Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,992
- 22,396
Hii ni kauli sahihi na ndio ukweli wenyewe.Huo ndio uhalisia wa mambo.
Tusiendeshwe na mihemko. Kila jambo lina uhalisia wake. Hutaki wacha!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ni kauli sahihi na ndio ukweli wenyewe.Huo ndio uhalisia wa mambo.
😀😀😀😀😀😀😀Usichokijua ni kwamba wananchi wakiamua, wana uwezo wa kpiga pini Rais na Serikali yake. Kila upande ni muhimu kwaajili ya mstakabali wa Taifa.
Serikali ina polisi, mabomu na bunduki, wapinzani wana akili ja weledi.
Magufuli alikuwa na vyote bavyo Samia anavyo lakini mapambano yake na vyama vya upinzani, aliangukia pua. Angekuwa hai, siku moja kama angehojiwa angeeleza wazi jinsi CHADEMA ilivyomwendesha. Serikali ya Magufuli ilifikia hatua mpaka ya kwenda kukopa kwenye mabenki ya biashara baada ya kuishiwa mbinu zote.
Wajinga walimwona Magufuli ni mwamba lakini Magufuli alibanwa mbavu kila sehemu. Hakuna alichopanga kilichofanikiwa. Utekelezaji wa bajeti ukawa unacheza kati ya 35 na 40%. Akabakia kutawala akiwa na frustration.
Baada ya kushindwa mbinu zote, akaamua kutumia njia ovu kutawala. Baadaye akaamua kujishughulisha na vitu vidogo vidogo maana vikubwa ikawa ngumu kuvimaliza. Pesa kidogo aliyokusanya na kupora watu, akaamua kuitumia kwenye miradi midogo midogo kama vile visima vya maji, vipande vya barabara za mijini, ujenzi wa masoko na stand, huku miradi mikubwa akisubiria mikopo.
Rais Samia, nia yake njema ya kufufua uchumi itakuwa ngumu sana kutekelezeka, akishindwa kuvifanya vyama vya upinzani kuungana naye kwenye ajenda za kitaifa.
Katiba mpya haiwezi kuja pasipo kuwa na maelewano baina ya pande mbili, hivyo basi chama tawala na vyama pinzani vikae vielewane kila kitu kitakuwa sawa. Nawasalimu kwa jamuhuri ya muungano.Facts
- Ni wazi kuwa wapinzani (wa kweli), wanaharakati, CCM Zanzibar, CCM wapenda mabadiliko bara na watanzania wengi kwa ujumla wao wanataka mabadiliko ya katiba ili kuondoa changamoto nyingi za kisheria na kiutawala zilizopo sasa.
- Ni wazi kuwa wazanzibari wengi (Mh. Rais akiwemo) wanatamani mabadiliko ya katiba ili kujaribu kutafuta ufumbuzi wa zinazoitwa kero za muungano.
- Ni wazi kabisa kuwa Rais Samia hawezi kuanzisha mchakato wa katiba mpya katika ungwe yake ya kwanza, itakuwa ni political suicide. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kufufua mchakato akiwa katika ungwe yake ya mwisho (inshaallah).
- Ni wazi kuwa wapinzani wa kweli wamedhamiria kutoshiriki uchaguzi wowote nchini ambao utakua chini ya tume hii ya taifa ya uchaguzi (ya uchafuzi). Vilevile hawatoshiriki uchaguzi utakao simamiwa na ule mfumo kichekesho wa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa kupitia waziri wa TAMISEMI. Jambo hili ni doa na hatari kwa ustawi wa nchi.
Ushauri
Lazima mchakato wa mabadiliko ya katiba uanzie mahali fulani, hivyo basi Mheshimiwa Rais nakuomba kwa unyenyekevu ukutane na wadau wote kwenye swala hili ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa (hususani CDM), kisha mkubaliane kwa kuanza na marekebisho ya sheria ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuirekebisha tume ya uchaguzi.
