Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Karibu sana kwenye haya maisha ya kujiajiri,ni raha mustarehe,fursa zipo kibao,,hakuna cha bosi wala mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona kama anachelewa kuja...tena anaingia na mtaji wa mil 10...watu tuliingia bila mia moja na maisha yakaenda....sipendi wanaomtia ujinga eti aendelee kuajiriwa wakati anafanya kazi zake.

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 
Tatizo moja ndugu zetu,mukipata pesa nyingi munawaza kufunga Bar.Sasa fikiria vizuri usijemaliza pesa na kazi huna.
Huku nje kusikie tu hivyo hivyo.Na kibaya utakua unasikia kauli kali tu kila siku wakati kibarua huna."Asie fanya kazi na asile"
 
Kwanza nikupe hongera mkuu kwa wazo lako maana hata huo mshahara unaopata ni kama zawadi tu ya kukufanya uendelee kufanya kazi na si kutimiza malengo yako bali malengo yao.
~Ni vizuri kujiwekezea hela ili uje kutumia kama mtaji na si kukopa maana mkopo unasaidia kuendeleza na kukuza biashara.
~Usitishike kua mtaani kugumu kwani kufeli ni mojawapo ya kujifunza, bila kufeli utajifunza lini?? Kumbuka: watu wengi walio na malengo wanawafanyia kazi watu wenye malengo, utaendelea kua mtumwa hadi lini? Better be a risk taker
~ Fanya research kuhusu biashara unayotaka kufanya na pia tafuta ushauri kwa watu mbalimbali.
Start with commitment finish with consistence

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena lililojema ila kama itamchukua 10 yrs kuipata hiyo 10m kwa kazi hiyo anayofanya ni bora atoke fasta achukuwe huo mkopo na a hit the ground like a real man.

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 
Wakuu habari za majukumu.

Natambua JamiiForums ni kijiwe cha wasomi na mchanganyiko wa watu wenye busara zao.

Najitokeza mbele yenu mnipe ushauri kidogo, kwa ufupi mimi ni muajiriwa katika serikali yetu hapa Tanzania, kutokana na changamoto za kazi na hali halisi ya maisha nina plan kukopa fedha kiasi cha 10m kisha nianzishe miradi yangu binafsi ili nijiajiri niachane na kuajiriwa maana naona napelekeshwa ilihali maslahi ni duni sana.

Kazi ni nyingi mno na maslahi ni kiduchu sana, nilitamani kuanzisha miradi nikiwa katika ajira lakini muda ninaoingia na kutoka kazini ni wastani wa masaa 11 mpaka 12 kwa siku, hali hii inanichosha sana kiasi kwamba hata nikifika home akili inakua imechoka sana naishia kulala tu.

Kwa mantiki hiyo naona umaskini wangu unaweza kua wa kudumu maana hata nikiwatazama walionitangulia naona hawana kitu kikubwa sana walichofanya maishani.

Nina dreams nyingi na kubwa, napenda kua mtu huru na mwenye mafanikio makubwa kupitia biashara na kilimo, naiona ajira kama kifungo cha kunifanya niwe maskini. Sasa kwakua nimekaa kwenye system kwa takribani miaka mitatu naona ni vema nijilipue nikafanye yangu.

Naomba ushauri na mapendekezo yenu, watu hatulingani akili endapo unaona niko wrong basi naomba unishauri namna ya kuboresha hili wazo.

Kejeli na matusi sio mahala pake hapa, mimi ni kijana kama ulivyo kijana pengine nikawa sawa na mwanao ni vema unishauri kwa kujua unamshauri ndugu yako na mwana JF mwenzako.

Natanguliza shukrani.
Vichaa / Wehu / Wasiojihurumia kama ambavyo tumezoea kuwaita ndio wanaoifanya hii dunia ikasogea mbele. Amini usiamini kama hujawahi kufanya jambo ambalo kila mtu wa pembeni yako akakuona unaenda kujimaliza / hutatoka mzima, bado hujaishi Joh, " You are still dwelling in your comfort zone".

Chunguza watu waliofanya wonders in life, they sacrificed their lives, reputation, even their parent's trust. Kama wewe kila ulichokifanya nyomi iliyoko nyuma yako ilikupa support bado hufai kujiita successful man/woman. Successfully people are few, Minority na sio Majority.

