Nimekusoma kwa makini kabisa, na nimegundua haya:
1: Wewe bado unampenda sana huyo mwanaume, na bado hujaamini yaliyotokea. Bado una tegemeo kuwa kuna siku atabadili mawazo, aje akuombe radhi ili mlirudiane.
2. Huyo mwanaume ''anakupenda'' kwa sababu ya uchakarikaji wako, haiba yako na nidhamu yako lakini humvutii sana kimwili/kimapenzi. Kimapenzi bado yuko kwa huyo wa kwanza. Wewe anaendelea kukung'ang'ania kwa sababu ya sifa nilizozisema, na anapata wakati mgumu kuchagua ama awe na mwanamke asiyemvutia kimwili lakini mtii na mchapakazi au anayemvutia kimwili lakini hana sifa kama zako.
3. Hili suala lako wala siyo la kupewa ushauri kwani jibu liko wazi. i.e. achana naye kwani hakufai na ukiendelea kung'ang'ania utakuja juta siku moja. Infact una bahati sana kwani hamkufanya maamuzi ya kuoana kwa haraka hivyo umepata muda wa kujua ''rangi zake'' halisi. Niseme tu una bahati sana na huenda ni Mungu anayekuongoza ili ukwepe kukumbana na maisha ya ndoa ya mateso siku sijazo, hivyo tumia hii fursa kikamilifu. Usicheke na kima. Nina uhakika kabisa mwanamke kama hamtaki mwanaume ana uwezo mkubwa sana wa kumwambia HAPANA na mwanaume akakaa mbali naye.