Hii itawezesha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2025 kufanyika kwa uhalali machoni pa watanzania na jumuiya za kimataifa na vyama vyote vitaweza kushiriki. (Wewe Mheshimiwa sana utashinda ili uongoze kwa awamu ya pili).
Pia, CDM na wapinzani wengine watashinda viti vya kutosha bungeni na kwenye udiwani. Mheshimiwa Rais, utawahitaji sana watu hawa pindi utakapo fufua mchakato wa katiba mpya.
Hata wewe mwenyewe Mheshimiwa sana ukweli unaujua, upinzani wa mabadiliko ya katiba unaletwa na wana CCM wahafidhina kutoka Tanzania bara. Hivyo basi support ya vyama vya upinzani ni muhimu sana pamoja na ile ya wale CCM 'moderates' wa bara na CCM Zanzibar.
Kwenye hili lazima pande zote zikubali ku 'compromise' ili tupate pa kuanzia.
You Chadema guys are very low kwa kweli.Lazima akimbie
Kumbe na wewe hueleweki unaongea kishabiki.Haizuiliki, ni ajenda ya wananchi. Mheshimiwa rais awe makini na akubali maelewano, vyama vya upinzani wamempa mkono wa heri kwa kuomba kukutana naye lakini amejikausha mpaka sasa.
Wanasema ni agenda ya wananchi, hahahaahahah wananchi wapi?? Hawa si wamekataliwa nchi nzima juzi tu kwenye sanduku la kura? Hata mbunge mmoja hawajapata hahahahahaahNdio mpaka wananchi waamue sasa,CDM mumekataliwa na wananchi sasa mnajifanya kuwasemea,waliwatuma lini?
Kazi iendelee......Katiba mpya haiwezi kuja pasipo kuwa na maelewano baina ya pande mbili, hivyo basi chama tawala na vyama pinzani vikae vielewane kila kitu kitakuwa sawa. Nawasalimu kwa jamuhuri ya muungano.
Wanakwambia ni haki ya wananchi kudai katiba 😅 na ipo kisheria ila wao wanakosa lugha ya staha tu wanataka kutukana na kushurutisha mamlakaHapana. Hawa watu ni mafedhuli wasio na staha wala busara.
Mheshimiwa rais aliwaambia vizuri tu kwamba wasubiri hiyo issue ataishughulikia. Kisa cha kuanza kumporomoshea matusi ni nini? Wengine ndio wamo humu humu JF kazi yao kutukana tu.
Watu tunaowategemea kama wapinzani wanakaa na kutoa kauli za ajabu ajabu kwa rais. Hii haikubaliki, hamjifunzi??? How do you really want to be treated you guys??
Anyway, walisema watamlazimisha atake asitake. Sasa ok, kila mtu na ashinde mechi zake!
Impitie: Extrovert
Jumbe Brown
Na waendelee Sisi tupo tunaangalia.Wanakwambia ni haki ya wananchi kudai katiba 😅 na ipo kisheria ila wao wanakosa lugha ya staha tu wanataka kutukana na kushurutisha mamlaka
Eeh si kafiwa na kaka yake so ana msiba kwanzaNa waendelee Sisi tupo tunaangalia.
Naskia Mbowe anashauri mikutano ya katiba mpya yote isitishwe.
Nachokisema ni muhimu kwa rais kukutana na wapinzani, sisemi kuwa ni lazima katiba upatikane ndani ya awamu hii.Kumbe na wewe hueleweki unaongea kishabiki.
Kwenye bandiko kuu unasema ngwe hii ya kwanza katiba kupatikana ni ngumu halafu kwenye post hii unasema haizuiliki.
Unafuata tu mkumbo kama NYUMBU sio??
AbsolutelyKatiba mpya haiwezi kuja pasipo kuwa na maelewano baina ya pande mbili, hivyo basi chama tawala na vyama pinzani vikae vielewane kila kitu kitakuwa sawa. Nawasalimu kwa jamuhuri ya muungano.
