Ushauri: Ndugu wameharibu ndoa ya dada yangu

Ushauri: Ndugu wameharibu ndoa ya dada yangu

Wakuu,

Mwezi Mei mwaka jana, kuna dada yangu mmoja aligombana na mumewe na kukimbilia kwangu. Nilipoongea na mumewe, akasema yeye hana tatizo nae, arudi tu wayamalize.

Nilipomsihi dada arudi wakayamalize, akawa hataki, anang'ang'ania aendelee kuishi kwangu tu. Nikaamua kumfukuza aondoke, kwangu sina nafasi ya kuhifadhi mke wa mtu mimi.

Kumbe alivotoka kwangu akahamia kwa ndugu wengine wakampokea akaishi. Nikawa naskia tu, sasa dada anakaa kwa ndugu flani, mara kahamia kwa ndugu mwingine, kwa mumewe kagoma kabisa kurudi.

Nimewasihi ndugu zangu sio vizuri kukaa na mke wa mtu majumbani kwenu, hawataki kunielewa, wanadai namtetea sana mume wa dada yangu, nataka mpk afe ndo nijue mumewe ni mnyanyasaji wa kijinsia.

Wakasema kama mumewe anamtaka mkewe basi amfate mwnyw ukweni na akaiombe radhi familia, vinginevyo asahau kabisa kama alishawai kumuoa ndugu yao. Nikaamua kujiweka kando na hayo mambo.

Amekuja kurudi kwa mumewe mwezi huu tar 02 (miezi 11 imepita) akiwa na mimba ya kubwa sana. Mumewe kagoma kabisa kumpokea akidai mkewe aliondoka akiwa hana mimba, inakuaje arud kwake akiwa na mimba? Hiyo mimba sio yake.

Nmemhoji dada yangu, anadai ile mimba ni ya mumewe 100% na aliondoka nayo, ila alishindwa kumtaarifu mumewe kutokana na ugomvi uliokuepo kati yao.

Ndugu waliomhifadhi miezi yote hiyo wananipigia kunisihi niongee na shemeji yangu, ampokee mkewe maana ni mjamzito sana anaweza kujifungua muda wowote. Nimewaambia hiyo kazi siifanyi, fanyeni nyie wenyewe mlioyasababisha. Wanadai jamaa hawezi kuwaelewa, walishagombana tayari na hawapokelei kabisa simu zao.

Nmemtafuta shemeji, anachosema ni kwamba, kama kweli mkewe aliondoka na mimba yake ile mwezi Mei mwaka jana walipogombana, basi mwaka huu mwezi January au February alitakiwa awe tayari keshajifungua mtoto.

Sasa hivi ni mwezi March, ni miezi 11 tangu mkewe aondoke bado ni mjamzito hajajifungua, hivyo kwa vyovyote vile ile mimba sio yake. Kaipatia huko huko kwa ndugu zake na kwa tafsiri hiyo, hamna ndoa tena hapa.

Kiukweli mpaka sasa kichwa kimepata moto, sielewi nifanye nini dada yangu akae sawa maana analia muda wote (na hii mimba alionayo nahisi itamletea shida au huenda akajidhuru).

Pia nishauri nini kifayike ikiwezekana arudiane na mumewe, maana jamaa hataki hata kumskia mkewe wala habari zake na kahama kabisa pale nyumbani, kaenda kupanga sehemu nyumba nyingine kabisa.

Nawasilisha. 🙏
Apo jamaa akubalu kua Fala ndo atakubaliana na jambo, wanawake hua wanajihusi wajanja , afu hutuona maboya sana, anasingizia jambo huku akijua ukweli lakini anakaza tu,

Aende kwa mwenye mzigo, si alijiona janja
 
Haraka ya nini jamaa asubirie mtoto azaliwe akapime.
Je akikuta ni wake itakuaje
 
ila mnapenda kukimbilia manyumbani kwenu na kusiko julikana nyie viumbee, njia sahihi sahihi ya changamoto za kimahusiano ni better kila kunapoibuka mgogoro, subini hasira zenu zipoe mnakaa chini na mwenzio baada ya nyote kupoza hasira zenu, kisha mnasolve mambo yenu.

Ila nyie wenzetu sasa, mnautoto wa kila mgogoro kutukimbia kama vile sisi ni mashetani na makatiri wa kutisha sana ........
Tena mashetani kweli
 
Yaan familia ikishakua na wadada wengi, Ni full kulishana ujinga TU afu wakishaharibu uko ndo wanatukumbuka mabrother wao[emoji35]
Pia wadada huaribu pia ndoa za kaka zao, bila shaka huonea wivu wifi zao wakiwa na amani na wake zao
 
Hapo Hata wakirudiana huyo mtoto atakayezaliwa hatapata upendo wa baba, Mimi naona wandugu mjipange Ili dada ajifungue salama. Na mtoto akiwa mkubwa kiasi mumlee na dada mumtafutie mtaji wa biashara ajitegemee.Hayo mambo ya kumrudisha Kwa mume muachane nayo yakitokea iwe ni wao wenyewe. Hiv wewe unaona ni rahisi kumrudia mwanamke ana mimba ya miezi 11 manake sio Yako. Wewe unaweza? Hiv akija kumdhuru mtoto Au dada yenu mtamlaumu? Nasemaje, mchuma majanga hula na wakwao Hilo ni lenu.

