Ushauri: Niende Serikalini au nibaki private sector

Ushauri: Niende Serikalini au nibaki private sector

Karibu tabora mkuu,sijui wilaya gani,privet sectors kuna mambo mengi mno licha ya mishahara minono,na kufukuzwa ni kugusa tu, huku halmashauri kuna pesa nyingi mno za dili mshahara ni geresha tu, karibu tabora, nitumie namba yako pm tuzungumze.
 
Wakuu habari, niliomba kazi taasisi flani ya umma (utumishi) sikupata nafasi jina langu likahifadhiwa kwenye database juzi kati kuna mkeka wa kuitwa kazini umetoka na jina langu likiwemo kwenye kazi za halmashauri. ila kwa sasa kuna taasisi binafsi nafanya kazi ambayo nalipwa vizuri sana nimefuatilia mshahara wa hapa ni zaidi ya mara mbili ya mshahara huo wa serikalini na haki nyengine zote za mwajiriwa napata kama bima n.k ila changamoto ya hapa private mkataba wao ni wa miaka 3 ila unarenew kila mkataba unapoisha hawana shida. Serikalini nimepangiwa Tabora na mimi makazi yangu miaka yote ni Dar sasa nikienda huko naenda kuanza moja. Nilifikiria kutoenda huko ila kuna mtu kaniambia nisipoenda utumishi jina langu litakuwa blacklisted na sitopata tena nafasi nyengine ya kuingia serikalini maisha yangu yote. Kuna ukweli wowote juu ya hili au nifanye nini wakuu I'm so confused nakosa usingizi kabisa.
Nenda Serikalini bob .
Hakuna kusumbua Kichwa..

Ila usipoenda sahau Daima kupata hiyo chance
 
Hapa utapata maushauri kibao lakini final decision itakuwa mikononi mwako. Kwa upande wangu kwenda kuanza kazi serikali ukapata hayo ma network wanayosema hapa itakuchukua not less than 3-4 years. Ukienda serikalini na hayo MaTSDG ya mishahara utakesha na kupiga kwata muda mrefu. Utakuwa desk officers na kazi wala majukumu ya kuingiza ma$. Newcomers mpaka uje upate hayo ma-deal, connection, safari ili upae $, utakesha sana.

Baki private sector, ongeza ufanisi, anzisha biashara, ongeza connection maisha yatakwenda vizuri tu
 
Wacha kutishwa kama katoto kadogo wewe yaani ukiambiwa hautakuja kufanya kazi serikalini unaogoopa kwani umezaliwa kufanya kazi serikalini? Kutangatanga sio kuzuri baki ulipo na utengeneze mambo yako vizuri na huo mshahara wako wa mara 2 ya wa halmashauri
Ushauri wangu ni huu japo Mimi sio evilspirit
 
Hapo sasa inategemea na malengo yako, Serikalini (Local Gvt) exposure ni ndogo sana ama hakuna kabisa.
Pia, itategemea na idara uliyopo.

Kama unahitaji kukua, exposure baki Private sector. Lakini pambana haswa kwani wao wapo kwa ajili ya profit na sio Service kama ilivyo kwa Serikali.

Salary unayoipata huko ukiipangia mipango vilivyo itakuanzishia kitu kingine cha kukuongezea kipato mbali ya ajira pasipo kuingia madeni ya mikopo na kwa muda mfupi.

Private sector utatengeneza CV yako nzuri na hata siku mkataba ukiisha ama mradi kuphase out CV yako itakuwa na soko zaidi kuliko ile ya upande wa pili. (Kama unahitaji kukua).

NB: Ukienda kule utadumaa kiakili kwani maarifa utakayokuwa unahitaji kuyaimplement yatakosa nafasi.

Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom