
Nimekua nikisoma mazonge mengi ya watu humu jf baadhi wamekua wakisimulia kuhusu kufirisika ndio nikabidi nijifunze ni nini kinachosababisha yote hayo, sasa kwenye kujifunza nimegundua ikiwa wewe ulifirisika au uliwahi kufirisika basi kuna namna uliitupa Pesa yako kwenye mikono isiyo salama ikaenda kufanyiwa mambo mambo gizani na kwa kua wewe ulinzi wako ni mdogo kwenye Pesa ukajikuta unaanguka haraka sana na kufirisika kabisa ukabakia mtupu.
Tuje kwenye Noti...
Unaambiwa Pesa hutolewa kwa mkono wa kulia na kupokelewa kwa mkono wa kulia.
Mtu yoyote akikupa Pesa kwa mkono wa kushoto na wewe pokea kwa mkono wa kushoto, usijifanye mjuaji umepewa Pesa na mkono wa kulia wewe ukapokea na mkono wa kushoto au umepewa na mkono wa kushoto ukapokea na mkono wa kulia kisha ukaichanganya hio pesa uliyopewa na mkono mwingine na Pesa nyingine, litakukuta jambo.
Tukizungumzia Noti kuna mabwana huja kwenye maeneo ya biashara ila wakiwa na lengo la kuja kuchukua 30% ya pesa za mauzo yako ya kila siku kwa nguvu za gizani, kwa hio wakifika wao watachofanya ni km amebeba box mkono wa kulia (mkono wa kutoa) atakupa pesa na mkono wa kushoto (mkono wa kupokea) ukiipokea na mkono wa kulia tayari umeingia KING, kifuatacho utaichanganya ile Noti na Noti zingine na kumpa Chenji (kosa).
Baada ya kumpa Chenji katika mauzo ya siku utakuja kugundua km wewe ni mwepesi hauna ulinzi wa Pesa basi utagundua km mauzo ya siku hio yalikua 10,000 basi una 7,000 za mauzo na haujui 3,000 ilipoenda yaan yule mtu wa 30% ameshaingilia himaya yako ya Pesa na yeye anachukua asilimia zake kaondoka na 3,000.
Kwa kuhitimisha, Pesa yako ikiwa upande wako ina nguvu sana iwekee ulinzi usiitapanye, usiimwage mwage, usiitoe bila nidhamu, usiitupetupe ovyo ovyo, usiitoe kwa watu usiowafahamu, usiitoe kwa watu usiowatambua, usiitoe kwa watu usiokua na mahusiano nao, usiitoe kwa watu ambao hawana uhitaji wa kweli bali wanaitaka kwa kwenda kutumia kwenye mambo yao mengine huko gizani. Iwekee pesa yako ulinzi.
Suluhisho ni nini, ukikutana na mtu akakuomba msaada mfano anakwambia ana shida ya nauli anaelekea sehemu fulani na amepungukiwa nauli usimpe Sarafu au Coins zako, wewe cha kumsaidia ndugu yangu hio hela usimpe mwambie twende kwenye gari unalotaka kupanda ukifika mwambie apande mwite kondakta wa gari mpe nauli mwambie nimemlipia yule pale mpe tiketi yake, ukimaliza kufanya hivyo ondoka umeshamaliza kutenda wema.
Ukikutana na mtu uumfahamu akakuomba 500 au 1000 ya chakula amepungukiwa usimpe Pesa ya Sarafu (Coins) wala Noti, wewe km unayo pesa msogeze mgahawa wa karibu mnunulie chakula ale, utakua umetenda wema wako kwa kikomo, pesa yako inabaki na ulinzi.
Ukikutana na Bibi anakwambia ana shida ya mafuta umpe Sarafu zako, usimpe Sarafu yoyote, wewe mchukue nenda nae mpaka dukani nunua mafuta anayohitaji mpe, kisha utakua umetenda wema kwa kiasi chako na pesa yako itakua imebakia na ulinzi wako.
Ngoja niishie hapo kwa leo.