Ushauri: Nimekuja kugundua naishi na mwanamke ambaye amewahi kuugua Ukichaa

Ushauri: Nimekuja kugundua naishi na mwanamke ambaye amewahi kuugua Ukichaa

We ishi nae tu mkuu, kwan amekuletea mawenge yoyote??....we endelea kufurahia maisha kama kawaida siku kikiibuka kichaa hospital zao zipo na wanatibiwa tu kama magonjwa mengine, kikipona ama kutulia unaendelea kula tamu yako bn

Unawezakuta aliyekufikishia ujumbe hana nia njema pia aisee, chakufanya pia kama anao ujacri wa kusema mbele ya mke wako maneno aliyokupa ni sawa ila kama hawezi Kuna tatizo.

Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako
 
Kikubwa msaidie kwenye matumizi ya dawa zake tu. Ugonjwa wa akili ni tatizo kama vile Malaria au UTI, utofauti lenyewe ni sugu na la muda mrefu.
Chukua hili wazo.. Lina utaalam ndan yake manake akiacha tu anakutwa na madnes
 
Kuna mwanamke naishi naye mwezi wa Sita Sasa ila nimekuja kuambiwa na mtu wa karibu kutoka Familia yao kuwa huyu mwanamke alishawahi kuugua ukichaa mwaka 2015 akatibiwa akapona. Tatizo ni mie baada ya kujua nimeanza kuogopa. Je hili likoje? nishawahi sikia kua mtu kama aliwahi kua kichaaa huwa kinarudi tena hata bada ya miaka kadhaa, Je ni Kweli mtu akiwahi kuwa kichaa huwa hakiponi kabisa bali kinatulia hata miaka kadhaa halafu kinarudi?
Mkuu ni vzr kufanya utafiti , kama huyo ndugu yake yupo ni vzr kujua ni hospitali gani, hizi nyaraka huwa zinahifadhiwa kwenye kumbukumbuku

Yawezekana ilisababishwa na malaria au kitu fulani nakuomba ufanye uchunguzi yawezekana ukaja kumletea huo ukichaa mara mbili na siku zote mtu ambaye alishaugua huo ugonjwa kama hakupona vzr unaweza kujua mwenyewe maana mda mwingi uko naye

Usiwe na haraka
 
Sema hivi, wakuu nimeshajisevia saizi yangu nashindwa kusepa.

Wakulungwa watakupa mbinu za kutemana na huyo mwanamke.

Haya mengine ni ngonjera tu ushashiba hapo ugali wa mchana shubamit.
 
Afadhali wewe umepata taarifa kamili. Kuna mwenzako alirudi kutoka kazini akakuta suruali zake zote zimekuwa kaptura.

Kama mnaishi pamoja lazima muaminiane. Kaa nae chini mliongelee hili. Akikueleza dawa zilizomsaidia kupona pia mfanye miadi na mtalaamu wa afya ya akili awape ushauri nasaha.
 
Kuna mwanamke naishi naye mwezi wa Sita Sasa ila nimekuja kuambiwa na mtu wa karibu kutoka Familia yao kuwa huyu mwanamke alishawahi kuugua ukichaa mwaka 2015 akatibiwa akapona. Tatizo ni mie baada ya kujua nimeanza kuogopa. Je hili likoje? nishawahi sikia kua mtu kama aliwahi kua kichaaa huwa kinarudi tena hata bada ya miaka kadhaa, Je ni Kweli mtu akiwahi kuwa kichaa huwa hakiponi kabisa bali kinatulia hata miaka kadhaa halafu kinarudi?
Umeanza kuogopa nini ngosha,...." ....life spin in a very strange & mysterious orbit..... no one can guess exactly what/how his/her tomorrow gonna look/sound like....

Huyo anaweza kuwa ni mke bora kabisa kwa maisha yako yaliyobakia hapa duniani.

Stop worrying.
 
Siku akiamka akachukua shoka akakutenganisha mguu urudi Tena hapa kutupa mrejesho. Wengine huwa ni magonjwa ya familia m2 akishakuwa na shida kichwani always be cautious unapodeal nae.
 
