Ushauri: Niende Serikalini au nibaki private sector

Ushauri: Niende Serikalini au nibaki private sector

Kwanini usifanye kazi zote mbili sababu wewe ni 2in1
Anyway sijawahi fanya kazi serikalini na suitokuja kufanya japo niliwahi pata nafasi ya kwenda kufundisha DIT nikaamua kubaki zangu private sector
Hahaha we jamaa umewaza nje ya box
 
Bwana mkubwa:
1. Umesema uliomba kazi. Kwa nini uliomba i.e. ulisumbua watu halafu sasa unajishauri eti uende au usiende.
2. Qualification Professional ww ni nani au ndo Utumish i.e. Human Resources Officer? Hili ni muhimu sana niwekee wazi ili nikupe ushauri muafaka.
3. Umeshajiuliza ni kwa nini Private Sector (almost all private Sectors) uliyopo imeweka 3 yrs Contract but Renewable?????
4. Ni vizuri ukatoka nje ya box na ili upate exposure ya huko kwingine.
5. Dar itakuponza mkuu. Take it from me.
1.Niliomba taasisi kubwa ya serikali mzee na ningepata huko nisingejishauri kwa chochote ningeenda sema nilikosa nafasi jina likabaki kwenye database ndio wamenipangia huko halmashauri sahv ambapo sikuombea ajira nimepangiwa tu
2.Mechanical Engineer
 
Wakuu habari, niliomba kazi taasisi flani ya umma (utumishi) sikupata nafasi jina langu likahifadhiwa kwenye database juzi kati kuna mkeka wa kuitwa kazini umetoka na jina langu likiwemo kwenye kazi za halmashauri. Ila kwa sasa kuna taasisi binafsi nafanya kazi ambayo nalipwa vizuri sana nimefuatilia mshahara wa hapa ni zaidi ya mara mbili ya mshahara huo wa serikalini na haki nyengine zote za mwajiriwa napata kama bima n.k ila changamoto ya hapa private mkataba wao ni wa miaka 3 ila unarenew kila mkataba unapoisha hawana shida.

Serikalini nimepangiwa Tabora na mimi makazi yangu miaka yote ni Dar sasa nikienda huko naenda kuanza moja.

Nilifikiria kutoenda huko ila kuna mtu kaniambia nisipoenda utumishi jina langu litakuwa blacklisted na sitopata tena nafasi nyengine ya kuingia serikalini maisha yangu yote.

Kuna ukweli wowote juu ya hili au nifanye nini wakuu I'm so confused nakosa usingizi kabisa.
ni ngumu kukushauri, because hatujui terms za huko private Vs public!
 
1.Niliomba taasisi kubwa ya serikali mzee na ningepata huko nisingejishauri kwa chochote ningeenda sema nilikosa nafasi jina likabaki kwenye database ndio wamenipangia huko halmashauri sahv ambapo sikuombea ajira nimepangiwa tu
2.Mechanical Engineer
Ndio umepangwa halmashauri ya nzega mkuu
 
Mwenye jibu ni wewe mwenyewe.Kwa sababu ni wewe uliyeomba hiyo kazi huko serikalini huku ukiwa muajiriwa wa private sector.Je ulilenga nini kuomba kazi wakati una kazi?mbona umezuia nafasi za wenzako.
Hana budi kuachia kijiwe aendee huko serikalini aliko kutaka
 
Bwana 2in1 heri kwako.
Jitathmini, nini hasa malengo ya maisha yako!
Hujasema hapo ulipo umesha renew mkataba mara ngapi na uwezekano wa kuendelea ku renew upoje.
Serikalini kuna job security ingawa malipo ni kidogo, inapaswa uwe na akili ya ziada above kuvalishwa vitenge vya mwenge.
Nimeshakutana na waajiriwa wa serikalini lakini pia wanatumia nafasi zao kukuza network (and eventually) biashara zao. Kumbuka issues nyingi mfano businesses na Projects zinaanzia/zinapitia serikalini, na ukiwa serikalini unakuwa na access ya taarifa sahihi kuhusu programs/Projects, funders
Waweza kuwa Mwajiriwa na pia ukawa private Consultant, farmer, engineer, trader, NGO owner etc
So waweza kwenda serikalini kwa purposes (1) job security (2) networking
Nakushauri nenda Tabora, Tanzania ni yetu sote.
fuata huu ushauri utakuja kushukuru baadaye.
 
Nenda serikalini mkuuu awamu hii serikalini kuna pesa acha kuwaza
 
Wakuu habari, niliomba kazi taasisi flani ya umma (utumishi) sikupata nafasi jina langu likahifadhiwa kwenye database juzi kati kuna mkeka wa kuitwa kazini umetoka na jina langu likiwemo kwenye kazi za halmashauri. Ila kwa sasa kuna taasisi binafsi nafanya kazi ambayo nalipwa vizuri sana nimefuatilia mshahara wa hapa ni zaidi ya mara mbili ya mshahara huo wa serikalini na haki nyengine zote za mwajiriwa napata kama bima n.k ila changamoto ya hapa private mkataba wao ni wa miaka 3 ila unarenew kila mkataba unapoisha hawana shida.

Serikalini nimepangiwa Tabora na mimi makazi yangu miaka yote ni Dar sasa nikienda huko naenda kuanza moja.

Nilifikiria kutoenda huko ila kuna mtu kaniambia nisipoenda utumishi jina langu litakuwa blacklisted na sitopata tena nafasi nyengine ya kuingia serikalini maisha yangu yote.

