Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Ingekuwa pesa ni yako cash ningekwambia uache kazi lkn kwa mkopo tuliza Mpira mkuu. Kopa muajiri mtu jitahd kusimamia hata kama unakuwa umechoka ndo uanaume.

Baadaye biashara ikistawi na mkopo ukamaliza kulipa unaweza drop kazi yako
 

Ndugu yangu umetoa ushauri ambao umenisikitisha sana.
Huyu jamaa alieamua kuacha kazi amefanya uamuzi sahihi sana.Kazi ya kuajiriwa ni utumwa na kamwe mtumwa hawezi kutajirika.Wafanyakazi wenye maisha mazuri ni wale waliowekeza kwenye biashara lakini watu wenye maisha na pesa nzuri ni wafanyabiashara.
Kwa kila hali naumga mkono kuacha kazi maana hapo atakuwa amechagua kukosa au kupata lakini kuendelea na kazi atakuwa amechagua kukosa.
 
Umetoa maelezo mengi mengi,... Unaoneka wew ni mtu wa maelezo mengi bila vitendo,.. Unaweza anzisha ata biashara ya 1M bila ata kumwambia mtu,...
 

Maisha ya kazi ni mlima siku zote na hakuna mteremko.Maisha ya milima,mteremko na tambarare yapo kwenye biashara.Ukiwa mtumishi ujue umechagua upande wa kushindwa.
 
Jiulize why wastaafu baadhi hufeli pamoja na mafao waliovuta!

Sent using Jamii Forums mobile app

Wastaafu wanafeli kwa sababu hawajui biashara na hawaipendi.Wanaingia humo kwa sababu hawana shughuli ya kufanya.Sababu nyingine ni Umri kuwatupa mkono hivyo hawawezi pilikapilika za Biashara.
Kazi yoyote inaanzwa ujanani sio Uzeeni.
 
Kama umefanya iyo kazi zaidi ya 10 years lakini huna hata saving ya 10m mi nakushauri ondoka mara moja. Yani jijue upo katika rat race.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Km ni mkopo usiache kazi ila km ulijiwekezea hizo hela na ni zako kabisa, ni sawa ukiacha job uwekeze. Usiteme bigG yako kwa karanga za kuonjeshwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Km ni mkopo usiache kazi ila km ulijiwekezea hizo hela na ni zako kabisa, ni sawa ukiacha job uwekeze. Usiteme bigG yako kwa karanga za kuonjeshwa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa hiyo unataka aendelee kuteseka maisha yake yote?
Uoga wako ndio umaskini wako.Hata siku moja huwezi kupata mafanikia katika njia ya tambarare.Huo mkopo ndio atumie kuanzisha biashara na atalipa deni kupitia faida ya biashara.Kazi inabidi aache mara moja kwani mshika mawili moja humponyoka.Naamini kwa machungu aliyonayo na maisha ya msoto aliyopitia akwa mwajiriwa lazima afanikiwe.
 
Mleta Mada kwanza hongera kwa kujitambua, pili mawazo yako ya kujiajiri ni hatua inayofuata tatizo lipo kwny hatua moja unayotaka kuruka, ambayo ni hujajiandaa vizuri katika ujasiriamali unaotaka kujiajiri, ulitakiwa mpka hatua hii hapa utuambie naacha kazi naenda kuendeleza kilimo changu cha,,,,,,au ufugaji wa,,,,,,,yaani atleat uwe umeshaanza huo ujasiriamali, siyo uache ndiyo ukaanze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati mbaya hujatuambia haya...
1/Kazi yako ya sasa inakulipa mshahara wa kiasi gani?
2/Unataka kwenda kufanya biashara gani?
3/Unategemea huo mkopo utaweza kuurejesha baada ya muda gani kwa kutumia hiyo biashara mpya?
4/Unategemea hiyo biashara utakulipa faida ya kiasi gani?
5/Utaishi hivi baada ya kuacha kazi kabla ya biashara yako mpya haijasimama kiasi cha kuweza kurejesha mkopo na kukupa faida?

Ushauri wangu wa jumla ni kwamba USIACHE KAZI. Jipange taratibu taratibu kuanzisha biashara na kutafuta mtaji kwa kutumia sehemu ya kipato chako cha mshahara cha sasa.
Mazingira ya sasa ya biashara nyingi hapa Tanzania ni magumu kupita maelezo, ni kama kucheza kamari fulani hivi.
 
Ni wazo zuri,
Lakini ukikopa hiyo mil 10 utailipa vp na umeacha kazi? Ingekua vizuri sana unaacha kazi usichukue mkopo,kiasi ulichotunza tu kinatosha hata kama mil 3 ila usiwe na familia,naona ni bora sana uanze kuanzia zero na pesa yako kuliko pesa ya kukopa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Teh, teh, 10M inakuzuzua?
Ukapimwe mkojo wewe. Si ivi iv unatatizo kwenye halmashauri ya ubongo wako, ni vizuri kuwai kupima mkojo kabla hali haijawa mbaya.

Utu ni mwema.
 
Wengi watakukatisha tamaa sana kuhusu mawazo yako . Ukijiamini unaweza kufanya mambo makubwa tu ya kimaendeleo ktk maisha yako. Bi siturongu
 
Hujaonesha unataka kufanya nini. Usitake kufanyia kazi mawazo ya wengine. Jua nini unataka kufanya, changamoto zake na matarajio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kawaida wanadai kua pesa ya mkopo si vyema ukaianziashia biashara, ni bora ukaanza na kidogo ulichonacho baadae ukishajua stability ya biashara yako ndiyo waweza kukopa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nakushauri omba ruhusa uende shule tena ukiwa unajiandaa kuanza biashara ili uweze kujua nje ya kazi kuna nini hii itakusaidia kuwa na muda wa kutengeneza network lakini ukiwa bado kazini na pia shule.
kama una shahada ya kwanza nenda master au post, miaka mitatu ni michache sana kuacha kazi ya serikali kumbuka kwamba hakuna fao la kujitoa.
hivyo tumia fursa hiyo kujipanga.
pia ni vizuri ukaweka wazi ni biashara gani unategemea kufanya ili tukushauri kwa ukaribu zaidi chagua hata tatu.
binafsi nafanya biashara ya ushauri lakini kuna kipindi wakati naanza ilipita miaka kama mitatu napata vijikazi vidogo sana kiasi vilikuwa haviwezi kulipa gharama za ofisi. ikawa nafika wakati naomba poo kwa kutafuta kazi.hivyo jipange taratibu kabla ya kujilipua
 
Coment za watu waoga. Kusoma ndo nini kuenda Masters ili iweje? ndo apate pesa nyingi? awe huru? ndo mnavyo jidanganya kwamba ukiwa na Masters basi maisha kwako ni Bora na utakuwa na pesa?

Kwani akiwa kijana hawez acha kazi? wanao paswa kuacha kazi ni wazee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…