Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Kuna gari zinakunywa oil mkuu...
 
Toyota ni wife
 
Hao ni Waturuki au Walebanon. Pamoja na huduma nzuri, bei zipo inflated sana. Sema ndiyo hivyo, wanawakamata madon kama wewe boss.
 
Bila shaka ni yule wa karibu na HK Hospital! Yaani hawa jamaa ukienda na vitu vyako, wananuna!

Nishasema humu, kama una Euro make, inabidi ujiongeze haswa kwa suala la kuijua gari yako, nini inataka na wapi utapata vifaa na lubricants. La sivyo utageuzwa gari la mshahara!
 
BMW recommends getting your 2021 BMW X3 oil & filter changed every 3,000-5,000 miles for conventional oil. Synthetic oil commonly should be changed every 12,000 - 15,000 miles.

Nimeitoa kwenye mtandao.
 
Hiyo ina engine ya N52B25 weka Castrol Oil 5W30 Fully synthetic, Ujazo ni Lita 6.5 na siyo lita 8.
Hili ni tatizo jingine la watu wenye Euro makes, na wasiozijua gari zao. Mafundi wengi wamezoea gari aina ya SUV zinawekewa engine oil lita 8 na kuendelea. Kwa mfano, XC90 inaingia lita 5.9. Fundi anakwambia humu inaingia lita 8 kwa kuangalia ukubwa wa engine! Kama hujui gari lako, unakubali na kuzidishiwa engine oil. Mwishowe “engine system service required” message inatokea kwenye dashboard!
 
Blaza pita njia yako na mm acha nipite kule nilikozoea hata kama napigwa acha niendelee kupigwa as long as haikuumizi
Cha msingi ni kama walivyosema wadau humu, jitahidi ulijue gari lako. Fanya tafiti ya wapi utapata vifaa na kwa bei gani. Ingia kwenye online fora za watu wenye gari kama lako. Cheki kazi za mafundi wa sehemu mbalimbali duniani Youtube n.k. Ukilijua gari lako vyema na utakapopata vifaa bora na kwa bei halisi, huwezi kupigwa hata kidogo.
 
Pia oil recommended kwa BMW ni Castrol hata kwenye mfuniko wameandika. Kuhusu grade hapo ndio itategemea na aina ya engine.
Castrol Ni oil? So Castrol yoyote unaweka kwa BMW yoyote bila kujalisha viscosity yake?🤔 Wanachofanya Castrol Ni Kama total na kampuni zingne wanatengeneza oil kwa viwango tofauti mfano 5w 30 ama 20w 30 kama total na kampuni zingne sasa ukisema Castrol ndo oil recommended Bado sijaelewa
 
Hebu pitia post zote nilizomquote huyo jamaa. Maswali yote uliyouliza hapa yamejibiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…