Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Wakuu habari za majukumu.

Natambua JamiiForums ni kijiwe cha wasomi na mchanganyiko wa watu wenye busara zao.

Najitokeza mbele yenu mnipe ushauri kidogo, kwa ufupi mimi ni muajiriwa katika serikali yetu hapa Tanzania, kutokana na changamoto za kazi na hali halisi ya maisha nina plan kukopa fedha kiasi cha 10m kisha nianzishe miradi yangu binafsi ili nijiajiri niachane na kuajiriwa maana naona napelekeshwa ilihali maslahi ni duni sana.

Kazi ni nyingi mno na maslahi ni kiduchu sana, nilitamani kuanzisha miradi nikiwa katika ajira lakini muda ninaoingia na kutoka kazini ni wastani wa masaa 11 mpaka 12 kwa siku, hali hii inanichosha sana kiasi kwamba hata nikifika home akili inakua imechoka sana naishia kulala tu.

Kwa mantiki hiyo naona umaskini wangu unaweza kua wa kudumu maana hata nikiwatazama walionitangulia naona hawana kitu kikubwa sana walichofanya maishani.

Nina dreams nyingi na kubwa, napenda kua mtu huru na mwenye mafanikio makubwa kupitia biashara na kilimo, naiona ajira kama kifungo cha kunifanya niwe maskini. Sasa kwakua nimekaa kwenye system kwa takribani miaka mitatu naona ni vema nijilipue nikafanye yangu.

Naomba ushauri na mapendekezo yenu, watu hatulingani akili endapo unaona niko wrong basi naomba unishauri namna ya kuboresha hili wazo.

Kejeli na matusi sio mahala pake hapa, mimi ni kijana kama ulivyo kijana pengine nikawa sawa na mwanao ni vema unishauri kwa kujua unamshauri ndugu yako na mwana JF mwenzako.

Natanguliza shukrani.
Ingekuwa pesa ni yako cash ningekwambia uache kazi lkn kwa mkopo tuliza Mpira mkuu. Kopa muajiri mtu jitahd kusimamia hata kama unakuwa umechoka ndo uanaume.

Baadaye biashara ikistawi na mkopo ukamaliza kulipa unaweza drop kazi yako
 
Swali dogo tu kwako mtumishi kabla ujaacha kazi je ulishawahi kuchukua mkopo wowote ule angali ukiwa mtumishi? Je kama uliuchukua uliufanyia nini? Kama ukuchukua uliogopa nini?

Mtumishi amini hakuna kazi mbaya ni wewe tu mtazamo wako fikiria hiyo ajira yako inakupa uwezo wa kukopa milioni kumi huoni ajira yako ni zaidi ya biashara ukitulia vizuri, ulizia wafanya biashara ambao unataka ukaifanye hiyo biashara je biashara zao zinaweza kuwa dhamana benki wakapewa milioni kumi?

Kabla ujaacha kazi ulizia wafanyakazi wenzako ambao unamini pamoja na changamoto za kazi yenu ila wao wanafurahia maisha na wanasonga mbele kimaisha


Jambo jingine nyie watumishi mnafanyaga mipango yenu siri sana hampendi shirikisha watumishi wenzenu mnasahau wapo wenzenu umo makazini umri mdogo mnaona kama wajinga ila wana experience ya maisha na utafutaji zaidi yako

Ndugu yangu umetoa ushauri ambao umenisikitisha sana.
Huyu jamaa alieamua kuacha kazi amefanya uamuzi sahihi sana.Kazi ya kuajiriwa ni utumwa na kamwe mtumwa hawezi kutajirika.Wafanyakazi wenye maisha mazuri ni wale waliowekeza kwenye biashara lakini watu wenye maisha na pesa nzuri ni wafanyabiashara.
Kwa kila hali naumga mkono kuacha kazi maana hapo atakuwa amechagua kukosa au kupata lakini kuendelea na kazi atakuwa amechagua kukosa.
 
Umetoa maelezo mengi mengi,... Unaoneka wew ni mtu wa maelezo mengi bila vitendo,.. Unaweza anzisha ata biashara ya 1M bila ata kumwambia mtu,...
 
Hiyo 10m hesabu ya kuwa una mtaji wa 7m kwa sababu 3m lazima iingie katika maandalizi ya sehemu ya biashara. Maandalizi ninamaanisha kodi ya chumba na kukiandaa chumba ili uweke bidhaa. Hivyo huo ni mtaji mdogo sana kwani na mzunguko wa biashara kwa sasa si wa kuridhisha

Lakini pia elewa maisha ya kazini ni sawa na sura ya dunia ilivyo. Kuna milima, mitelemko na tambalale. Hivyo kwa sasa unapanda mlima vumilia. Kwani itafiki wakati utashuka na Kuna kipindi utatembea katika tambalale.

Maisha ya kazi kamwe haiwezekani ukayaona ni mtelemko au tambalale siku zote. Kaza buti ndiyo majaribu ya maisha hayo.

Maisha ya kazi ni mlima siku zote na hakuna mteremko.Maisha ya milima,mteremko na tambarare yapo kwenye biashara.Ukiwa mtumishi ujue umechagua upande wa kushindwa.
 
Jiulize why wastaafu baadhi hufeli pamoja na mafao waliovuta!

Sent using Jamii Forums mobile app

Wastaafu wanafeli kwa sababu hawajui biashara na hawaipendi.Wanaingia humo kwa sababu hawana shughuli ya kufanya.Sababu nyingine ni Umri kuwatupa mkono hivyo hawawezi pilikapilika za Biashara.
Kazi yoyote inaanzwa ujanani sio Uzeeni.
 