Lakini bila kupepesa macho huo ndio ukweli, ACT ilianzishwa kama CCM B, na NCCR mageuzi ilianzishwa na TISS. CUF iliyokuwa moto nayo tayari ilishaingiliwa na CCM na kufa rasmi.Kazi iendelee......
Mkuu unajua kwamba hapa nchini CDM ndio wanajiona wao ndio "Vyama pinzani "???
Yaani kwao wao NCCR na ACT na CHAUMA wote ni CCM??
Kwani rais si amesema atakutana nao!!! Au mnachotaka ni lazima iwe ndani ya wakati mliopanga nyinyi??Nachokisema ni muhimu kwa rais kukutana na wapinzani, sisemi kuwa ni lazima katiba upatikane ndani ya awamu hii.
Hii ya kuwapuuza ndiyo inawafanya waanze kuwa na mashaka na matokeo yake inaleta vita majukwaani.
Wanaweza kukutana na kuelezana kwa uwazi na ukweli kuwa mchakato utaanza baada ya uchaguzi 2025, na pia walau Mh. Rais akakubali kuifanyia maboresho sheria ya uchaguzi.
Hiyo ni kwa mujibu wa wewe. Tukimuuliza Ado Shaibu au Abdul Nondo au ACT Wazalendo Watapinga haya unayoyazungumzia and they will be right as well.Lakini bila kupepesa macho huo ndio ukweli, ACT ilianzishwa kama CCM B, na NCCR mageuzi ilianzishwa na TISS. CUF iliyokuwa moto nayo tayari ilishaingiliwa na CCM na kufa rasmi.
Hapo kwenye lugha za maudhi wengi wamewashauri waache lakini naona ndio utamaduni wa CDM.Kwani rais si amesema atakutana nao!!! Au mnachotaka ni lazima iwe ndani ya wakati mliopanga nyinyi??
Halafu, rais akikutana na NCCR ACT na CHAUMA na CDM wote kwa pamoja si itatosha?? Maana kukutana na mmoja mmoja inaweza kuwa ngumu kwa sababu ya ratiba za rais, protokali na mambo ya COVID-19.
Halafu ni kipi kinachokwambia kwamba amewapuuza??? Si unajua kwamba mama hajafikisha hata miezi minne madarakani??
Halafu pia inaonekana hata akikutana na Chadema hakuna kitakachokuwa na wala asipoteze her valuable time maana Chadema wanam-regard mama kama Magufuli wa kike. Wewe unaonaje mkuu???
Na hizo hoja nyengine kwenye post hiyohiyo mbona umeziruka ndugu??Hapo kwenye lugha za maudhi wengi wamewashauri waache lakini naona ndio utamaduni wa CDM.
Hata mimi sipendezwi na baadhi ya kauli za CDM.
Wananchi kwa sasa wanahitaji stable income,huduma za afya,maji,umeme,barabara na elimu za uhakika ndio hayo mengine yatafuata wakishashiba.Wanasema ni agenda ya wananchi, hahahaahahah wananchi wapi?? Hawa si wamekataliwa nchi nzima juzi tu kwenye sanduku la kura? Hata mbunge mmoja hawajapata hahahahahaah
Wanasahau Tzn sio Marekani wala Kenya kila nchi inautamaduni wake wa kutafsiri uhuru kwa mujibu wa sheria,utamaduni na mazingira.Hapana. Hawa watu ni mafedhuli wasio na staha wala busara.
Mheshimiwa rais aliwaambia vizuri tu kwamba wasubiri hiyo issue ataishughulikia. Kisa cha kuanza kumporomoshea matusi ni nini? Wengine ndio wamo humu humu JF kazi yao kutukana tu.
Watu tunaowategemea kama wapinzani wanakaa na kutoa kauli za ajabu ajabu kwa rais. Hii haikubaliki, hamjifunzi??? How do you really want to be treated you guys??
Anyway, walisema watamlazimisha atake asitake. Sasa ok, kila mtu na ashinde mechi zake!
Impitie: Extrovert
Jumbe Brown