Kuna watu wanachukua maamuzi ya kuacha kazi hali wakiwa mifuko mitupu kabisa. Mtu kama huyo akija hapa akaomba ushauri " Nataka niache kazi nijiajiri ila sina hata mia mfukoni ". Majority ya comments atakazopata hapa ni kumuona mpumbavu na mtoto na asiye na life experience. Atatahadharishwa kuisoma number hadi akome.
KWA NINI? Kwa sababu wanaomshauri hawajawahi ku take risk kama hizo, they are doing nathing rather than Screaming., Hawajawahi kuwa risk takers.

Kuna watu waliamua kuahirisha kama sio kuacha kabisa masomo yao ya elimu ya juu hali wakiwa hawana kitu kwenye mifuko yao, hawakujua wangeanzia wapi, lakini leo hii ndio madereva wa hii dunia..

Believe me or not asikudanganye mtu akakwambia Jiajiri huku umeajiriwa huyo ni screamer not a risk taker.

Failure zipo kila mahali, kila siku,kwa kila mtu, they are "Inevitable". Ukianguka ukalala hapo ndo pana tatizo. Kila mtu keshafeli kwa kitu fulani hata unaowaona wamefanikiwa walishafeli mara nyingi mno asikwambie mtu. The road to success is rough x 100 Joh, and only few dare to take.

Nimeamua kuanzisha huu uzi ku share mastory za kujilipua kimaisha kuwapa courage wale wote wanaotaka kuchukua maamuzi magumu in life. Wazamiaji wa mamtoni, waacha vyuo/shule kama mimi, waacha kazi, waliofukuzwa makwao na wengineo ili risk takers msijiskie wapweke au mko wenyewe.

"Taking risk is the quickest way".

Nakupa akili ndogo sn na ya kijinga sana ambayo nina ushuhuda kbs jinsi mtu wangu wa karibu alivyotoboa kijinga jinga...alikopa m.10,mwezi wa 6 mwaka jana...tupo nae mbeya...akanunua mahindi debe 7500 alinunua debe za 9,500,000 akanunua dawa zA kupuliza kuyahifadhi na gharama ya kuyasafirisha hadi kwake sowetto kutoka mbeya vijijini alitumia 100,000/- akaweka store hadi mwezi wa kumi na moja kati kati akauza kwa debe moja 16,000/- bei ya jumla kipindi ambacho sokoni debe la mahindi nin18,000/- akapata zaidi milion 18 +...kwa uoga wake akalipa deni bank akanunua kiwanja halafu mwaka huu ameshindwa ht kuweka debe mbili store...kama unaogopa hela huwezi kuipata naukiipata haikai...na siku zote elimu yako ndo umasikini wako linapokuja swala la biashara...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadiriki kusema kuwa MTU anayesema kuwa mtaji wa sh mil.10 hautoshi kuanzisha biashara.
Kwa mawazo yake sijui ni sh ngapi zitatosha kuanzisha biashara.

Mi nilianzisha biashara kwa sh laki 3, hadi sasa biashara yangu ina kama bidhaa za sh laki 8. Mdogomdogo nakimbiza

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu niambie ni biashara gani hiyo nianzishe na mimi kama hutojali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maamuzi yoyote unayofanya kutokana na pesa inayopita mikononi mwako yanaweza kukufanya kuwa tajiri ama masikini.

Pesa yoyote inayopita mikononi mwako iwe ya ku save ama kukopa inaweza kukufanya kuwa masikini ama tajiri.

Maamuzi yoyote unayofanya iwe kuajiliwa ama kujiajili yanaweza kukufanya kuwa tajiri ama masiki.

Pesa sio msingi wa mafanikio ni kifaa kinachokusaidia kufikia mafanikio ama malengo yako.

Hatuachi kazi kwakua tuna mtaji wa kufanya ama tunapenda kuajili wenyewe. Tunaacha kazi wakati tunapoona muda tunaoutumia kumzalishia boss ni mwingi kuliko muda tunaoutumia kuzalisha vyakwetu binafsi. Unapoona mshahara kwa mwezi ni sawa na faida unayoipata kwa ulichokianzisha wakati unatumika kotekote.

Ushari wangu.
Usikope 10mil, kopa 6mil tu baada ya miezi mitatu pima faida unayoipata kutokana na uwekezaji wa 6mil. Tathimin Kama inalingana na mshahara au lah! Ukiwa smart itakuwa zaidi ya mshahara wako.

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri usiache kazi,mara upatapo huo mkopo tafuta mtu mwamininifu umuajiri aweze kuendesha biashara yako,au tafuta business partner,wewe uwekeze kwenye mtaji na yeye awekeze kwenye nguvu kazi,mara baada ya kuona matokeo chanya ndio uache kazi.
Pole sana kusikia unachoka sana na ukirudi nyumbani wewe ni kulala tu? Vipi humpi huduma yake shemeji? Au majirani wanakusaidia kuhudumia.
Jiajiri mkuu uwe huru bhana!

Wakuu habari za majukumu.

Natambua JamiiForums ni kijiwe cha wasomi na mchanganyiko wa watu wenye busara zao.

Najitokeza mbele yenu mnipe ushauri kidogo, kwa ufupi mimi ni muajiriwa katika serikali yetu hapa Tanzania, kutokana na changamoto za kazi na hali halisi ya maisha nina plan kukopa fedha kiasi cha 10m kisha nianzishe miradi yangu binafsi ili nijiajiri niachane na kuajiriwa maana naona napelekeshwa ilihali maslahi ni duni sana.

Kazi ni nyingi mno na maslahi ni kiduchu sana, nilitamani kuanzisha miradi nikiwa katika ajira lakini muda ninaoingia na kutoka kazini ni wastani wa masaa 11 mpaka 12 kwa siku, hali hii inanichosha sana kiasi kwamba hata nikifika home akili inakua imechoka sana naishia kulala tu.

Kwa mantiki hiyo naona umaskini wangu unaweza kua wa kudumu maana hata nikiwatazama walionitangulia naona hawana kitu kikubwa sana walichofanya maishani.

Nina dreams nyingi na kubwa, napenda kua mtu huru na mwenye mafanikio makubwa kupitia biashara na kilimo, naiona ajira kama kifungo cha kunifanya niwe maskini. Sasa kwakua nimekaa kwenye system kwa takribani miaka mitatu naona ni vema nijilipue nikafanye yangu.

Naomba ushauri na mapendekezo yenu, watu hatulingani akili endapo unaona niko wrong basi naomba unishauri namna ya kuboresha hili wazo.

Kejeli na matusi sio mahala pake hapa, mimi ni kijana kama ulivyo kijana pengine nikawa sawa na mwanao ni vema unishauri kwa kujua unamshauri ndugu yako na mwana JF mwenzako.

Natanguliza shukrani.
kus
 
Acha Kazi haraka,mafanikio ni imani.Utapigika sana tu ila usikate tamaa,jambo moja tu fanya saving ya mishahara yako ukipata pesa kiasi fulani cha kutosha kuanza biashara yako anza,mkopo achana nao kwanza,wingi wa pesa sio mafanikio.wazo lako na jinsi utakavyo litekeleza ndio litakalokufanikisha start small with Mtaji kidogo utafanikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atapataje experience akiwa kazini? au atakuwa anaifanyia kazini kwake?

Biashara ikiwa changa inamihitaji sana Initiotor wa Idea. ni sawa na.mtoto mchanga kumuhitaji sana mama yake kwa miezi 3 ya mwanzo na ndo maana ya likizo ya miezi 3 ya uzazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi sana ndugu ushauri wako ni mzuri sana,huwezi kuanzisha biashara ukamuweka mtu aifanye tena ikiwa changa itakufa tu........namshauri mleta mada aache kazi mara moja akiwa na hiyo mil.10 aanze biashara na hela kidogo asiiweke yote aweke kidogo ikifeli atakuwa amejifunza ataweka tena ..........kufanya biashara ukiwa umeajiriwa ni kujidanganya tu na kupoteza nguvu pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BAKI KWENYE KIBARUA CHAKO MKUU

Niliwahi kuandika nyuzi apa yenye kichwa UZUSHI/UPOTOSHWAJI UNAOHUSISHWA NA UJASIRIAMALI, nilipata critics nyingi hasa kwa watu wasioelewa au pengine wamepotoshwa au hawajui na wala sio wajasiriamali.

