Ushauri: Roho inaniuma, nimezaa na mwanamke nisiyempenda. Bado anataka kuishi na mimi

Ushauri: Roho inaniuma, nimezaa na mwanamke nisiyempenda. Bado anataka kuishi na mimi

Aisee!

Maisha ya mtoto inaonekana kabisa huna habari!

Katika maisha tunafanya sacrifice kwa sababu ya watoto ndio family.

Achana na wewe kufurahia mahusiano ila hakikisha unarudiana na huyo mwanamke ili mtoto afurahie family (wazazi wake).

Acha upumbafu boss wangu wa kuwa selfish kiasi hicho cha kujifikiria wewe tu.

Kila la kheri mkuu ila hakikisha unarudiana na huyo mwanamke.

Huyo mwanao wa kike unataka akuzwe na nani kama si baba na mama wote kwa pamoja.
 
Mkuu mimi pia niko na situation kama yako ila uanaume ni majukumu tu,mambo ya kupenda achia wanawake angalia maisha yako ya baadae na mwanao anahitaji malezi ya baba na mama.

Kama mwanamke ana kuheshimu na kusikiliza maagizo yako na yuko matured inatosha kuweka ndani.Hao wenye sifa uzitakazo ndo watakuwa mchepuko wako full stop! Mimi huyu babymama naoa tu
Kunywa soda
 
Heheheh na hapo ndipo karma itakapomshughulikia [emoji23][emoji23][emoji23] unless awe hana mvuto kabisa ila mwanamke atakayenipenda nikajua ananipenda haswa sintomuacha. Soko la wanawake limejaa matapeli sana ukipata mwanamke real kwako namna hio aheri utulie tu kabla hujaangukiwa kwa jambazi la kike. Ndicho kitakachofuata, jamaa atapata mwanamke atampenda ila atafanyiwa vimbwanga hadi akome.
Sure kabisa

Mwanamke akikupenda komaa hapo hapo

Kuna matapeli na wadangaji siku hizi
 
Sikia broo, mimi ni Malaya na kitombi haswa Hawa wanawake nimekaa nao Sana Kama uhuni nishafanya Sana ila kitu nilichojifunza ni mpende akupendae hata usipompenda utajifunza taratibu "time heals , time is a good teacher " nikwambie umezingua Sana umeyumba

Siku zote huwezi pata unachokitaka ila upatacho sometimes kinakuja kuwa bora kuliko ulivyotarajia



Kunguru mwana wa manzese
Afadhali baharia umemwambia [emoji1]
 
Baada ya biashara kuenda vizuri kamtosa anataka slay queen

Ngoja biashara ianze kwenda mrama[emoji1787]
 
Heheheh na hapo ndipo karma itakapomshughulikia 😂😂😂 unless awe hana mvuto kabisa ila mwanamke atakayenipenda nikajua ananipenda haswa sintomuacha. Soko la wanawake limejaa matapeli sana ukipata mwanamke real kwako namna hio aheri utulie tu kabla hujaangukiwa kwa jambazi la kike. Ndicho kitakachofuata, jamaa atapata mwanamke atampenda ila atafanyiwa vimbwanga hadi akome.
Mbona mi nakupenda na wewe ndo hunielewi hata kidogo 😢😢
 
Sijasoma story yako Ila nakuuliza tu,mwanamme mwenzangu,unajua kabisa humpendi,halafu unaingiza dyudyu Tena bila ya jezi,then unajojoa humo humo,unasema humpendi,ungetumia zana baharia[emoji38][emoji38]
 
Habari wadau! Katika mihangaiko ya hapa na pale kuna binti nilimkuta mahali, kifupi nikamtamani na nikataka nipite tu.

Baada ya mbinu za hapa na pale, alinipa namba na tukajikuta penzini, baada ya mawasiliano ya kama wiki, nilimwambia aje home.. nilitaka kula mzigo akabana na mimi kulazimisha huwa siwezi na ukizingatia sikumuelewa kabisa ikabidi nimpotezee mazima.

Yule binti baada ya hapo hakukata tamaa aliendelea kunitafuta mara kwa mara, kila mara alikuwa akianza yeye, pamoja na kumchunia kote hakukata tamaa na kipindi hicho alikuwa hayupo tena mkoa niliokuwepo!

Muda ulienda ikapita kama miaka miwili, mimi juhudi zangu za kupata mwenzi zikawa zinagonga mwamba, kuna wakati uchumi wangu uliyumba sana na kwa vyovyote nilikuwa nahitaji mtu wa kusimamia shughuli zangu ili mimi nipambane kivingine.

Huyu binti nilimpanga nianze kuishi naye akakubali, hapo kiukweli moyo haukuwepo kabisa kwake, kilichonivuta kwake ni ule uvumilivu na kutoomba hela kabisa. Nikajipa moyo pengine nitampenda nikianza kuishi naye.

Baada ya kama miezi mitatu, alipata ujauzito na mimi mambo yangu angalau yakaanza kwenda mbele. Hapo kuna mwanamke wangu ambaye alikuwa bado A level nilikuwa nachatt naye bado. Kuna siku alikuta sms, akatishia kuondoka akafunga mpaka mabegi, nikaona isiwe kesi nikaomba msamaha nikaita mpaka mtu akaniombea msamaha maisha yakaendelea.

