Ushauri: Roho inaniuma, nimezaa na mwanamke nisiyempenda. Bado anataka kuishi na mimi

Pointi mkuuu mwambie uyo ,wanawake wa sasa sanaa tupu
 
Yatakurudia mateso anayopitia mwenzii sa iv mrudie na umlee mtoto wenu ao ndio ndugu zako wa ukweli...mwanamke aliekaa na ww kwny dhiki zako zte na akakuvumilia cha zaidi akakuzalia uyo ndo mkeo ...usifanye uharibifu kwny maisha ya uyo dada mpende na umpendezeshe uone utampenda ka ao wa nje
 
Hata sasa napata mateso makubwa, sasa ni mateso gani zaidi ya haya ambayo naweza kuyapata?
 

Suala la kutompenda halina shida ila sio poa kumtukana kimaumbile etu ‘’ Kifupi’’
 
Suala la kutompenda halina shida ila sio poa kumtukana kimaumbile etu ‘’ Kifupi’’
kabla ya kumgegeda hauwezi ona mapungufu ya kimaumbile
jiulize mara ya kwanza alitamani nn au ni nyenge silizidi
 
Nakushauri yafuatayo.
1.Mtunze mtoto wako na hakikisha anakaa vizuri, mpatie mahitaji na mkatie bima ya afya ili usisumbuliwa kila wakati anapoumwa.

2. Tumia akili unapotafuta mke, usitumie hisia na moyo. Ukitumia hisia ukaoa baadaye ukiwa naye ukiona upungufu ndipo akili yako itafanya kazi utajua kuwa ulikosea. Na hilo ndilo lililokutokea ukampa mtoto wa watu mimba maana ulimtamani na ukafanya nae ngono zembe ili hali akili yako ilimkataa.

3. Acha tamaa ya kutaka penzi la haraka itakuharibia maisha yako inaelekea unapenda sana mashepu mkuu,, hahaha nakutania mkuu.
 
Roho mbaya, kutokujali hisia za mwenzio na ubinafsi vimekujaa mkuu. Unaweza vipi kumuita mtu usiempenda muishi pamoja kwa manufaa yako kibiashara.

Hukufanya vyema mkuu ungemkataa toka mwanzo tu, ushampa usingle maza na si ajabu wewe ni mmoja kati ya wanaopa kwa miungu wote kua hawawezi kuoa single maza.
 
Ila wanaume kama humpendi mtu kwanini umtongoze kwanini uamshe hisia za mapenzi kwenye moyo wake then baadae unamuacha ateseke it's very sad acheni kuplay na hisia za watu jamani
 
Kijana kumbuka misemo ya wahenga, mpende akupendae, ipo siku utakuja kumkumbuka, wakuu humu wana msemo wao kuwa husipende kutumia kichwa cha chini kwenye maamuzi yako tumia kichwa cha juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…