Ushauri: Niende jeshi au niendelee na biashara zangu?

Ushauri: Niende jeshi au niendelee na biashara zangu?

Mnamwambia asiende jeshi mnataka tulindwe na nani jamani!!
Japo hata mimi sikushauri kwenda jeshi.
 
Natamani sana ningeipata hiyo nafasi.

Kwa ulivyoelezea sidhani kama wewe kuna haja ya kwenda huko jeshi
 
Mwaka Jana ulikua una miaka 24,mwaka huu una miaka 28.

Nice story.View attachment 2184875
Huezi jua mkuu labda kwake miezi 3 ni mwaka.
Huyu mbona kama wana genes za ukichaa siyo wa kumwamini.

Hawa ndo wanaofanya jf ionekane uongo ni mwingi na hata wanaotaka ushauri kiukwelikweli waonekane waongo na wapigaji au wanajitengenezea mazingira.
 
Habari za mida? Mimi ni Daktari ,doctor of medicine nina umri wa miaka 28yrs nimejiajiri nina pharmacy moja na maabara moja na nipo mbioni kufungua dispensary na pharmacy nyingine faida ninayopata kwa siku wastani ni laki 5, hapa kati imetokea changamoto mzee aliniambia niandae CV zangu ana rafiki yake jeshini yupo ngazi za juu kabisa amesema anataka vyeti.. haraka tu natinga gwanda za mabaka.

Mzee nilimkatalia nikamwqmbia hapana siwezi kuingia jeshi sababu ya kwanza faida ninayopata kwa mwezi ni mara *6 ya mshaara wa jeshi, pili nipo huru sana na biashara zangu ninaweza kufanya chochote bila shuruti ya mtu,tatu naifurahi kazi yangu.

Mzee amekuja na sababu zake kwanza amesema kwa nchi kama tanzania biashara hazitabiriki hakuna sera nzuri kwa wafanyabiashara akatoa mfano yeye biashara zake zilivyofungwa na TRA, pili jeshini kuna security kubwa iwe kuumwa au laah lakini mshahara upo pale pale tofauti na kujiajiri ukiumwa tu ukipatwa na majanga biashara lazima itetereke, tatu ni heshima,nne unakuwa na uhakika wa maisha hata biashara zangu zikiyumba basi ajira itanipa back up.

NB: Mwisho kabisa amesema niende jeshini uku nikiendelea kusimamia biashara zangu.

Naombe ushauri wenu niende jeshi huku nikiendelea na biashara zangu au nitulie na biashara zangu niachane na jeshi?
Kwanza story yako ni uongo kutokana na post zako sa zamani.

Pili usiende JESHI hata kama story yako ni ya uongo ingawa kuna ukweli ndani yake.
 
Back
Top Bottom