Km ni mkopo usiache kazi ila km ulijiwekezea hizo hela na ni zako kabisa, ni sawa ukiacha job uwekeze. Usiteme bigG yako kwa karanga za kuonjeshwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Km ni mkopo usiache kazi ila km ulijiwekezea hizo hela na ni zako kabisa, ni sawa ukiacha job uwekeze. Usiteme bigG yako kwa karanga za kuonjeshwa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa hiyo unataka aendelee kuteseka maisha yake yote?
Uoga wako ndio umaskini wako.Hata siku moja huwezi kupata mafanikia katika njia ya tambarare.Huo mkopo ndio atumie kuanzisha biashara na atalipa deni kupitia faida ya biashara.Kazi inabidi aache mara moja kwani mshika mawili moja humponyoka.Naamini kwa machungu aliyonayo na maisha ya msoto aliyopitia akwa mwajiriwa lazima afanikiwe.
 
Mleta Mada kwanza hongera kwa kujitambua, pili mawazo yako ya kujiajiri ni hatua inayofuata tatizo lipo kwny hatua moja unayotaka kuruka, ambayo ni hujajiandaa vizuri katika ujasiriamali unaotaka kujiajiri, ulitakiwa mpka hatua hii hapa utuambie naacha kazi naenda kuendeleza kilimo changu cha,,,,,,au ufugaji wa,,,,,,,yaani atleat uwe umeshaanza huo ujasiriamali, siyo uache ndiyo ukaanze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati mbaya hujatuambia haya...
1/Kazi yako ya sasa inakulipa mshahara wa kiasi gani?
2/Unataka kwenda kufanya biashara gani?
3/Unategemea huo mkopo utaweza kuurejesha baada ya muda gani kwa kutumia hiyo biashara mpya?
4/Unategemea hiyo biashara utakulipa faida ya kiasi gani?
5/Utaishi hivi baada ya kuacha kazi kabla ya biashara yako mpya haijasimama kiasi cha kuweza kurejesha mkopo na kukupa faida?

Ushauri wangu wa jumla ni kwamba USIACHE KAZI. Jipange taratibu taratibu kuanzisha biashara na kutafuta mtaji kwa kutumia sehemu ya kipato chako cha mshahara cha sasa.
Mazingira ya sasa ya biashara nyingi hapa Tanzania ni magumu kupita maelezo, ni kama kucheza kamari fulani hivi.
 
Ni wazo zuri,
Lakini ukikopa hiyo mil 10 utailipa vp na umeacha kazi? Ingekua vizuri sana unaacha kazi usichukue mkopo,kiasi ulichotunza tu kinatosha hata kama mil 3 ila usiwe na familia,naona ni bora sana uanze kuanzia zero na pesa yako kuliko pesa ya kukopa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Teh, teh, 10M inakuzuzua?
Ukapimwe mkojo wewe. Si ivi iv unatatizo kwenye halmashauri ya ubongo wako, ni vizuri kuwai kupima mkojo kabla hali haijawa mbaya.

Utu ni mwema.
 
Wengi watakukatisha tamaa sana kuhusu mawazo yako . Ukijiamini unaweza kufanya mambo makubwa tu ya kimaendeleo ktk maisha yako. Bi siturongu
 
Hujaonesha unataka kufanya nini. Usitake kufanyia kazi mawazo ya wengine. Jua nini unataka kufanya, changamoto zake na matarajio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kawaida wanadai kua pesa ya mkopo si vyema ukaianziashia biashara, ni bora ukaanza na kidogo ulichonacho baadae ukishajua stability ya biashara yako ndiyo waweza kukopa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nakushauri omba ruhusa uende shule tena ukiwa unajiandaa kuanza biashara ili uweze kujua nje ya kazi kuna nini hii itakusaidia kuwa na muda wa kutengeneza network lakini ukiwa bado kazini na pia shule.
kama una shahada ya kwanza nenda master au post, miaka mitatu ni michache sana kuacha kazi ya serikali kumbuka kwamba hakuna fao la kujitoa.
hivyo tumia fursa hiyo kujipanga.
pia ni vizuri ukaweka wazi ni biashara gani unategemea kufanya ili tukushauri kwa ukaribu zaidi chagua hata tatu.
binafsi nafanya biashara ya ushauri lakini kuna kipindi wakati naanza ilipita miaka kama mitatu napata vijikazi vidogo sana kiasi vilikuwa haviwezi kulipa gharama za ofisi. ikawa nafika wakati naomba poo kwa kutafuta kazi.hivyo jipange taratibu kabla ya kujilipua
 
nakushauri omba ruhusa uende shule tena ukiwa unajiandaa kuanza biashara ili uweze kujua nje ya kazi kuna nini hii itakusaidia kuwa na muda wa kutengeneza network lakini ukiwa bado kazini na pia shule.
kama una shahada ya kwanza nenda master au post, miaka mitatu ni michache sana kuacha kazi ya serikali kumbuka kwamba hakuna fao la kujitoa.
hivyo tumia fursa hiyo kujipanga.
pia ni vizuri ukaweka wazi ni biashara gani unategemea kufanya ili tukushauri kwa ukaribu zaidi chagua hata tatu.
binafsi nafanya biashara ya ushauri lakini kuna kipindi wakati naanza ilipita miaka kama mitatu napata vijikazi vidogo sana kiasi vilikuwa haviwezi kulipa gharama za ofisi. ikawa nafika wakati naomba poo kwa kutafuta kazi.hivyo jipange taratibu kabla ya kujilipua
Coment za watu waoga. Kusoma ndo nini kuenda Masters ili iweje? ndo apate pesa nyingi? awe huru? ndo mnavyo jidanganya kwamba ukiwa na Masters basi maisha kwako ni Bora na utakuwa na pesa?

Kwani akiwa kijana hawez acha kazi? wanao paswa kuacha kazi ni wazee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom