Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025

Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025

Kwa mtazamo wangu binafsi napendekeza Rais wetu Mama Samia apumzike mwaka 2025 kama analo wazo la kuendelea kutuongoza.

Kwanza niseme wazi Mama ni moja ya Marais bora kabisa kuwai kutokea katika taifa letu. Sijawai kusikia kashifa yeyote ya wizi na ufisadi kutoka kwake, ni Rais mwadilifu kweli kweli.

Ila shida yake ipo kwenye kuchukua hatua juu ya watu wanaomzunguka na kufanya mambo ya hovyo katika utawala wake.

Naunga mkono michakato yote ya kodi inayoanzishwa kufanyika Ila shida ipo kwenye matumizi yake ni jinsi gani tunaitumia hiyo pesa inayopatikana kwenye kodi, mfano serikali kwa ujinga imetumia bilioni 629 kwenye zoezi la sensa pekee huu ni ufisadi.

Zoezi lenyewe watu wengi bado hawajahesabiwa mpaka sasa. Leo ni siku ya 6 ndani ya zile siku saba zilizopangwa maana yake kesho ni siku ya mwisho. Zoezi limegubikwa na wizi na ufisadi wakati zoezi lingewatumia mabalozi wa nyumba kumi tu na mwenyekiti wa kijiji lingekuwa limeshakamilika kwa 100%.

wangetumia karatasi za kawaida kujaza taarifa za watu, then kwenye kata ndio wangeweka mfumo wa TEHAMA wa kuingiza zile taarifa kwa kutumia tablet tungefanikiwa kwa 100%

Kukwama kwa zoezi la katiba na tume huru ya uchaguzi kabla ya 2025, ili nalo ni donda ndugu. Watu wanakushauri kwamba utashindwa uchaguzi 2025 ukileta sasa Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Wanakudanganya ungeweka mazingira sawa ya uchaguzi na katiba lazima watu wangukupigia kura 2025 ili kulipa mema uliyowafanyia hata kama wasingekuchagua mema yako yangeandikwa duniani na mbinguni.

Swala ya mfumuko wa bei ndio bomu kuu, watu hawakatai kwamba vitu vinapanda duniani lakini watu wanachokataa ni kwanini vitu muhimu ndio vipande tu kwani vitu vingine ambavyo havipandi vitu havisafirishwi?

Mfano unakuta kiberiti kinauzwa shilingi 100 Tanzania nzima hakipandi bei zaidi ya miaka 10, wakati na chenyewe kinatumia mafuta kuzalishwa. Ila Ngano, mafuta ya kula na sembe inapanda kila muda kila mwaka.

Utasikia usafirishaji, kwanini mafuta ya alizeti yanayozalishwa Rukwa na Singida hapo hapo kiwandani ukiyafuata yana bei ile ile kama unayoinunua Dar es salaam?

Mh. Rais hapa tukubaliane kwamba umeshindwa ku control inflation kwa sasa, mwezi umepita mafuta yanashuka kila siku kwenye soko la dunia kwanini sisi mafuta yanazidi kupanda tu?

Kwanini uwashughulikii wafanyabiashara Ili waache ulafi wa kutaka faida kubwa?

Tofauti yetu na Zanzibar iko wapi, kwanini Zanzibar kila kitu kinachoingizwa kwenye visiwa hivyo bei zake zipo chini, hata bei zao za mafuta zipo chini kuliko sisi au ndio kusema Zanzibar ni taifa tofauti na sisi?

Basi Kama hivyo Rais Mwinyi ana uwezo wa kupambana na mfumuko wa bei vile, bora tumchukue aje atusaidie huku bara baada ya 2025.

Mambo ni mengi, Ila naomba nikushauri kama unahitaji heshima ya milele basi pumzika 2025 aje mtu mwingine afanye kazi ya Urais. Inawezekana watu wanakushauri vibaya kwa sababu haukuchaguliwa na wananchi ili kukuchonganisha kwa watanzania.
Mama Hana shida ...yupo mpaka 2030 utake usitake!
 
Huyu mama kuna muda nikimtafakari nakoswa majibu , ametupeleka mpaka kwenye hatari yaani ndani ya mwaka mmoja tu kila kitu kinaharibika zaidi ,[emoji22][emoji22]
 
Kuchukua hatua juu ya watu anaowaongoza anaweza, ndio maana aliwaondoa kina Kabudi na Lukuvi.

Tatizo lake kuwachukulia hatua wale vipenzi vyake wa karibu aliowateua yeye ndio anakuwa mgumu kuwachukulia hatua.

Matokeo yake jamaa sasa wanajiamini wanajua hayupo wa kuwafanya chochote kwani ulinzi wanao.

