Ndrugu zangu wapendwa,
Nimefurahishwa sana na michango, maoni, mitazamo, ushauri, elimu, ufahamu na uelewa wenu juu ya bandiko langu muhimu la namna nzuri na bora ya kumweleza mwenzi wako kwa jambo Fulani haliko sawa na asijiskie vibaya.
Harufu ya tupu na maeneo mengine mwilini ni sehemu tu ya mambo mengi yanayofanya ndoa na mahusiano mengi hivi sana kuwa legevu, na yaliyokosa furaha, uelekeo na uhai.
Nikiri tu, mimi ni mdau wa muda kidogo kwenye masuala ya ushauri na usuluhishi katika changamoto za ndoa, uchumba sugu na mahusiano.
Suala la usafi linahatarisha Uhai, amani na furaha katika ndoa, chumba na mahusiano mengi....
wamama na wadada wanalalama waume au wachumba zao kutoshiriki nao tendo la ndoa kwa muda mrefu.
Sababu ikiwa ni ulevi kupindukia, visingizio vya uchovu, lakini pia uchafu uliokithiri mathalani harufu kali ya pombe,sigara na ugoro, harufu ya kikwapa, miguu, pua na uvivu wa kuoga au kufanya usafi wa mwili.
Nimeona kwenye koment mtu amesema harufu hadi kwenye pua nimeongeza chumvi.
Pua zinatoa harufu kali sana, na inatakiwa kuzisafisha kwa maji safi kila unapooga. Unaziba pua moja na kufanya kama unapiga chafya kisha unamaliza na nyingine.
Mtu asie safisha pua akipiga chafya lazima utaskia harufu kali mbaya sana. Na huenda unanuka pua mwenzie anakuvumilia tu.
wababa nao wanalalama sana kwamba wamama hawaogi, tupu zinatoa harufu kali mbaya hiyo hamu ya tendo utaipata wapi?
hawanyoi huko chini, nywele zinanuka, ukimwambia bendi down harufu ni kali zaid n.k.
So,
Ndugu zangu,
kwa Kuhitimisha lakini sio kufunga mjadala, tujitahidi sana kuwa wasafi. Sio tu tukiwa kwenye ndoa, tuwe wasafi wakati wote ni muhimu sana.
Tusijibweteke na kujisahau kwenye ndoa au mahusiano na kuacha jambo muhimu kama hilo.
Safisha tupu vizuri wote akina baba na mama, ondoa nywele zisizotakiwa, safisha kinywa, safisha makio, nywele zenye harufu, pua, safisha chini ya matiti kwa akina dada, safisha mfereji ulotenganisha kalio zako, kalio huifadhi harufu kali na mbaya ya kinyesi hususani unapojamba, safisha miguuni, safisha kwapa, meno, macho mara kwa mara na hauta kua kwazo kwa mwenzie.
Mfanye mwenzi wako rafiki na mshikaji wako wa karibu sana na hiyo ndio njia rahisi zaid kuitumia kumweleza mwenzi wako kwa jambo fulani si zuri na asijiskie vibaya.