Wasi wasi wako upo wapi? Unataka kumuacha kisa aliugua kichaa?
Unaijua kesho yako? Kama unaijua basi umuache huyo mwanamke.
Waswahili husema 'Haujafa haujaumbika'
🌎
Kuna mwanamke naishi naye mwezi wa Sita Sasa ila nimekuja kuambiwa na mtu wa karibu kutoka Familia yao kuwa huyu mwanamke alishawahi kuugua ukichaa mwaka 2015 akatibiwa akapona. Tatizo ni mie baada ya kujua nimeanza kuogopa. Je hili likoje? nishawahi sikia kua mtu kama aliwahi kua kichaaa huwa kinarudi tena hata bada ya miaka kadhaa, Je ni Kweli mtu akiwahi kuwa kichaa huwa hakiponi kabisa bali kinatulia hata miaka kadhaa halafu kinarudi?
 
Sikiliza ile nyimbo ya "Upendo" yule binti aliugua kichaa lakini jamaa akaoa ivyo ivyo ..nimesahau mwimbaji ..sikiliza halafu utanishukuru baadae.
 
Achana naye huyo ataleta kichaa kwenye ukoo wenu wazee zamani walikuwa makini na hizo mambo jiandae mkuu
 
Inategemea kilichomfanya apate ukichaa, Kama ni vitu Kama depression nk Hicho hakitarudi, lakini cha ukoo /kurithi ni Kimetulia tu Siku yoyote ataamsha
Mleta maada jaribu kufuata ushauri wa huyu jamaa .
Mie nilipataga stress mbaya Sana afu nikaishi nazo muda mrefu.
Sure Cha kurithi sio Ila Cha kupoteza kitu Cha thamani Cha maisha yako unaugua utapona.
Mfano ukiibiwa 500M na ndo haso zako zote
 
Na ndo masuala haya kupendana mjini umemuona mtu kisa ama umbile zuri,kazi nzuri,ni msomi,maisha mazuri,ameng'aa unatongoza anakubali unanogewa unatangaza ndoa.

Ndoa bana unaleta damu kwenye ukoo wako ujue.

Ishu na mtu unayejua chimbuko lake haswaa mpaka ndugu zake wote unawafahamu.

Sie unaletewa ma ex unaambiwa huyu wa anti,anko ama wa bamdogo kumbe huwajui wote.
Nishawahi pelekwa sehemu ivyo Tena nikalalapo kuwa ni MTT wa anko wangu nikaambiwa na jina nitakalojitambulisha liwe na ubini wa ukoo wao kabla sijaoa.
So nilichukua SoMo.

Mie lifestyle ya babu zangu nimezunguka Ila naikubali Sana.

Wanachagua Koo wanaijua a to z. Sie vijana tunachagua muonekano.
So nilitumia ushauri wao.so usidharau watu kisa una kadigirii kamoja ama tutatu,Mana elimu sio maisha. Uzoefu wa maisha haupati kwa miaka mingi ya darasani.
 
My beautiful wife baada ya kujifungua first born alipata ugonjwa wa akili yaani Depression after birth ( postpartum ). Ilinipa shida lakini thanks to God nilitatua na baada ya miezi 3 akawa sawa baada ya matumizi ya dawa za kutuliza akili na kuendelea na shughuli zingine.

Na kwa mtoto wa pili tena ilitokea hivyohivyo and this time nilimuanzisha clinic ya akili na yuko sawa akiendelea na majukumu. Lakini jambo la msingi nilijielimisha mimi kwanza juu ya tatizo lake and then nilikaa naye chini yeye binafsi kuikubali hali yake na kukubali matibabu badara ya kufikiri analogwa.

I love her very much kwa kuwa combination yetu imetokeza very beautiful girl and handsome boy wenye akili darasani pia.

Sometimes maisha na stress vinaweza kufanya uwe kichaa na tukumbuke kila mtu ana tatizo lake sugu lisilovumilika.

Ikitokea mkiwa tayari kwenye ndoa na mna watoto tayari hakuna namna. Lakini kama mchumba ndio ana tatizo hilo basi una uhuru wa kuamua kusuka au kunyoa si lazima kuendeleza mahusiano ambayo tayari una wasiwasi nayo na haitakuwa na afya kwa penzi lenu
 
Back
Top Bottom