Ushauri: Roho inaniuma, nimezaa na mwanamke nisiyempenda. Bado anataka kuishi na mimi

Ushauri: Roho inaniuma, nimezaa na mwanamke nisiyempenda. Bado anataka kuishi na mimi

Kuwa makini sana na chaguzi sasa, na ni kipi ndiyo kigezo chako pindi unachagua.... Kuna vitu vingine sio muhimu sana kuweka kama kigezo namba moja hasa urembo sawa wenge mtakataa ila likija swala la ndoa mimi nitaweka heshima,upendo, hofu ya mungu na awe mwenye kujitambua ila uzuri wa kiasi sio mbaya hasa kwa lengo la kuingia kwenye ndoa, ndoa ni taasisi inahitajai watu makini sana kuyaishi maisha ya ndoa kuliko hata huo uzuri
Sure Thing..
 
Kiufupi ishu yako iko hivi;

Bora mara mia ukaishi na huyo mwanamke anayekupenda coz huko mbele utakayempata utakuwa we unampenda yeye hakupendi hata kidogo, mbona utadataa[emoji1]




[emoji848][emoji848]
 
Kwanza pole kwa kusema kuwa ilibidi uendelee kuish nae labda utampenda, na haikuwa hivyo..
Pili: ulikosea kuish nae chin ya paa moja huku ukijua huna hisia nae.

Mi nakushauri mambo yafuatayo:-
(1) Muhudumie Mtoto hadi aje kujitegemea (huyu hana makosa , usije mtesa mja wa mwenyez Mungu)
(2) Mwombe msamaha mzaz mwenzako kuwa ulimkosea
(3) Tafuta mwengne unayezani utampenda ila uwe makini kuhakikisha unampata mtakayependana wote kwa pamoja na sio vinginevyo (ikitokea tofauti yaan upendo ukawa wa upande mmoja baina yenuxbasi hesabu maumivu MAKUBWA SANAA na hapa ndipo utakapokuja kuwakumbuka watoa michango hapa jf wanavokukanya)

N.B
Hakuna kitu kibaya kitakachokuja kukuumiza na Kuja KUJUTIA Maisha yako yoote kama kuja kumpenda mwanamke asiyekupenda..hapa UTAZIONA RANGI ZOOTE Duniani..
 
Habari wadau! Katika mihangaiko ya hapa na pale kuna binti nilimkuta mahali, kifupi nikamtamani na nikataka nipite tu.

Baada ya mbinu za hapa na pale, alinipa namba na tukajikuta penzini, baada ya mawasiliano ya kama wiki, nilimwambia aje home.. nilitaka kula mzigo akabana na mimi kulazimisha huwa siwezi na ukizingatia sikumuelewa kabisa ikabidi nimpotezee mazima.

Yule binti baada ya hapo hakukata tamaa aliendelea kunitafuta mara kwa mara, kila mara alikuwa akianza yeye, pamoja na kumchunia kote hakukata tamaa na kipindi hicho alikuwa hayupo tena mkoa niliokuwepo!

Muda ulienda ikapita kama miaka miwili, mimi juhudi zangu za kupata mwenzi zikawa zinagonga mwamba, kuna wakati uchumi wangu uliyumba sana na kwa vyovyote nilikuwa nahitaji mtu wa kusimamia shughuli zangu ili mimi nipambane kivingine.

Huyu binti nilimpanga nianze kuishi naye akakubali, hapo kiukweli moyo haukuwepo kabisa kwake, kilichonivuta kwake ni ule uvumilivu na kutoomba hela kabisa. Nikajipa moyo pengine nitampenda nikianza kuishi naye.

Baada ya kama miezi mitatu, alipata ujauzito na mimi mambo yangu angalau yakaanza kwenda mbele. Hapo kuna mwanamke wangu ambaye alikuwa bado A level nilikuwa nachatt naye bado. Kuna siku alikuta sms, akatishia kuondoka akafunga mpaka mabegi, nikaona isiwe kesi nikaomba msamaha nikaita mpaka mtu akaniombea msamaha maisha yakaendelea.

