Ushauri: Serikali idhibiti vipindi vya michezo kwenye redio na TV nchini

Wacha upuuzi, yaani mtu uache kufanya kazi unasikiliza kipindi cha michezo kisicho na tija maishani mwako? Jiulize, toka uanze kusikiliza vipindi vya michezo umefaidika na nini maishani mwako zaidi ya kusikia kelele tu za watu?
 

Wewe inaonekana ndio huna kazi, maana ungekuwa una kazi ya maana pengine usingeyajua hayo! Ina maana wewe hutumia muda mwingi kusikiliza hivyo vipindi huo muda wa asubuhi, kuna wengine hata hawajui kama hivyo vipindi vipo!

Halafu kama unataka huo muda ubadilishwe, unataka vipindi gani ndio viwekwe huo muda ama radio na tv zisiwe na vipindi kabisa huo muda unaosema ni wa kazi ili watu wakafanye hizo kazi unazosema hawafanyi!??
 
Freedom of speech ipo kwenye Sport ndio maana radio wana toa Airtime muda mrefu.
 
Hoja iko sahihi ila wanaojadili naona wameamua kumjadili mtoa hoja na sio hoja yenyewe.
Mtoa hoja kachemsha jioni wakati watu wamerudi nyumbani ndio wawekewe vipindi vya maana, asubuhi watu wako busy wawekewe michezo special for jobless
 
Halafu huo uchambuzi hao watangazaji wanashindana yupi anaewajua vizuri wachezaji wa Ulaya na timu zao fully porojo

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Ikiwa watafungia vipindi vya michezo itabidi wafungie pia vipindi vya music na burudani za aina nyingine kitu ambacho sidhani kama kina tija sababu hakuna anaekulazimisha kusikiliza,
Mi sijui we unafanya kazi gani ambayo ukimsikia Kitenge au Ambangile anaongea unashindwa kabisa kufanya kazi kiasi cha kudhani uchumi utadorora sababu ya vipindi hivyo kuwepo asubuhi!

Naomba kufahamu ni kituo gani hicho ambacho kinauchambuzi wa michezo masaa 8[emoji848][emoji848]
 
Nimeonyesha mchango wa michezo kwenye uchumi, hivyo michezo ni muhimu ila tatizo liko kwenye vipindi vya michezo hapa nchini.
Hivyo vipindi vinazuiaje watu kufanya shughuli zao za kujipatia kipato?
 
Kumbuka lakini kuwa hata hao wanaotangaza hiyo michezo wapo kazini
 
Nimeonyesha mchango wa michezo kwenye uchumi, hivyo michezo ni muhimu ila tatizo liko kwenye vipindi vya michezo hapa nchini.
Hizi habari za kutaka serikali iingilie uhuru wa watu, na uhuru wa habari ni ujinga mtupu.

Mwisho wake ni censorship na serikali kuminya uhuru wa habari.

Kitu kibaya zaidi, wananchi ndiyo wanashauri hivi.

Lakini siwezi kushangaa. Hii nchi watu wamejazwa ujinga mpaka serikali ilikataza bunge kuoneshwa live!

Yani unawafanya watu wote kama watoto na serikali ndiyo baba hao!
 
Reactions: Auz
Exactly my thoughts....ukipanda daladala michezo, mwendokasi michezo, habari zingine mpaka kwenye taarifa ya habari.
 
Mkuu lazima ukubali kuwa sio lazima watu wote tuwe na mtazamo sawa kwenye mambo.

Wewe unaweza kuona kama ni censorship lakini mimi nikaona ni regulations tu ambazo zinaweza kutumika kuhamasisha watu kufanya kazi nyingine za uzalishaji.
 
Upo sawa kabisa. Hadi thamani ya vipindi vya michezo imepotea. Sipendi sana hii tabia.
 
Ndio maana kwa sasa hakuna kitu chenye kuelimisha na kufundisha zaidi michezo michezo kila wakati.

80% ya soga masokoni na vijiwe vingi ni mpira tu
Sasa hizo TV zikianza kuichambua serikali au mambo ya matukio yanayoendelea nchini wanaishia KUPIGWA MA FINE MAKUBWA MPAKA KITUO CHA TV NA REDIO KINAPOTEZA DIRA LA SIVYO VITUO VYOTE VIWE KAMA TBC MWENDO WA KUPONGEZA
 
Mkuu lazima ukubali kua sio lazima watu wote tuwe na mtazamo sawa kwenye mambo.

Wewe unaweza kuona kama ni censorship lakini mimi nikaona ni regulations tu ambazo zinaweza kutumika kuhamasisha watu kufanya kazi nyingine za uzalishaji.
Kwani wapi nimesema wote lazima tuwe na mawazo sawa?

JF nayo utataka serikali ipange muda wa kuchangia?
 
Mtoa mada upo sawa kabisa tatizo wengi wamekuja kinyume na wewe kwa kuwa wana mawazo yao tofauti na yako. Kwa upande wangu napendekeza vipindi vya michezo vifanywe mida ya jioni baada ya wahangaikaji walio wengi kurudi majumbani mwao.

Wale wachache wanaohangaika usiku watakua wanapata hizo habari kupitia taarifa za habari au mitandaoni. Michezo ni burudani yafaa mtu aipate hiyo burudani akiwa amepumzika. Huo mchana wafanye vipindi vingine tu kama mziki visivyohitaji concentration ya watazamaji na wasikilizaji.
 
Ushakua mkubwa Sasa, ACHA utoto ,Kuongeza,

Sasa ni vipindi gani unataka viwekwe asubuhi Ili viangaliwe na wasio na KAZI?

Na wale wanaoingia KAZI za usiku na asubuhi wanakuwepo nyumbani na jioni tena WANAONDOKA hao nao umewafikiliaje??

Au umejiangalia wewe???

Tutolee uchafu wako hapa.
 
Ingekuwa agricultural revolution ya China ni sawa na hicho unachokisema wewe naamini wasingefanikiwa,
 
Ukisema hivyo utakuwa sawa lakini ukiongezea tu kuwa serikali idhibiti hapo ndio shida inapokuja maana itabidi ipange hadi vile vipindi vyao shilawadu au fashion viwe vinafanyika muda upi, sasa hapo zitabaki tu media za serikali na za dini zile zinazojiendesha zitashndwa kufanya biashara maana wao kila kipindi chao kinakuwa kimetarget watu flan kwa muda huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…