Ushauri: Nichague ipi kati ya BMW X3 2013 au Subaru Forester 2013

Mkuu, Subaru yangu ya pili ilikuwa SG Turbo(2004-2008), hii inanyanyasa na ni hatari.
Na bado ninayo ingawaje naiuza sasa.
Ukisikia Subaru imepinduka mara nyingi ni hizi za Turbo.
Take off speed yake ni hatari, na usipokuwa na mkono wa ku control gari itakutupa mtaroni.

SH (2008-2013) ambayo nayo ninayo sasa, haina take off speed kali lakini baada ya 120km/hr nayo valve zinazibuka, kufika 150 hadi 160km/hr, nayo inanyanyasa.
Ni gari nyepesi na very maneuverable.
Ina nafasi kubwa zaidi ndani na ni comfortable.
Ila niseme ukweli tu kuwa coolant tank yake inaweza pasuka.
Bahati yangu ilipasuka nikiwa mjini.
 
Pamoja Sana kiongozi....
Hii gari aisee lazima niagize Tu hakuna namna
 
Mkuu kuna Jirani yangu anataka kuniuzia SF5 turbo ya mwaka 2000 vipi...kwa uzoefu wako unaonaje...ni pasua kichwa au Ni kama subaru nyingine?

Yeye ni mzee sasa ana miaka 65 na ni mtunzaji sana anazingatia service na huwa hasafiri nalo umbali mrefu sana...
 
Siku hizi kucheki gari ni rahisi.
Agiza fundi wa Diagnostic Computer na atarun diagnostic check na faults zote kama zipo zitajulikana.
 
Ushaloa tayari! Kusikia mwanaume ananunua gari, ushaloa tayari πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Mimi mwanamke mbona nina magari kabla hii post ya MwanaumeπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Yaani mawazo yako ni kwamba gari maliiiii sanaaaaaaa kiasi cha kutupimia uwezo wa kumiliki🀣🀣🀣🀣
Uje nikuazime nikupe na dereva mshamba wewe😣😏😏
 
Subaru habari nyingine. Niliwahi kutembea 400 Kms Kwa masaa machache. Nilipo speed limit Ni 120kph
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…