Yaani elfu 50 ni kubahatika!!!!! Watu mna roho ngumu. Ingekuwa hata hela unayoweza kununua jumba sawa. Hiyo ukipanda daladala masaa mawili imeisha!!!
Siku za nyuma mtu alikosea akatuma laki moja kwenye namba yangu. Nikiangalia,namba ni ngeni. Nikajiuliza nani huyu ananipa hela ya siku kuu, na nilivyopinda hivi. Sikuitoa. Baada ya kama nusu saa, akapiga mdada, anaomba samahani, na kwamba alikuwa anamtumia mama yake mzazi hela ya siku kuu. Akaomba nikate 20k basi nimrudishie 80k. Nikafanya hivo. Badae roho ikakataa. Hii pesa si harari yangu, hujui kaipatapataje, na yenyewe nikamtumia. Hakuamini. Hatufahamiani, ila sometimes salamu salamu.
Kuna vitu vingine ni vidogo siyo vya kukushushia hadhi, na wakati mwingine unaweza kukuta kitu kidogo kama hicho kimekufungulia mlango.