Ushauri: Nimeokota wallet yenye Tsh. 50,000 pamoja na risiti za miamala ya pesa nyingi nahofia kurudisha nahisi naweza bambikiwa kesi

Ushauri: Nimeokota wallet yenye Tsh. 50,000 pamoja na risiti za miamala ya pesa nyingi nahofia kurudisha nahisi naweza bambikiwa kesi

Fikiria hili tukio. " Police mmoja, trafiki, na mbwembwe zake alikamata gari ya jamaa. Jamaa akashuka na police akapanda ile gari na kuipeleka central police. Jamaa palepele akaingia benki kwenye account yake akachomoa 10M akaweka anapojua. Akafuata gari yake fasta police. Alipokabidhiwa gari akadai haoni mzigo wake katika bahasha aliyoiacha ndani ya gari, 10m. Kufupisha maelezo, kusovu tatizo wakataka ushahidi benk; ikaonekana mda uleule jamaa alikuwa ame-withdraw kiasi hicho cha fedha. Bila ubishi police aliingia hatiani akalipa ile fedha".
Ishauri sasa, weka chini hiyo wallet, sepa.
Polisi trafic akalipa mil 10? Serious?

Basi walikuwa sio makini , risiti ya bank inaoneaha umetoa hela saangapi,pia bank huwez toa hela dakika hio hio labda mikoani huko

Pia police aliendaje na gari police pekeake . Hio wangepeleka mahakamani hashindi huyo jama
 
Nina maanisha kwamba, kama Ile receipt iliambataana na hizo pesa nikiwa na maana zimetolewa kwaiyo kama zilikuwa kwenye bag na ndani ya bag Kuna wallet nahisi itakuwa rahis kusema nimeibiwa pesa nyingi Zaidi kwasababu iyo wallet ilikuwa kwenye bag lenye pesa mana nilikuwa nimetoa pesa na receipts zote zipo kama ushahidi.
Mazingira ndio yatakuweka salma

Lakini Kama unahisi hivyo basi hivyo vitu achana navyo . Toa hela wallet kaiache barabarani itupe .

Hio hela usiitumie ,ukiwezekana kaitolee sadaka yote usitumie
 
Hata akiipeleka polisi, hiyo hamsa polisi watatia kwapani kisha mwenyewe ataitwa aje kuchukua maratasi yake.

Muhimu hapo chukua hamsa yako, hiyo wallet mpe bodaboda wale wanaovaa ndala moja inaning'inia(vishandu) mwambie apite kituo cha polisi na ukali kisha aitupie kituoni halafu atembee na ukali.
Mchafuzi wa lugha, mzee kifimbo cheza kazeeka la sivyo ungekiona 🤣
 
Uko wapi nikupe akili?

Hivyo vitambulishi majina ya dini Gani?

Sijakwambia uchukue elfu hamsini ila hizo risiti na vitambulishi na wallet peleka kanisani.

Viache hapo
 
Ni wallet yangu Kama unaogopa ntakumbambikia kesi basi nenda kwa wakala nitumie hiyo 50k yangu alaf wallet tupa hapohapo
 
Tumia hela hivyo vingine tupa wataokota wengine
 
Hata Mimi,bila shaka ningepatwa na hofu tena hofu ya wayahudi...
situation inatokea umeokota wallet ina pesa na IDs kuitumia unaogopa kurudisha pia unaogopa, kurudisha ulipoiokota napo unaona ni ushamba 😳
 
Nimeokota wallet ina pesa kiasi cha elf 50,000 ila ina risiti ya miamala ya Milioni 45 pamoja na Milioni 10m. Tarehe ni siku niliookota, ndani kuna pia kitambulisho cha bima, nk.

Nahofia kurudisha anaweza kunibambikia kesi ya kupoteza pesa zake!

Nahisi anaweza kusema wallet ilikuwa na pesa hizo.

Naombeni ushauri.
Cha kuokota sio cha kuiba mkuu.

Tumia hio Fedha kiasi kwa kuwasaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu inayobaki fanyia mambo yako.

Hapo utakua umejitakasa kwa sababu ukiirudisha unaweza kubambikiziwa kesi nzito kama ukabaji ama kuvunja na kuiba
 
Hakuna wallet inayoweza kuhifadhi kiasi hicho cha pesa. Millioni 45 labda mkoba.
Kuna yule jamaa wa futuhi wa kuitwa "Wa kukurupuka" soma vizuri alichoandika mleta mada
 
Back
Top Bottom