Wakuu kuishi na mtu usie na hisia naye ni kazi sana, nikawa naona yote nafanya kumfurahisha yeye tu, kweli ananipenda sawa lakini kwangu je? Nitajidanganya mpaka lini, nikawa nawaza sana hivi huyu kweli ndo wa kufa na kuzikana? Kifupi sikuwahi kuwa proud na yeye hata siku moja, mapenzi yakageuka mateso bila chuki, hakuna kitu kigumu kama unalala na kuamka na mtu ambaye humpendi na wala huna hisia naye

Miezi ilienda mimba ikawa kubwa ikabidi arudi kwao kujifungua, hapo kwao hawanifahamu zaidi ya kuwasiliana na dada ake. Miezi ilienda akajifungua mtoto wa kike, copy yangu kabisa..furaha yake ilikuwa kubwa ila mimi kwangu ilikuwa tofauti nikawa nawaza sana hatma yetu.

Ilipita miezi kadhaa nikawafuata wakarudi nyumbani, hapo furaha sina najilazimisha tu. Mwanamke naye akaanza visirani vya hapa na pale, tatizo dogo mara atishie kurudi kwao, mara naenda lini kujitambulisha (moyoni nikawa najisemea huyu angejua).

Basi kuna siku katika pita pita huko mtaani kuna binti nikapata namba yake nikaanza kumtongoza kwa kutumia kisimu kidogo, sms inbox nikawa nafuta dah kumbe nilisahau kusett sent item zijifute, basi kwenye pekua pekua yake akakuta zile sms, akalia sana mara mimi nataka kumuua sijui mtoto mdogo n maneno mengine mengi sana.(kifupi toka nimekuwa naye sikuwahi chepuka kabisa). Basi baada ya hapo minuno ikaanza, nikijaribu kujirudi anakaza, nikasema poa isiwe shida.

Siku moja niliamka asubuh, sikumsemesha kitu akaweka maji bafuni sikuoga wala chai aliyoandaa sikunywa nikaondoka zangu, baadaye akatuma sms kwa haya maisha yamemchosha nikamwambia sawa, akataka nauli na mtaji. Nikamwambia mm nina nauli tu, akasema bila mtaji haondoki nikamwambia nauli hiyo hapo, ukiondoka sawa usipoondoka sawa ni wewe.

Kweli akakusanya mazaga yake, asubuh nikawapeleka ubt, wakaondoka. Niseme tu ukweli siku hiyo nilijihisi kutua mzigo mzito sana, nafsi ikawa nyeupe sana, japo nilijua nilimkosea na kumpotezea muda lakini ningefanyeje.

Sasa baada ya kuondoka haikupita hata wiki akaanza kuomba kurudi na kuomba msamaha sana. Kiukweli mimi sikuwa tayari, niligoma na sasa ni mwaka umepita tangu aondoke, kifupi bado sijapata mwanamke wa kueleweka atakayetuliza moyo wangu, kwenye hili wala sina haraka najipa moyo nitampata tu hata kama nitatumia miaka kumpata.

Sasa changamoto inakuja huyu mama wa mtoto wangu, bado hajakata tamaa mpka leo anaamini atarudi kwangu, kumwambia ukweli kwamba simpendi naona itamuumiza sana na hii sioni kama ni option nzuri.

Kwa wazoefu wa mambo, nitumie njia gani kumfanya huyu mwanamke aendelee na maisha yake, najua anadeserve furaha na kupendwa, but kwangu hivyo havipo na kamwe hatakuja kuvipata. Je nitumie njia gani kumuweka ajue kwamba hana nafasi kwenye maisha yangu.
wewe hujielewi.Kama humtaki mwambie ila usilete habari za ooh sina hisia naye.Mimi nachokiona ni kwamba kuna kitu unakitafuta na utakipata.
 
