Ushauri, Nataka kuanza biashara ya handbag au viatu toka China/Uturuki

Ushauri, Nataka kuanza biashara ya handbag au viatu toka China/Uturuki

Gan star

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
379
Reaction score
982
Wakuu habari za majukumu,

Nataka nifungue biashara ya kuuza mikoba au handbag za wadada, wallet na viatu pia special toka China na Uturuki.

Eneo ni Kibamba Dar es salaam. Kwa wale wenye ujuzi vipi inalipa wakuu, ushauri nahitaji wakubwa, mtaji ni 1.5 mil plain nje ya Gharama za fremu.

Mimi ni kijana wa kiume na nitafanya mwenyewe sitaweka mtu.

1618811053090.png
 
Mimi nilidhani wewe ndio unauza au unataka kuleta mrejesho wa biashara kumbe unataka kujua abs za hiyo biashara ngoja tusubiri waje.
 
Ningependa kujua pia. Ngoja nisubirie majibu
 
Inategemea. Ila ukiwa makini hiyo 1.5m waweza pata mikoba kama 150pcs mchanganyiko za kuuza tsh 10000 hadi 35000. Nunua bando la kutosha ingia Alibaba tazama vitu kiundani utapata kinachokufaa.
 
Inategemea. Ila ukiwa makini hiyo 1.5m waweza pata mikoba kama 150pcs mchanganyiko za kuuza tsh 10000 hadi 35000. Nunua bando la kutosha ingia Alibaba tazama vitu kiundani utapata kinachokufaa.
Ahsante mkuu, vipi nikitumia hawa wanaonunua na kusafirisha wabongo wenzetu, japo na was na uaminifu wao na bei zao zipo wakat mwingine naona zpo juu sana. Au nitumie tu Alibaba.
 
Ahsante mkuu, vip nikitumia hawa wanaonunua na kusafirisha wabongo wenzetu , japo na was was na uaminifu wao na bei zao zipo wakat mwingine naona zpo juu Sana .... Au nitumie Tu alibaba
Hapo kwenye woga ndio mwanzo wa anguko lako ukiwa Mjasiliamali usiogope kupoteza mkuu.

Nikushauri tu anza na Alibaba China utakuja kushuhudia Ukuu wa Mungu hapa.
 
Ahsante mkuu, vip nikitumia hawa wanaonunua na kusafirisha wabongo wenzetu , japo na was was na uaminifu wao na bei zao zipo wakat mwingine naona zpo juu Sana. Au nitumie Tu alibaba
Acha uoga. Wauzaji waliosajiliwa Alibaba ni waaminifu kuliko hao wabongo. Mimi nilianza na wabongo tukawa tunaishia kugombana tu. Sasa hivi ni Alibaba tu.
 
Huwa natamani kuagiza vitu Alibaba Ila hata sijui naanzaje naishia tu kutamani vitu na Bei Basi.
Ukishampata muuzaji Alibaba mtumie pesa kwa Western Union au kama ni nyingi fanya Bank Transfer. Akishapokea mpe contacts za wasafirishaji wa mizigo China-Dar kama Silent Ocean na wengine. Ataufikisha mzigo then subiria ukifika kawalipe Silent then endelea na biashara yako. Rahisi sana.
 
Na wale vijana wa Magu.Unawatoa vipi?
Ukishampata muuzaji Alibaba mtumie pesa kwa Western Union au kama ni nyingi fanya Bank Transfer. Akishapokea mpe contacts za wasafirishaji wa mizigo China-Dar kama Silent Ocean na wengine. Ataufikisha mzigo then subiria ukifika kawalipe Silent then endelea na biashara yako. Rahisi sana.
 
Acha uoga. Wauzaji waliosajiliwa Alibaba ni waaminifu kuliko hao wabongo. Mimi nilianza na wabongo tukawa tunaishia kugombana tu. Sasa hivi ni Alibaba tu.
Tuelekeze sasaa unaanza kuna app au?
 
Eneo ni Kibamba Dar es salaam. Kwa wale wenye ujuzi vipi inalipa wakuu, ushauri nahitaji wakubwa , mtaji ni 1.5 mil plain nje ya Gharama za fremu
Mkuu hizo gharama za fremu huko ulipo zitacost kiasi gani kwa mwezi?

Kama ni sehemu zenye mzunguko mkubwa wa watu na fremu ni Tshs 50,000/month huko kibamba sawa lakini kama ni zaidi ya laki sikushauri ni bora ukaongezea tu mtajo wako wa 1.5 mil.

Kisha ukaangalia mbinu za kusupply mzigo wako kama kuuza online na kuwatembezea wahitaji

Mtaji ukiwa mkubwa unaweza kukodi fremu
Ukalipia hzio gharama za kodi ya frem, Tra, manispa , uchafu, umeme, ulinzi na n.k
 
Halafu wewe ni mtu ninayevutiwa sana na post & comments zako humu. Pia wewe ni mkongwe humu.
Unatumia kampuni ya kusafirisha mizigo kutoka huko China to Tz mkuu? , Au unaagizia mwenyewe tu kwanjia ya Posta?
 
Mkuu hizo gharama za fremu huko ulipo zitacost kiasi gani kwa mwezi?

Kama ni sehemu zenye mzunguko mkubwa wa watu na fremu ni Tshs 50,000/month huko kibamba sawa lakini kama ni zaidi ya laki sikushauri ni bora ukaongezea tu mtajo wako wa 1.5 mil
Kisha ukaangalia mbinu za kusupply mzigo wako kama kuuza online na kuwatembezea wahitaji
Mtaji ukiwa mkubwa unaweza kukodi fremu
Ukalipia hzio gharama za kodi ya frem, Tra, manispa , uchafu, umeme, ulinzi na n.k
Click to expand...
Mkuu frem ni laki (100000), Ila na Mimi pia nimetarget kwenye digital marketing , pale ni kama ofisi ,mana usipokuwa na ofisi watu wanakuona kama Tapeli , kiukweli siwez kusema nategemea watu wanaopita njian ,mana ni wachache lakn pia sio wa kutegemea Sana , ... Nategemea kuweka na miamala ya pesa ,maji , na uwakala wa bank as days goes ona...ili kulinda Gharama za frem na tozo zingine .....
 
Nina group la whatsapp la wateja wengi ninaowanunulia kutokea huku Guanzhou, karibu kama utakuwa interested.. uaminifu utaverify kwa wateja wengine pia, na bei ruksa kuuliza ukafananishe na alibaba
 
Back
Top Bottom