Ushauri: Nimemaliza chuo, nina mtaji wa 2M. Naweza kufanya biashara gani?

Nikifikiria zaidi kusambaza Mchele sababu najua unapopatikana kwa bei rahisi lakini nikaja kufanya research nikagundua shule nying iwe serikali iwe private inahitaji maharage kwa wing kuliko Mchele wala Unga! Lakini wa hii 2M yangu nilitaka kuomba tenda kwa hizi private school!, kwa Mchele sana sana Ila na doubt! So kwa hizo private ndo sijajua ulipaji wao upoje?
Nimesoma shule private mwaka 2014 tulikua tunakula maharage yaliyobunguliwa, Unga sometimes ulikuwa umeoza
nilipo ingia advance ndo kabsa maharage yale yenye wadudu ndo maana nimetamani hii business, no 2.
Asante kwa mawazo pia
 
Ttz la wazo lako lipo zaidi ya miaka 20 mbele kwa hapa bongo 😄
 
Nashukuru mimi sichagui kazi Ila kwenye eneo hapo ndo mtihani!
Unapoajiriwa ndio usichague kazi ila unapojiajiri unatakiwa uchague kazi na mostly huwa tunaangalia upande ambao ni bora kwetu, kila mtu anakitu chake ambacho anaamini ni bora na hata akikifanya anakifanya kwa ufanisi then unaangalia kama hiko kitu kinaweza kuwa fulsa ya kukupatia pesa ila kama hakiwezi kukupatia pesa ndio unaangalia option zingine.

Biashara nyingi ambazo zinaanzishwa kimasihara ndizo ambazo huwa zinafikaga mbali na huwa zinaanzishwa kimasihara coz zinaanzaga kama passion then baadae ndio muhusika anaona anhaaa kumbeeee.

So ushauri wangu anza na kile unachokipenda then angalia namna ukifanye kiwe fulsa coz kwakufanya hivyo hautajali hata wanunue au wasinunue but utaendelea kufanya kwasababu unapenda unachokifanya.

Umri wako bado mdogo na ndio umri mzuri kwenye kipindi cha try and error so mostly utafeli kwenye biashara nyingi sana and always odds huwa ziko hivyo unapoanzisha biashara yoyote probability ya kufeli huwa ni kubwa kuliko ya kufanikiwa so usijipe matumaini makubwa sana juu ya huo mtaji and usifanye biashara kisa umeskia mtu fulani alifanya na akafanikiwa sana kwasababu wewe unaweza ukaenda ukashindwa kufanikiwa.

Najua unaweza usinielewe ukisoma juu juu hiko nilichoandika ila nataka tu nikuamshe kwamba unatakiwa ukae katika hali ya utulivu wa akili and ask yourself deeply unahisi wewe ni bora zaidi katika upande gani na biashara za namna gani ambazo huwa zinakuchukulia mawazo yako yote wakati unapofikiria maisha hayo ya biashara, then anzia huko.

Haya mawazo mengi ya humu utapewa kulingana na mafanikio ambayo watu waliyapata baada ya kufeli kwenye biashara nyingi ambazo waliwahi kuzijaribu.
 
Kitu nachokipenda ni entertainment mziki na sehemu za kurefresh like kuown club, ukumbi ambapo watakuwa wanafanya sendoff, birthday Yan sherehe zote kwa ujumla kwenye upande huo Ata napokuwa kwenye sherehe yoyote nipo vizuri kwenye namna ya kuorganize kwa sababu nimerudi mkoa huku ss wasukuma sio watu wa entertainment sana ni kazi kazi lakini for my age kuown such asset ni mtiti kiwanja tu ni 10Million heka moja kwa huku kwetu eneo la barabarani ni 60M and above so inabidi nianze na kitu kidogo ili nisikose fedha ya kujikimu kuliko kutumia cheti changu kwenda kuzunguka nacho
 
Fanya hiyo biashara ya chips ni nzuri na mtaji wake hata 1m haufiki. Pesa nyingine utaweka akiba. Na biashara ya chakula ndio biashara inayotoka sana kuliko biashara ya nguo.

Hiyo biashara ya vinywaji ni pasua kichwa sana, yani kwa katoni moja unaweza kukuta unapata 500 faida. Lazima uuze Sanaa ili faida ionekane. Lakini kwa chips faida utaiona haraka. Uweke na mishikaki na kuku na ujitahidi usafi
 
Wewe naye sasa umesema una mtaji milioni mbili mara unataka ufungue Duka la vinywaji jumla mara ukajenge ukumbi kweli mdogo wangu au ulimanisha?
 
Kaka pata mawazo humu alafu pita mitaani fanya research sawa...

Biashara kama biashara ukishapata humu nenda kwa watu ambao wanafanya hiko kitu alafu kaa nao at least hata week ...

Au fanya ile ya share an umepata wazo humu sasa wewe nenda kwa mtu ambaye tayar ana hiyo ishu alafu wewe nenda pale ukaombe share uongeze kitu mpige kazi
 
Biashara zinazotokana na majibu ya swali lako zinakufaga kibudu mapema sana.

Mimi kila siku nasema ukiona biashara yoyote imedumu miaka mingi basi jua inafuata kanuni hii "inatatua matatizo ya watu wa eneo husika ndio maana watu hao wapo tayari kuipa pesa kila siku"

Sasa fanya hivi zungukua hapo geita chunguza matatizo na changamoto au uhitaji wa watu wa geita kisha andaa suluhisho.Make business around your solutions utatoboa.

The market doesn't care about your business ideas kama hutatui uhitaji wao.
 
Wewe naye sasa umesema una mtaji milioni mbili mara unataka ufungue Duka la vinywaji jumla mara ukajenge ukumbi kweli mdogo wangu au ulimanisha?

Wewe naye sasa umesema una mtaji milioni mbili mara unataka ufungue Duka la vinywaji jumla mara ukajenge ukumbi kweli mdogo wangu au ulimanisha?
Soma kwa makini hadi mwisho mambo kujenga hayo ni mawazo ambayo nayafakiria maybe for 6 years to come but kwa now kama nilivosema mwishoni nataka kufanya kibiashara kidogo kidogo cha kunikwamua kimaisha ili nisiwe tegemezi Tena home
 
Dah we jamaa hili wazo lako mbona la kimkakati sana hahahahah!
 
Mbona huku Njombe na Makambako tunauziwa 1,900/= hadi 2,000/= kifaranga kimoja.... Imekaaje hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…