Nimehusunisha uzi huo na hiki kinachokusibu ww, apa ushauri uliotolewa mwingi ni wa watu waliosikia au kusoma kuhusu ujasiriamali kutoka kwa watu wasio wajasiriamali au nao ni wajasiriamali tayari lakini hawajui dhana ya uhalisia wake ulivyo.

Mengi yamesemwa lakini kwa ushauri wng ni kuwa BAKI KWENYE KIBARUA CHAKO, infact kuwa mpole tu hata usidiriki kukopa na kufanya 'side husle/business' utalia charii.

Baki kwenye ajira yako maana unachokitafuta au kinachokusukuma kukimbilia ujasiriamali hutokipata na kwa ukweli ulivyo ni bora ubaki kibaruani. Nime highlight sabab zinazokufanya utake kuwa mjasiriamali na kwa hakika kama dhumuni lako ni kuchoka kupelekeshwa, kufanya kazi nyingi na kupata maslahi duni..huku chalii ni kwamba utafanya kazi kubwa tena kubwa na unaweza usipate malipo(faida) ata kwa mwaka mzima.

Unasema unataka uhuru, unafanya kazi masaa 11/12 jaribu kutizama mtu kama Elon musk au Marc Cuban hawa jamaa wanafanya kazi zaidi ya masaa 17-19 kwa siku, sasa ww 11 hrs zinakuchosha..fikiria mara mbili.

Anyway ya kuambiwa changanya na yako, ila kama sabab ni hizo zinakusukuma kutaka biashara/ujasiriamali nafikiri unahitaji kufikir zaid na kuwa na motive kubwa zaid ya hizo maana huku shuruba ni marambili zaid ya hizo kazini.

Kila la kher, kumbuka Men who do not have goals are doomed forever to work for these who do have goals.
Mawazo finyu sana haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuu..kwanza hongera sana kwa wazo jema...Hongerassnaaaa. .

Nimegundua hapa unapata ushauri kwa ""WATUMWA"" wengi...waoga..wadhaifu wakufikiri..waive Sana Hawa. .hawapendi kujishughulisha..

Kupanga nikuchagua..
Kwanza Fanya OPPORTUNITY COST. .
Linganisha kaziyako namalipo.mda na jinsi yakuacha kazi..
Waajiriwa wengi wana mawazo mgandosana..hasa hawa WA SEREKALI WAVIVU MNOOO WAOGA ..
Kama utakopa kopa tuu..najua mkopo una INSURANCE na NSSF au mfukowowote watakata kwenye malipo yako..
Kapige kazikaka biashara inalipasana..jitume zingatia..wengine tulishasahau kutumikishwa zsidi ya miaka mi5..heriyako unayekopa..mm sikukopa hatakumi..niliamua kuacha baada yakuchoka mishahara midogo ya serekali.

Usiogope mkuu...hakuna kitu muhimu kama resource muhimu kama MUDA...

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi sana ushauri mzuri sana huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wazo ulilonalo tu Naomba nikuite "Mdogo wangu"
Mdogo wangu, please USIACHE KAZI...

baki na Kazi yako na omba huo mkopo ufanye biashara, tena omba Mikopo kama hiyo Zaidi ya mmoja Baada ya kuona maendeleo ya kile utakachoanzisha
Tafuta watu 10 walioacha kazi.... Nakwambia waliofanikiwa hawazidi 3.
Usiache kazi tafadhalini, Mimi nimeajiriwa kampuni Binafsi na bado Nina biashara zangu na nimeajiri watu.
Kwenye biashara kuna changamoto nyingi Sana, unaanguka na kusimama, unaanguka, unajikwaa unasimama, wengine wanaanguka jumla...
Baki na Kazi yako na anzisha biashara
HAPA KIYOSAKI HANA NAFASI
Acha kumuogopesha mwenzako wewe kila mtu ana njia yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BAKI KWENYE KIBARUA CHAKO MKUU

Niliwahi kuandika nyuzi apa yenye kichwa UZUSHI/UPOTOSHWAJI UNAOHUSISHWA NA UJASIRIAMALI, nilipata critics nyingi hasa kwa watu wasioelewa au pengine wamepotoshwa au hawajui na wala sio wajasiriamali.