Nimesoma comment zote so far zilizotolewa
Zaidi ya asilimia 90% wanashauri kuwa usifanye hivyo kwani karma itakuja kukuwajibisha. Ni wachache wenye mtazamo kinzani na huo kuwa usiogope kutafuta kile unachokipenda coz sio afya either kuishi kwa kuogopa kuonekana mbaya.

Kundi la kwanza mbali na kusisitiza uwajibikaji ila hoja yao imejengeka kihisia ya hofu, kuwa bila shaka utalipia na utateseka pia. Swali ni kuwa mbona hata sasa unavyoishi nae pia unateseka na hauna furaha???

Maisha siku zote ni kuchagua. Hakuna maisha yaliyokamilika ila ni vizuri kuchagua yale yanayokupa amani na kijisikia vizuri. Maisha yana maudhi sana hivyo ni busara kujaribu kuyaishi katika mazingira yenye shock absorber and stress relief.

Sina uzoefu mkubwa na maisha haya ila naamini always kuna fursa ya kuchagua vyema Kama unahisi umekosea. Kuanza upya sio ujinga wala udhaifu ila ni kuwa na mtazamo chanya wa kuwa you deserve the best.

Daima Kuna changamoto kupata ushauri wa mambo ya mahusiano hasa kunapokua na msingi wa kihisia ndani yake Kama hilo la kutojulikana hatima ya mtoto, na bahati mbaya hujaeleza unavyowajibika au una mipango ipi umeiweka juu ya future ya mwanao.

Ni vizuri kuwa mwajibikaji. Sifa hii ndo inafanya watu ku surcrifice maisha na ku compromise a lot ili tu kubalance mambo . Ndoa nyingi Kama sio zote wanandoa sio kuwa wanafurahia Sana na kulizika bali kinachowaweka pamoja ni hiyo sense ya uwajibikaji.

Hivyo bro ni wakati wako wa kufanya maamuzi. Zingatia mantiki na uhalisia wa mambo na sio hofu pale unapotaka kufanya maamuzi. Zaidi Sana zingatia ndoto zako na maono ya maisha yako. Tunaishi mara moja huna sababu ya kuishi maisha yako kwa huzuni na majuto.
This is pureman2...
 
Lets hope ataelewa mkuu. Haya mambo tumetapitia. Mtu anakwambia kbs sijawahi kukupenda i was just having fun. Haya machozi huwa ni mabaya sana asikwambie mtu. Wala sikumshtakia mtu kwa Mungu. Umashangaa tu unaombwa misamaha ya kutosha ili mambo yake yaachiliwe Mungu anamuadhibu sana. Kuna watu wana dharau nyie acheni tu. Mpaka leo wanahangaila na dunia tu
Pole mpendwa.
 
Mkuu mimi pia niko na situation kama yako ila uanaume ni majukumu tu,mambo ya kupenda achia wanawake angalia maisha yako ya baadae na mwanao anahitaji malezi ya baba na mama.

Kama mwanamke ana kuheshimu na kusikiliza maagizo yako na yuko matured inatosha kuweka ndani.Hao wenye sifa uzitakazo ndo watakuwa mchepuko wako full stop! Mimi huyu babymama naoa tu
 
Watu wa hivi uwakute kwenye threads za
"SITAKUJA KUOA MWANAMKE ASIYE NA BIKRA"
au
" USIOE SINGLE MOTHER"

mxxxxxxxxxiiiiiièeee
Yaani achaaa kbs. Halaf yet utakuta majority wako raised na single mothers. Hawa single mothers majority siyo by choice. Wamejawa na upweke sana kwa mambo kama haya. Utakuta baadaye anasakamwa sana maskini. Binadamu hatuna huruma sisi. Tuwahurumie gawa wamama jamani. Kwanza nawapenda sana. Watoto wap wanapendezaga sana. Wanapambana mno. Later unaskia mtu anataka mtoto wake ameshazeeka
 
Rudia tena kusoma huo mstari vizuri.
Utakuja kupata ambaye atarudisha mambo yako nyuma.
IMG_20201226_085038_396.jpg
 
Back
Top Bottom