Usipime sana kazi kwa kiwango cha malipo unacholipwa bali angalia factors nyingine nyingi. Mf hapo ulipo kama hicho unachikipata ndani ya mkataba mmoja unaweza kutimiza malengo yako ya muda mrefu baki, mf. Unaweza kujenga ndani ya muda mfupi na kuanzisha uwekezaji mwingine ambao hata mkataba wako ukiisha au kusitishwa huwezi kuanza kuhangaika hangaika na kulia huku na kule.
Pili jikite kwenye faida za muda mrefu sio muda mfupi hasa juu yako mwenyewe baada ya miaka 10,15,20....,familia yako hasa watoto kuwasomesha mpaka mwisho bila kukwama njiani.
Mkeo, wazazi na wategemezi wengine.
Tatu angalia umri wako je bado kijana sana una future ndefu au tayari una majukumu ya familia au wategemezi.
Mwisho kitu chochote chenye ushindani mkubwa jua kinathamani kubwa hata kama haionekani kwa macho leo.
NB. Swali kwa nini watoto wa vigogo na viongozi wakubwa haijalishi wamesoma wapi, wana mitaji mikubwa ya kuweza kuwekeza au kuanzisha miradi au business kubwa kubwa.... Lakini wazazi wao wanahakikisha wanapata ajira selikarini???? Why????? Kwenye maisha fikiria miaka 20 ijayo au zaidi sio fikra za 2025 na 2027.