Ushauri: Samia asipogombea CCM itapata hasara kubwa haijawahi kutokea tangu kiundwe

Ushauri: Samia asipogombea CCM itapata hasara kubwa haijawahi kutokea tangu kiundwe

Fanfa

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2009
Posts
2,399
Reaction score
3,775
Chama cha mapinduzi (CCM) kitapata hasara kubwa sana kama Samia hatagombea Urais kwa sababu zifuatazo;

1. CCM imewekeza kwenye matangazo nchi zima kwa takribani miaka minne sasa kumtangaza Samia. Bill Boards kila kona ya nchi zimejaa. Barabara zimejaa matangazo ya Samia. Huu ni uwekezaji mkubwa sana kwa chama. Kuruhusu asigomber chama kitapata hasara kubwa sana kwa sababu kimemu-Brand kwa miaka mingi na kwa pesa nyingi sana mabilioni na mabilioni.

2. Chama kimetengeneza Baiskeli na pikipiki nyingi sana kwa gharama kubwa sana kwa ajili ya kumtangaza Samia nchi nzima. Haya yote ni maandalizi ya kampeni na ndo kampeni zenyewe kwa takribani miaka miwili iliyopita. Samia kutogombea tutapata hasara ya mabilioni.

3. CCM iliunda vikundi vya machawa na makunguni wa mama kwa lengo la kutangaza Samia na kumfanyia Branding. Vikundi hivi vimezunguka nchi zima kuweka mabango na kumnadi kwa pesa za CCM na serikali. Kimewalipa mishahara na posho kwa takribani miaka minne. CCM Imewekeza mabilioni ya pesa. Samia Kutogombea chama kitapata bonge la hasara.

4. CCM imegawa kanga, vitenge, tshirt, kofia, miwani, mikoba na hata chupi kwa akina mama na baba nchi nzima zenye picha yake wakimnadi. Yote hayo ilikuwa ni kumfanyia Branding na kutangaza ili ashinde uchaguzi. Chama kimetumia mabilioni na mabilioni kwa ajili ya Samia. Kutogombea chama kitapata hasara kubwa sana.

5. CCM iliwekeza kwenye michezo (mpira wa miguu na michezo mingine) kwa kununua magori na kutoa pesa. Kila kona tunasikia Mama kanunua magori mara katoa pesa hizi. Yote haya yalifanyika kwa ajili ya kumtangaza kwa wananchi ili apate ushindi mkubwa kwenye uchaguzi. Yametumika mabilioni ya pesa. Samia asipogombea chama kitapata hasara kubwa sana.

6. CCM iliwekeza kwenye ujenzi wa makanisa na misikiti kwa mgongo wa Samia, kuwa Samia kachangia mamilioni haya ili kutangaza kwenye makanisa na misikini kuwa ni mtu wa huruma sana kwa waumini wa kikristo na waislamu. Jina la Samia lilisikika kwa kila waumini na kujua kuwa anawapenda japo ni geresha tu. Mabilioni na mabilioni yametumika kumtangaza Samia. Samia asipogombea chama na serikali kitapata hasara kubwa sana ya ma B na B.

7. CCM imewekeza kwenye media kumfanyia branding Samia. Imewekeza kwenye kununua vyombo vya habari na waandishi wa habari uchwara. Yote haya ni kumtangaza Samia kwa wananchi na kumpa maujiko kemkemu. Yametumika mabilioni ya pesa. Asipogombea chama kitapata hasara kubwa sana.

8. CCM imewekeza kwa wasiojulikana kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wote wanaompinga Samia watakipata cha mtema kuni. Ama auawe, ateswe, apotezwe au afungwe. Vikundi hivi vimenunuliwa magari, bunduki, na pingu. Bado posho na mishahara yao. Bado mafuta ya kwenda popote wanakotaka. Yaani wanaweza kukuteka Arusha wanaenda kumalizana na wewe katavi. Wese lake si mchezo. Chama kimewekeza pesa nyingi sana. Samia kutogombea chama kitapata hasara kubwa sana.

9. N.k

Ushauri: CCM msibadilishie gia angani, endeleeni na msimamo wa kwenda na Samia hata kama hapendwi au taratibu zimekiukwa. Endeleeni kuimba wimbo wenu kuwa CCM mbele kwa mbele, wataisoma nambaaaaa. Imarisheni tu mbinu ya kupora kura kupitia makada wa CCM, polisi, Tume, wakurugenzi na vyombo vingine vya dola.
 
Back
Top Bottom