balimar
JF-Expert Member
- Sep 18, 2015
- 7,743
- 13,657
Salaam!
HALMASHAURI ndio Ofisi pekee zinazotekeleza Sera na Utendaji wa siku kwa siku wa serikali hasa zile za Mitaa. Kiukweli Maafisa Elimu Kata ndio wanayo mawanda mapana sana kwenye kusimamia shughuli za serikali anzia taaluma kwenye kata zao, miradi ya ujenzi wa majengo ya serikali na kuhamasisha Maendeleo huko Katani na uzoefu wa kushawishi wananchi kwenye Maendeleo kitu ambacho ni Adimu sana kwa sasa.
Uzoefu huo adimu sana wanajua namna ya kusimamia hasa miradi, waajiriwa wa serikali (walimu) shule za Msingi na Sekondari na mwisho ni ule uzoefu walionao kukaa hata maeneo ya vijijini kabisa ambapo Maafisa wengine hawawezi. Hawa ni field officers kweli kweli.
Tatizo la kuwa Maafisa Elimu Kata ni kukosekana kwa Magodfather (tabia inayoota mizizi nchi hii) na watu wa kuwasemeasemea. Lakini kama Madam SSH atapitia uzi huu, hakika hutojuta kuwachagua maafisa hawa kwani wana uwezo mkubwa na wana nidhamu sana za kiutumishi. Kwahiyo kazi ni yake kuwaibua ili wamsaidie kazi na hatimae HALMASHAURI zipae kimaendeleo.
Hivyo, Ofisi za teuzi zikiwa makini Maafisa Elimu Kata ni 'recruiting post' kwa nafasi yoyote ya DED au DAS kwenye ngazi ya halmashauri.
Kila la kheri Madam SSH!