Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025

Mama Hana shida ...yupo mpaka 2030 utake usitake!
 
Huyu mama kuna muda nikimtafakari nakoswa majibu , ametupeleka mpaka kwenye hatari yaani ndani ya mwaka mmoja tu kila kitu kinaharibika zaidi ,[emoji22][emoji22]
 
Kama magu aluvyokua anawakumbatia kina makonda, na wenzao waleeee...
Kila kiongozi yeyote duniani ana rafiki zake pendwa hata wakosee vipi hawezi watumbua.
 
Hoja yako imefeli kuonyesha hujui sababu ya znz vitu bei rahisi kuliko bara, hujui mambo ya nchi yaendavyo unafata mkumbo tu,
Huna tofauti na walalahoi waliodanganyika na yule mwovu kua kila alifanikiwa ni mwizi na mchawi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Bila tajiri maskini hana maisha....
 
Yatashuka kwa senti ndogo sana kulinganisha na yalivyopanda
 
Nasema kwa kuwa ninaishi na kukutana na watanzania wengi tu huku mtaani kwangu ambako watu wanaimani kubwa Sana na mh Rais wetu na wanaridhishwa na utendaji kazi wake ulio tukuka na wenye kugusa maisha ya watu hasa wanyonge
Huo mtaa unaishi wewe itakua ni kuzimu.
 
Reaction from the ground ya wananchi kuhusiana na huu utawala ni mbaya mno.

Wananchi wanaumizwa mno na hizi tozo.

Na kodi iliyowagusa mno ni ya wapangaji.

Hiyo imekita kwenye mfupa kabisa.

Ni kwakua tu wananchi wanahofia kusema publicly ila akitokea mtu atakayejitoa mhanga kupinga mambo haya hadharani.

Atapata support kubwa sana itayoshangaza wengi.

Serikali iachane na huu utaratibu wa kuleta matozo yasiyokuwa na tija, yanachochea hasira kali mno ndani ya wananchi.

Siku si nyingi tutakuja tafutana hapa na kuanza kulaumiana.
 
Mkuu, umeandika mada nzuri sanaa na pia umetoa mifano halisi.

Naubga mkono mada yako kwa 100%

Maisha yamekuwa magumu mno na mama hana makali kwa watendaji wake hasa huyu Waziri wa TOZO
 
Naunga mkono hoja.

Na sio lazima hio 2025.
Hata 2023 itakuwa vyema
 
Tufanye kazi kaka,kubadilisha uongozi sio kigezo cha wewe kufanikiwa.Mama anafaa na tambua kuwa tuligawanyika mama kaja katuweka pamoja.binafsi namkubali sana ikiwezekana akipewa miaka kumi tutakuwa mbali sana.Hata usimba na uyanga tulionao utaondoka
 
Hakika mawazo kama haya yatazidi kuididimiza Tanzania. Mtu umeshakariri kabisa kuwa kuwa CCM ndiyo wana haki ya kukuletea mtu. Ama! Kwa nini usipiganie haki ya kuchagua kiongozi anayefaa na unakubali kuletewa ''jitu''?
pendekeza Wewe kiongozi yupi unataka achukue nchi tofauti na CCM?
 
Apa dawa tukung'utane wenyewe kwa wenyewe italeta funzo kwa Kila mtawala atakae kuja kuheshimu anaowatawala ataiyo Katiba watu wanayoisema aitakua na mana kwakua asilimia kubwa watu wametawaliwa na mapenzi ya vyama kuliko maslahi mapana ya nchi
 
Ule utawala wa kijinga ulishakuingia damuni. Siku hizi unaishi kwa amani halafu moyo wako unataka kurudi awamu ya tano. Binadamu mna shida sana.
Ukisema utawala wa kijinga unamhusisha Rais wetu mama, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Hawa wote ndio walikuwa watawala wetu awamu ya tano..kwahiyo nakukanya ku generalize Mambo..ukome...kama umechoka kuishi Basi Hana nenda nchi nyingine..hatuwez ona mnatukana viongozi wetu tunanyamaza tu..narudia ukome..kama msumeno wa Sheria haujakufikia
 
Apa dawa tukung'utane wenyewe kwa wenyewe italeta funzo kwa Kila mtawala atakae kuja kuheshimu anaowatawala ataiyo Katiba watu wanayoisema aitakua na mana kwakua asilimia kubwa watu wametawaliwa na mapenzi ya vyama kuliko maslahi mapana ya nchi
Mmeshachoka amani Sasa mnataka kuijaribu Vita jomba....una laana ya mkweo wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…