Hii hali ikiendelea, ndio mbele ya safari itaenda kuzalisha mafisadi wa utawala wake, hao "untouchables" wataanza kufanya ujanja na baadhi yao naona wameshaanza.

Hao mafisadi wapya ndio watakuja kuchafua taswira yake siku itakapofika akaondoka madarakani hataacha legacy yoyote, kwa namna alivyoonesha kiu ya kuutaka Urais 2025 sidhani kama ataondoka kabla ya 2030.
Kama magu aluvyokua anawakumbatia kina makonda, na wenzao waleeee...
Kila kiongozi yeyote duniani ana rafiki zake pendwa hata wakosee vipi hawezi watumbua.
 
Kwa mtazamo wangu binafsi napendekeza Rais wetu Mama Samia apumzike mwaka 2025 kama analo wazo la kuendelea kutuongoza.

Kwanza niseme wazi Mama ni moja ya Marais bora kabisa kuwai kutokea katika taifa letu. Sijawai kusikia kashifa yeyote ya wizi na ufisadi kutoka kwake, ni Rais mwadilifu kweli kweli.

Ila shida yake ipo kwenye kuchukua hatua juu ya watu wanaomzunguka na kufanya mambo ya hovyo katika utawala wake.

Naunga mkono michakato yote ya kodi inayoanzishwa kufanyika Ila shida ipo kwenye matumizi yake ni jinsi gani tunaitumia hiyo pesa inayopatikana kwenye kodi, mfano serikali kwa ujinga imetumia bilioni 629 kwenye zoezi la sensa pekee huu ni ufisadi.

Zoezi lenyewe watu wengi bado hawajahesabiwa mpaka sasa. Leo ni siku ya 6 ndani ya zile siku saba zilizopangwa maana yake kesho ni siku ya mwisho. Zoezi limegubikwa na wizi na ufisadi wakati zoezi lingewatumia mabalozi wa nyumba kumi tu na mwenyekiti wa kijiji lingekuwa limeshakamilika kwa 100%.

wangetumia karatasi za kawaida kujaza taarifa za watu, then kwenye kata ndio wangeweka mfumo wa TEHAMA wa kuingiza zile taarifa kwa kutumia tablet tungefanikiwa kwa 100%

Kukwama kwa zoezi la katiba na tume huru ya uchaguzi kabla ya 2025, ili nalo ni donda ndugu. Watu wanakushauri kwamba utashindwa uchaguzi 2025 ukileta sasa Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Wanakudanganya ungeweka mazingira sawa ya uchaguzi na katiba lazima watu wangukupigia kura 2025 ili kulipa mema uliyowafanyia hata kama wasingekuchagua mema yako yangeandikwa duniani na mbinguni.

Swala ya mfumuko wa bei ndio bomu kuu, watu hawakatai kwamba vitu vinapanda duniani lakini watu wanachokataa ni kwanini vitu muhimu ndio vipande tu kwani vitu vingine ambavyo havipandi vitu havisafirishwi?

Mfano unakuta kiberiti kinauzwa shilingi 100 Tanzania nzima hakipandi bei zaidi ya miaka 10, wakati na chenyewe kinatumia mafuta kuzalishwa. Ila Ngano, mafuta ya kula na sembe inapanda kila muda kila mwaka.

Utasikia usafirishaji, kwanini mafuta ya alizeti yanayozalishwa Rukwa na Singida hapo hapo kiwandani ukiyafuata yana bei ile ile kama unayoinunua Dar es salaam?

Mh. Rais hapa tukubaliane kwamba umeshindwa ku control inflation kwa sasa, mwezi umepita mafuta yanashuka kila siku kwenye soko la dunia kwanini sisi mafuta yanazidi kupanda tu?

Kwanini uwashughulikii wafanyabiashara Ili waache ulafi wa kutaka faida kubwa?

Tofauti yetu na Zanzibar iko wapi, kwanini Zanzibar kila kitu kinachoingizwa kwenye visiwa hivyo bei zake zipo chini, hata bei zao za mafuta zipo chini kuliko sisi au ndio kusema Zanzibar ni taifa tofauti na sisi?

Basi Kama hivyo Rais Mwinyi ana uwezo wa kupambana na mfumuko wa bei vile, bora tumchukue aje atusaidie huku bara baada ya 2025.