Ndugu zako wamekosa na Wewe Kama mtoto wa kiume, ulipaswa kutazama Mbali, dada anapokaa Mbali na mmewe Kwa muda mrefu lolote linaweza kutokea, dada alizoea kupigwa mambo Mara Kwa Mara , Sasa mnapomng'ang'ania mlidhan atakua anaridhikaje, mmewe ni rijali pia hawezi kukaa muda wote bila kupiga mambo, akipata demu anaweza kuweka ndani mazima. Mlipaswa kuchukua hatua mapema, wewe Kama mtoto wa kiume ulipaswa Hata kutumia udikteta kumrudisha dada Kwa mmewe.

Kaa na mkeo umueleweshe tu ugumu uliopo na ukiweza msaidie dada kujitegemea , ukishindwa acha wapambane walioharibu ndoa. Ningekua Mimi ningeachana Naye mazima atajijua mwenyewe. Just image hapa nishakasirika.
 
Wewe ndo mzembe kwa nn usingemuita uyo mume mkaja kuyaongea na kuyamaliza wakiwa pande zote mbili wapo wewe utamwambiaje tu arud kwa mumewe bila kujua sababu zilizomfsnya aondoke
 
Unakumbuka Kifo cha Piariz Charles Hizza, kilicho trend Pale tabata ter 02/10/2022?
Screenshot_20240312_061326_Chrome.jpg
Ni haya haya Mambo ya Kulazimisha Ndugu arudi kwa Mume wake,

Pia alienda home kwa kaka yake akamuambia Kaka (Sitataja jina) Yule mwanaume ataniua...

Kaka akamuambia Hapana rudi kwa mmeo,
Pia akakatazwa kuja kwenye harusi ter 01/10/2022, kila mtu akashangaa kwa nini hajaja kwenye harusi, Usiku watu tupo ukumbini yupo live video Call, Asubuhi tunaambiwa Kajinyonga, kumbe aliuawa kifo cha kikatili na taratibu,

Mpaka leo Bro aliyemshauri Pia arudi kwa mmewe hana Amani akikumbuka, Ndugu wote walimgeuka.., Aliongea kwa nia nzuri kabisa, Ila ni kwamba Hakuamini kama shemeji yake anaweza akaenda Deep kiasi alichotenda.

Mimi isingekua experience hii ningekuunga mkono, ila kwa lile, HAPANA.

Pengine yote haya yanaweza kua nimeandika yakapita, Sawa, ombea usije ukajifunza kwa gharama kubwa kama ile.
 
Dada kaivunja nyumba yake mwenyewe!, ana watoto/ mtoto na aliyokuwa mumewe?.
 
A: wakati nampokea hakua na mimba na wala hajawai kunambia chochote khs kua na mimba mpk anarud kwa mumewe

B: Alinieleza kisa Nini, nikaona kisa chenyewe ni kama hakina kichwa Wala miguu, Ni mdomo tu wa dada yangu ndo umepemponza, ila nikamsihi tu arudi kwa Mumewe wakayamalize.

Dada Akadai hawez Kurudi mumewe atamdhuru, Nikampigia shemej yangu, Akasema Ni Mambo madg sn ayo, atayamaliza mwnyw TU Na mkewe, nisiwe na presha. Basi sikuendelea kuhoji sn, Nikamuuliza vp nimlete sahv myamalize kabisa au vp?.

Akasema hata akipumzika kwako Haina shida, ila kesho arud TU nyumbn, Hana tatzo nae Zaid ya mdomo mdomo wake ndo umepelekea kampiga vile. Nikasema POA, atalala kwangu ila kukicha ntamleta. Akasema POA, tumeagana Safi TU.

C: MKE wangu anaumizaa na yanayoendelea kwa wifi Yake, anatamanisha sn nifanye Jambo arudiane na mumewe,maana anaamini ni Mimi pekee kwny familia nnae elewana na yule mmewe
Wakapime dna wajue,ila wanawake wenye mdomo wanamsha amsha sana nyumba,mwanamke hatakiwi kuwa mkimya sana
 
Hekima ni pamoja na kuambiana ukweli huyu bwana alikosea kumpokea na kukaa na huyo dada ake tatizo lilianzia hapo
Kwa hiyo jamaa kumtia mimba dada ake ndio ukweli na hekima yenyewe?
 
Back
Top Bottom