Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Kama ni hivyo sasa itabidi tununue na ma tool box.....ninachojua mimi nikubadilisha Tyre tu
Sure.. Jinsi unavyokaa nayo na unazidi kuizoea jifunze kufanya baadhi ya vitu mwenyewe.. Itakusaidia sana kupunguza gharama janjajanja..!

Kama kwenye ndoa.. Ukishakaa muda mrefu baadhi ya kesi hakuna kwenda kwa wakwe kushitaki.. Mwenyewe unakuwa Mh. Jaji..!
 
Nilishangaa kabla ya kuwasha break ilikuwa loose! Nikapump ikajaa, nilipowasha ndiyo hiyo haikuzima. Kujaribu kukata kushoto ikawa ngumu. Kama kawaida sikulazimisha nikarejesha kwenye nyumba yake. Nini kifanyike?
Ni,gari gani,kwanza?

Badili oil ya dif kwanza/transfer case kama imechoka. Kama haijachoka basi tia tu mashine ya Diagnosis.
 
Nilishangaa kabla ya kuwasha break ilikuwa loose! Nikapump ikajaa, nilipowasha ndiyo hiyo haikuzima. Kujaribu kukata kushoto ikawa ngumu. Kama kawaida sikulazimisha nikarejesha kwenye nyumba yake. Nini kifanyike?

Mkuu zima switch ya central lock ya 4WD
 
Sijui chochote kuhusu Oils za Atlantic ila BMW najua inataka Castrol na kwenye mfuniko wa engine Oil wamendika.
Mkuu Castrol waliingia mkataba wa marketing na BMW kuwapa promo. Mkataba umeisha, sasa hivi huwezi kuta BMW mpya imeandikwa castrol, cha msingi cheki specs tuu, mfano N52B25 inakubali BMW LL-01: 0W-30, 5W30, 0W-40, 5W-40, depending na mazingira. Kwa bongo 5W-40 itapunguza leakage nyingi sana. Brands depends choice yako, kama Liqui molly, Mobil, BMW Oil, Shell, Total, Atlantic, Castrol, Puma, etc. Binafsi natumia Atlantic Oil, haijawahi niletea changamoto kwenye gari zote.
 
Mkuu naomba nitumie na mimi namba ya admin inbox. Asante.
 
Ukitegemea dashboard iko siku utakaanga injini. Hata ndege inachekiwa nje.
 
Ukitegemea dashboard iko siku utakaanga injini. Hata ndege inachekiwa nje.

Usifananishe ndege na gari, taratibu zake za kiusalama ni tofauti sana na kila mtu anajua kwa nini.
Kiuhalisia asilikia 98 ya watu hawafanyi hizo checks kwenye gari kila siku, practically its almost impossible. Wanaoweza hiyo labda ni watu ambao kazi ya ni udereva, gari ndio ofisi yake, hata akipaki tu kidogo unaona hadi anaifuta futa.

Atakaangaje engine akitegemea warning lights, tena gari za Europe??? Temp, oil levels, tyre pressure, sensor malfunctions vyote unaona.
In fact hata gari za mjapan siku hizi zina taa kibao tu.

Nasisitiza tu, kukagua gari physically ni muhimu kila unapopata nafasi
 
Kuna baadhi ya vitu inabidi mmiliki ujiongeze. Mimi gari yangu mambo ya oil nafanya mwenyewe tu napoza elfu 10 kwa ajili ya spana na kupandisha gari juu..
 

Superb!
Ila Castrol ndio imekua Puma baada ya uwekezaji au maana naona kuna containers za Castrol zimebadilika branding yake?

Atlantic nawaelewa sana maana tangu nianza kumiliki viusafiri BMW anakula Atlantic, Mjapani anakula Castrol (zamani ikiitwa BP).

Tofauti na brand hizo siweki[emoji3]
 
Kuna tatizo saana kwenye kuchagua oil sahihi kwa magari used. Mara nyingi kwa gari kama lako, oil recommended inakuwa yenye "viscosity" ndogo. Ila shida iliyopo ni kujua kama mtumiaji wa mwanzo alikuwa anatumia oil ya hivyo ama la.

Kuna kitu kinaitwe "service/maintenance history". Kwa baadhi ya gari tunazoa Japan huwa inakuwepo. Sema imeandikwa Kijapan. Hii ni muhimu saana. Maana kama mtumiaji wa mwanzo alitumia oil ya viscosity kubwa, wewe ukitumia ya viscosity ndogo lazima ipungue mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…