Mambo ni mengi, Ila naomba nikushauri kama unahitaji heshima ya milele basi pumzika 2025 aje mtu mwingine afanye kazi ya Urais. Inawezekana watu wanakushauri vibaya kwa sababu haukuchaguliwa na wananchi ili kukuchonganisha kwa watanzania.
Hoja yako imefeli kuonyesha hujui sababu ya znz vitu bei rahisi kuliko bara, hujui mambo ya nchi yaendavyo unafata mkumbo tu,
Huna tofauti na walalahoi waliodanganyika na yule mwovu kua kila alifanikiwa ni mwizi na mchawi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Bila tajiri maskini hana maisha....
 
Sheria zinawabana sana wanaokosoa matendo ya serikali kama aliyetumbuliwa juzi tu kisa kuongelea tozo, na kiongoz aliyetamka nchi itapigwa mnada. Ila kwa wezi sheria nchi inasheria ambazo ni ngumu kuzifuata.

NB: Mwezi agosti tuliambiwa kwenye soko la dunia mafuta yalishuka bei na sisi kuambiwa yatashuka mwezi wa 9 maana ya agosti yaliagizwa kipindi bei iko juu. Tunasubiria kuona hiyo septemba
Yatashuka kwa senti ndogo sana kulinganisha na yalivyopanda
 
Nasema kwa kuwa ninaishi na kukutana na watanzania wengi tu huku mtaani kwangu ambako watu wanaimani kubwa Sana na mh Rais wetu na wanaridhishwa na utendaji kazi wake ulio tukuka na wenye kugusa maisha ya watu hasa wanyonge
Huo mtaa unaishi wewe itakua ni kuzimu.
 
Reaction from the ground ya wananchi kuhusiana na huu utawala ni mbaya mno.

Wananchi wanaumizwa mno na hizi tozo.

Na kodi iliyowagusa mno ni ya wapangaji.

Hiyo imekita kwenye mfupa kabisa.

Ni kwakua tu wananchi wanahofia kusema publicly ila akitokea mtu atakayejitoa mhanga kupinga mambo haya hadharani.

Atapata support kubwa sana itayoshangaza wengi.

Serikali iachane na huu utaratibu wa kuleta matozo yasiyokuwa na tija, yanachochea hasira kali mno ndani ya wananchi.

Siku si nyingi tutakuja tafutana hapa na kuanza kulaumiana.
 
Mkuu, umeandika mada nzuri sanaa na pia umetoa mifano halisi.

Naubga mkono mada yako kwa 100%

Maisha yamekuwa magumu mno na mama hana makali kwa watendaji wake hasa huyu Waziri wa TOZO
 
Naunga mkono hoja.

Na sio lazima hio 2025.
Hata 2023 itakuwa vyema
 
Tufanye kazi kaka,kubadilisha uongozi sio kigezo cha wewe kufanikiwa.Mama anafaa na tambua kuwa tuligawanyika mama kaja katuweka pamoja.binafsi namkubali sana ikiwezekana akipewa miaka kumi tutakuwa mbali sana.Hata usimba na uyanga tulionao utaondoka
 
Hakika mawazo kama haya yatazidi kuididimiza Tanzania. Mtu umeshakariri kabisa kuwa kuwa CCM ndiyo wana haki ya kukuletea mtu. Ama! Kwa nini usipiganie haki ya kuchagua kiongozi anayefaa na unakubali kuletewa ''jitu''?
pendekeza Wewe kiongozi yupi unataka achukue nchi tofauti na CCM?
 
Apa dawa tukung'utane wenyewe kwa wenyewe italeta funzo kwa Kila mtawala atakae kuja kuheshimu anaowatawala ataiyo Katiba watu wanayoisema aitakua na mana kwakua asilimia kubwa watu wametawaliwa na mapenzi ya vyama kuliko maslahi mapana ya nchi
 
Ule utawala wa kijinga ulishakuingia damuni. Siku hizi unaishi kwa amani halafu moyo wako unataka kurudi awamu ya tano. Binadamu mna shida sana.
Ukisema utawala wa kijinga unamhusisha Rais wetu mama, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Hawa wote ndio walikuwa watawala wetu awamu ya tano..kwahiyo nakukanya ku generalize Mambo..ukome...kama umechoka kuishi Basi Hana nenda nchi nyingine..hatuwez ona mnatukana viongozi wetu tunanyamaza tu..narudia ukome..kama msumeno wa Sheria haujakufikia
 
Apa dawa tukung'utane wenyewe kwa wenyewe italeta funzo kwa Kila mtawala atakae kuja kuheshimu anaowatawala ataiyo Katiba watu wanayoisema aitakua na mana kwakua asilimia kubwa watu wametawaliwa na mapenzi ya vyama kuliko maslahi mapana ya nchi
Mmeshachoka amani Sasa mnataka kuijaribu Vita jomba....una laana ya mkweo wewe
 
Back
Top Bottom