Wakuu kuishi na mtu usie na hisia naye ni kazi sana, nikawa naona yote nafanya kumfurahisha yeye tu, kweli ananipenda sawa lakini kwangu je? Nitajidanganya mpaka lini, nikawa nawaza sana hivi huyu kweli ndo wa kufa na kuzikana? Kifupi sikuwahi kuwa proud na yeye hata siku moja, mapenzi yakageuka mateso bila chuki, hakuna kitu kigumu kama unalala na kuamka na mtu ambaye humpendi na wala huna hisia naye

Miezi ilienda mimba ikawa kubwa ikabidi arudi kwao kujifungua, hapo kwao hawanifahamu zaidi ya kuwasiliana na dada ake. Miezi ilienda akajifungua mtoto wa kike, copy yangu kabisa..furaha yake ilikuwa kubwa ila mimi kwangu ilikuwa tofauti nikawa nawaza sana hatma yetu.

Ilipita miezi kadhaa nikawafuata wakarudi nyumbani, hapo furaha sina najilazimisha tu. Mwanamke naye akaanza visirani vya hapa na pale, tatizo dogo mara atishie kurudi kwao, mara naenda lini kujitambulisha (moyoni nikawa najisemea huyu angejua).

Basi kuna siku katika pita pita huko mtaani kuna binti nikapata namba yake nikaanza kumtongoza kwa kutumia kisimu kidogo, sms inbox nikawa nafuta dah kumbe nilisahau kusett sent item zijifute, basi kwenye pekua pekua yake akakuta zile sms, akalia sana mara mimi nataka kumuua sijui mtoto mdogo n maneno mengine mengi sana.(kifupi toka nimekuwa naye sikuwahi chepuka kabisa). Basi baada ya hapo minuno ikaanza, nikijaribu kujirudi anakaza, nikasema poa isiwe shida.

Siku moja niliamka asubuh, sikumsemesha kitu akaweka maji bafuni sikuoga wala chai aliyoandaa sikunywa nikaondoka zangu, baadaye akatuma sms kwa haya maisha yamemchosha nikamwambia sawa, akataka nauli na mtaji. Nikamwambia mm nina nauli tu, akasema bila mtaji haondoki nikamwambia nauli hiyo hapo, ukiondoka sawa usipoondoka sawa ni wewe.

Kweli akakusanya mazaga yake, asubuh nikawapeleka ubt, wakaondoka. Niseme tu ukweli siku hiyo nilijihisi kutua mzigo mzito sana, nafsi ikawa nyeupe sana, japo nilijua nilimkosea na kumpotezea muda lakini ningefanyeje.

Sasa baada ya kuondoka haikupita hata wiki akaanza kuomba kurudi na kuomba msamaha sana. Kiukweli mimi sikuwa tayari, niligoma na sasa ni mwaka umepita tangu aondoke, kifupi bado sijapata mwanamke wa kueleweka atakayetuliza moyo wangu, kwenye hili wala sina haraka najipa moyo nitampata tu hata kama nitatumia miaka kumpata.

Sasa changamoto inakuja huyu mama wa mtoto wangu, bado hajakata tamaa mpka leo anaamini atarudi kwangu, kumwambia ukweli kwamba simpendi naona itamuumiza sana na hii sioni kama ni option nzuri.

Kwa wazoefu wa mambo, nitumie njia gani kumfanya huyu mwanamke aendelee na maisha yake, najua anadeserve furaha na kupendwa, but kwangu hivyo havipo na kamwe hatakuja kuvipata. Je nitumie njia gani kumuweka ajue kwamba hana nafasi kwenye maisha yangu.

Marriage nyingi ni inconvenience kibongo bongo huyo ndiyo Mke wako

Kaza jombaa usikate tamaa
 
Heheheh na hapo ndipo karma itakapomshughulikia 😂😂😂 unless awe hana mvuto kabisa ila mwanamke atakayenipenda nikajua ananipenda haswa sintomuacha. Soko la wanawake limejaa matapeli sana ukipata mwanamke real kwako namna hio aheri utulie tu kabla hujaangukiwa kwa jambazi la kike. Ndicho kitakachofuata, jamaa atapata mwanamke atampenda ila atafanyiwa vimbwanga hadi akome.
Legendary!

Mwanaume "ubarikiwe" kupata mke anayekutii. Utajisikia kama Amiri Jeshi unayeamrisha Jeshi kubwa lenye nguvu kushinda kila vita. Kinyume chache jiandae kushindwa na mapambano ya Maisha. Bila mke anayekupenda na kukutii ujue kabisa hutoboiiii.
 
Legendary!

Mwanaume "ubarikiwe" kupata mke anayekutii. Utajisikia kama Amiri Jeshi unayeamrisha Jeshi kubwa lenye nguvu kushinda kila vita. Kinyume chache jiandae kushindwa na mapambano ya Maisha. Bila mke anayekupenda na kukutii ujue kabisa hutoboiiii.
Haipingwi hii, 100% truth!
 
Back
Top Bottom