Nimehusunisha uzi huo na hiki kinachokusibu ww, apa ushauri uliotolewa mwingi ni wa watu waliosikia au kusoma kuhusu ujasiriamali kutoka kwa watu wasio wajasiriamali au nao ni wajasiriamali tayari lakini hawajui dhana ya uhalisia wake ulivyo.

Mengi yamesemwa lakini kwa ushauri wng ni kuwa BAKI KWENYE KIBARUA CHAKO, infact kuwa mpole tu hata usidiriki kukopa na kufanya 'side husle/business' utalia charii.

Baki kwenye ajira yako maana unachokitafuta au kinachokusukuma kukimbilia ujasiriamali hutokipata na kwa ukweli ulivyo ni bora ubaki kibaruani. Nime highlight sabab zinazokufanya utake kuwa mjasiriamali na kwa hakika kama dhumuni lako ni kuchoka kupelekeshwa, kufanya kazi nyingi na kupata maslahi duni..huku chalii ni kwamba utafanya kazi kubwa tena kubwa na unaweza usipate malipo(faida) ata kwa mwaka mzima.

Unasema unataka uhuru, unafanya kazi masaa 11/12 jaribu kutizama mtu kama Elon musk au Marc Cuban hawa jamaa wanafanya kazi zaidi ya masaa 17-19 kwa siku, sasa ww 11 hrs zinakuchosha..fikiria mara mbili.

Anyway ya kuambiwa changanya na yako, ila kama sabab ni hizo zinakusukuma kutaka biashara/ujasiriamali nafikiri unahitaji kufikir zaid na kuwa na motive kubwa zaid ya hizo maana huku shuruba ni marambili zaid ya hizo kazini.

Kila la kher, kumbuka Men who do not have goals are doomed forever to work for these who do have goals.
We jamaa bhaaana... unaishi mfumo wa elon musk...
Embu jiongeze kidogo.... uwe unaangalia nyanja zoote... mada.. mazingira ya kazi... kipato.... n.k

Haya uyo elon musk na masaa yake 17 anaringana na mlinz wa duka la wahindi masaaa 24...

We tulia acha uoga... risk taking ndio njia nyepesi ya mafanikio....

Sent from "La -Vista"
 
Wakuu habari za majukumu.

Natambua JamiiForums ni kijiwe cha wasomi na mchanganyiko wa watu wenye busara zao.

Najitokeza mbele yenu mnipe ushauri kidogo, kwa ufupi mimi ni muajiriwa katika serikali yetu hapa Tanzania, kutokana na changamoto za kazi na hali halisi ya maisha nina plan kukopa fedha kiasi cha 10m kisha nianzishe miradi yangu binafsi ili nijiajiri niachane na kuajiriwa maana naona napelekeshwa ilihali maslahi ni duni sana.

Kazi ni nyingi mno na maslahi ni kiduchu sana, nilitamani kuanzisha miradi nikiwa katika ajira lakini muda ninaoingia na kutoka kazini ni wastani wa masaa 11 mpaka 12 kwa siku, hali hii inanichosha sana kiasi kwamba hata nikifika home akili inakua imechoka sana naishia kulala tu.

Kwa mantiki hiyo naona umaskini wangu unaweza kua wa kudumu maana hata nikiwatazama walionitangulia naona hawana kitu kikubwa sana walichofanya maishani.

Nina dreams nyingi na kubwa, napenda kua mtu huru na mwenye mafanikio makubwa kupitia biashara na kilimo, naiona ajira kama kifungo cha kunifanya niwe maskini. Sasa kwakua nimekaa kwenye system kwa takribani miaka mitatu naona ni vema nijilipue nikafanye yangu.

Naomba ushauri na mapendekezo yenu, watu hatulingani akili endapo unaona niko wrong basi naomba unishauri namna ya kuboresha hili wazo.

Kejeli na matusi sio mahala pake hapa, mimi ni kijana kama ulivyo kijana pengine nikawa sawa na mwanao ni vema unishauri kwa kujua unamshauri ndugu yako na mwana JF mwenzako.

Natanguliza shukrani.
Hii mikazi ya serikalini hatuwezi kutoka baadhi ya wakubwa kwenye hizi ofisi Wana roho mbaya ukipata chance itumie ila kabla hujaacha hakikisha una biashara ya kueleweka, sio lazma kazi ndio ufanikiwe ni uoga wetu tu.
 
Back
Top Bottom