Kuna ukweli wowote juu ya hili au nifanye nini wakuu I'm so confused nakosa usingizi kabisa.
Mkuu baki private sector ila jitahidi uwe unawekeza pesa kama kununua Viwanja na kufungua Biashara za kukuingizia extra income.Dar es salaam kuna opportunities nyingi kuliko Tabora na pia serikalini utakacho ambulia labda job security compared to private sector.
 
Dj niletee watu wa "take it from me, utakuja kunishukuru baadae"
 
1.Niliomba taasisi kubwa ya serikali mzee na ningepata huko nisingejishauri kwa chochote ningeenda sema nilikosa nafasi jina likabaki kwenye database ndio wamenipangia huko halmashauri sahv ambapo sikuombea ajira nimepangiwa tu
2.Mechanical Engineer
OK.
1. Hapo na. moja umeipiga chenga (umekwepa) hoja yangu kwenye post #55. Lakini hiyo itoshe tu kukuhakikishia Serikali ni MOJA Tanzania hiyo kuitwa H/W au Central Gvt. au Taasisi haijalishi kitu alimradi ni ndani ya Serikali na ndo mana wakakupanga kule ambako ww kwa imani yako unasema hukuomba. Iko hv; Ukiomba Serikalini wao kama Serikali huangalia ni wapi pana upungufu na uhitaji mkubwa wa Taaluma yako na huko ndiko watakupanga.
2. Hongera sana kuwa umebobea katika Mechanical Engineer. Kwenye Halmashauri ndiko hasa Taaluma yako inahitajika - unless useme hupendi kuwa chini ya DED. Halmashauri ndizo ziko frontline tena karibu zaidi na wananchi na ndiko miradi yote hutekelezwa. Ukiwa Fundi mitambo na umeajiriwa Serikalini e.g. kiwandani n.k. bado wanaweza kukuhamishia Halmashauri au kukushikiza (on secondment basis) katika Taasisi nyingine hata zile za kutoka nje ya nchi na huwezi kataa. Kumbuka ukiomba kazi Serkalini hauombi kituo cha kazi. Utapangiwa popote Tz. Ndo mana wakakupanga Tabora.
 
𝚖𝚣𝚎𝚎 𝚔𝚒𝚖𝚋𝚒𝚊 𝚑𝚊𝚛𝚊𝚔𝚊 𝚐𝚟𝚝, 𝚜𝚑𝚊𝚞𝚛𝚒 𝚢𝚊𝚔𝚘 𝚘𝚏𝚏𝚒𝚌𝚎 𝚣𝚒𝚔𝚒𝚞𝚗𝚐𝚞𝚊 𝚑𝚞𝚔𝚘 𝚞𝚕𝚒𝚙𝚘 𝚗𝚍𝚒𝚘 𝚋𝚊𝚊𝚊𝚊𝚊𝚜𝚜𝚜 𝚗𝚍𝚒𝚘 𝚋𝚊𝚜 𝚝𝚎𝚗𝚊.
𝚂𝚊𝚜𝚊 𝚠𝚎𝚠𝚎 𝚓𝚒𝚌𝚑𝚊𝚗𝚐𝚊𝚗𝚢𝚒𝚜𝚑𝚎 𝚝𝚞 𝚙𝚛𝚒𝚟𝚊𝚝𝚎 (𝚞𝚜𝚒𝚛𝚒𝚗𝚒)
 
Private kuna majungu na fitna mkataba mpaka umnyenyekee mtu hapana private hata wanipe million 10 kuna jamaa aliacha kazi private licha ya kulipwa hela nyingi kwasababu ya majungu na fitna mkuu nenda serikalini kuna siku utakuwa na familia.
 
Kama siyo competent wahi serekalini kule hata uwe mbabaishaji unaenda kazini hufanyi kazi unazurura tu kutoka ofisi hii kwenda ofisi ile hadi jua linazama mshahara utapata wakikuchoka na ubabaishaji wako wanakuhamisha tu
Ila huo ujanja ujanja usiujaribu private sector wanakutumbua kabla hujavuta pumzi ya pili
 
Hapo kuwa na familia sijaelewa point yako mkuu
 
Hapo kuwa na familia sijaelewa point yako mkuu
Mimi nimefanya kazi private company tena international walikuwa wanalipa vizuri sana ila kwa fitna zile kuna siku watakupiga tukio hutaamini nina visa vingi ila nakushauri nenda serikalini ukithibitishwa chukua mkopo kama million 12 fanya bussness endelea kupiga kazi usiwe kama wale washamba anachukua mkopo wa kwanza kijana mdogo ananunua gari mwingine anajenga tena nyumba ya kukaa mbali na anapofanyia kazi nenda serikalini chukua mkopo fanya bussness sasa huo mkataba wa miaka mitatu ni bank gani itakupa mkopo labda oya microfinance siku ukija kuwa na familia kama hauna utakuja kunielewa vizuri.
 
Kama siyo competent wahi serekalini kule hata uwe mbabaishaji unaenda kazini hufanyi kazi unazurura tu kutoka ofisi hii kwenda ofisi ile hadi jua linazama mshahara utapata wakikuchoka na ubabaishaji wako wanakuhamisha tu
Ila huo ujanja ujanja usiujaribu private sector wanakutumbua kabla hujavuta pumzi ya pili
Wee bhana usimdanganye mwenzio. Unasema eti "Kama siyo competent wahi serekalini kule hata uwe mbabaishaji unaenda kazini hufanyi kazi unazurura tu kutoka ofisi hii kwenda ofisi ile hadi jua linazama mshahara utapata wakikuchoka na ubabaishaji wako wanakuhamisha tu....." sio kweli. Cjui kwa siku hIzi lakini siku za nyuma kulikuwa na fomu za kujaza almaarufu kama OPRAS.
 
Sasa sijui unabisha nini
 
Back
Top Bottom