Ushauri: Niende Serikalini au nibaki private sector

Swadakta. Ukiwa halmashauri usipojiongeza utadumazwa na mazingira ya kazi i.e. hutaweza kupata ujasiri wa kufukuzia Fursa nyingi kama wakubwa. Ila ukishagundua game limekaaje; utapapenda kwani ni almost nobody is behind tailing you kama inavyokuwa huko private.
 
Acha kukariri sio sehemu zote kuna maeneo anayeanza anaanza na 3M
Ni kweli ziko baadhi ya taasisi/mamlaka wanapokea hii mishahara ila kupata hadi uingie hapi huo mtanange wake sio wa kitoto hapo utakuwa unapambana na watoto wa vigogo ukipenya ujue mizimu ya kwenu imekusimamia kwelikweli
 
Dah sio poa, haiwezekani kuhama taasisi?
 
Unataka uende serikalini kufanyaje? Unafata nini kipya?
 
....Wanaofanukiwa serikalini ni MACHAWA tu.....kama hauna element za uchawa nakushauri baki Private.....utanikumbuka
 
E government ndio nn kiongozi
Wakati unasubiri majibu hebu nichangie kidogo hapa: Kama unakumbuka miaka iliyopita sio zamani sana, uendeshaji wa Serikali ulikuwa ni ule wa Kianalogia. Siku hizi Utendaji wa Mamlaka za Serikali huenda Kidigitali (Egoverment). e.g. Unanunua na kulipia huduma za Serikali popote ulipo na wakati wowote kwa kutumia Mtandao wa Serikali bila kwenda dirishani au Ofisini ili ukalipe.
Hakuna tena "cha juu" labda kwa nadra sana. Hakuna usiri mkubwa kwenye utendaji wa Serikali e.g. Waziri wa Maji anaweza (akitaka) kujua kinachoendelea huko DAWASA leo bila hata kumwita mkurugenzi. kwa kutumia mtandao Website yao. Jambo hili limeziba mianya mingi sana ya Upigaji Serikalini e.g. watoza ushuru ni lazima watumie mashine za EFD n.k.
 
Kwa hiyo mtu huoni hata aibu kupokea mshahara wakt unajua kabisa hakuna cha maana ulichofanya?
Ni taasisi gani hiyo ya umma mnaishi maisha hayo ya kuzurura kutoka office hii kwenda office hii?
 
 
Kwa hiyo mtu huoni hata aibu kupokea mshahara wakt unajua kabisa hakuna cha maana ukichofanya?
Ni taasisi gani hiyo ya umma mnaishi maisha hayo ya kuzurura kutoka office hii kwenda office hii?
Nakazia hoja. Umemwambia ukweli. Ni jambo la kushangaza sana eti mTz tena msomi anamawazo hayo.
 
Nitakujibu maswali yako kama ifuatavyo.
1.Impressive CV huwa inaandaliwa kwa miaka mingi mkuu kwenye uzoefu wa kazi sasa kama umekaa tu kitaa CV yako itapanda vipi ili iwe impressive.
Tunapoongelea CV hatumaanishi kumiliki mavyeti makubwa ya darasani la hasha bali CV inahusisha zaidi uzoefu ulioupata kazini baada ya kusomea fani yako.
2.Private sector huwa hawana mtandao rasmi unaowaunganisha kampuni zote na kampuni za private huwa zina ushindani/uhasimu baina yao kama ilivyo simba na yanga(mchezaji mzuri wa yanga simba wanamnunua),mfanyakazi hodari wa Cocacola Pepsi wanamnunua,mfanyakazi mahiri wa Tigo Vodacom wanamchukua iko hivyo yaani sasa wakishaikubali kazi yako hawawezi kukuacha eti kwa vile uliacha kazi kampuni yako ya zamani,hiyo ni propaganda tu.
3.Kujiupdate namaanisha ni kuangalia je ni kipengele gani cha kazi yako kipo hot cake sokoni kwa sasa kisha unajifunza kwa vitendo kisha unakiongeza hicho kipengele kwenye CV yako na siku ukiitwa interview ukaulizwa maswali kuhusu hicho kipengele utaprove kwamba unajua kisha ukisgaipata hiyo kazi unakifanyia mazoezi zaidi ili kuwa mbobezi.
Sasa hapo utaangalia wewe ni wapi utaenda kujifunza kwa vitendo either kazini au kwenye professional courses training centres ambao wako practical oriented.
Ukifanya hivi utajikuta kila mwaka CV yako inapanda na mshahara nao utakuwa unapanda kwa spidi unayoitaka wewe.
 
Nimekupata mkuu.
 
Shukran kiongozi
 
Una umri gani? Upo fani gani? Malengo yako ni yapi?
 
Baki ulipo !! Labda ukishapata CHQ No. ukae huku ukiangalia namna ya kutoka hapo (kama unauwezo wa kufanya hivyo) kwenda kunakoeleweka kulingana na taaluma yako !! Otherwise baki ulipo !!
 
Nimekupata mkuu.
Ndio hvyo mkuu private ni kuwa na confidence inasaidia sana usiwe na wasiwasi kwamba mwakani mkataba ukiisha sijui itakuwaje sijui nitaishi vipi usiwe na haya mawazo.
Yaani mimi enzi zangu ni kijana mdogo bado niko wa moto nimetoka chuo nina kauzoefu kama cha miaka miwili hivi ukiniita interview najikoki kuna maswali ukiingia kwenye mfumo wangu kama wewe ndio HR lazima unichukue kwa mikwara na mbwembwe nilizokuwa nazo unaniuliza swali moja nakupa majibu matatu.
Ikafikia hatua nikawa malaya wa kazi na kila mwezi nahudhuria interview angalau moja.
Na ilikuwa kila mwezi nahudhuria interview moja kwa ajili ya mazoezi
 

Jibu haya maswali:

1. Shirika limeanza lini?
2. Mapato ya Shirika ya natoka wapi?
3. Una nafasi gani kwenye shirika?

Ajira haipimwi kwa mshahara peke yake, kuna factors nyingi sana!

Amua mwenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…