Ushauri: Serikali idhibiti vipindi vya michezo kwenye redio na TV nchini

Yaani kila kitu mnataka mdhibitiwe why? Kwa nini? Inaonekana wewe umezoea kuchungwa kama kondoo...
 
Reactions: Auz
Kila kitu kwa wakati wake 75 % ya watu wanahitaji muongozo wakiachwa tu muda wote huo watakuwa kwenye redio na sio kuzingatia kazi. Tukienda maofisini tunalalamika kazi haziendi.
Hoja ya kipumbavu sana hii, hivi kuna mtu ameshawahi kuja kukumba chakula? Au kuna siku serikali imegawa chakula bure nchi nzima? Yaani unataka watu 60 milioni wapangiwe namna ya kuishi? Kuna watu asubuhi unamkuta anapiga supu na bia yake, je unajua usiku kucha alikuwa wapi? Hebu acheni kukariri maisha nyie.
 
Inategemea unazungumzia nani, dereva wa daladala, wa lori, wa Bus, bodaboda vijiweni kwao, wauza maduka, sokoni, mitumba etc hawawezi kusikiliza kweli?
 
Hii serikali ndio maana inaingilia kila kitu. Maana inakaribishwa hata katika mambo yaliyo katika uamuzi wa mtu binafsi. Yaani wewe huwezi kujidhibiti kutumia muda wako vizuri hadi serikali iingilie maisha yako?
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Unaweza kuwa sahihi kwa kiasi fulani ila naona umezungumzia kiujumla kama Watanzania wote wanapenda Michezo hasa mpira maana ndio mchezo unaopendwa.

Tunajua kila kipindi kina wasikilizaji wake na vimewekwa muda tofauti. Na ni dunia nzima iko hivyo. Kwa mawazo hayo basi itabidi vifungiwe vipindi vyote vianze hiyo saa 10 jioni.

Utu uzima unahusisha kutambua majukumu yako, vipaumbele ,na matumizi mazuri ya muda. Dunia ina vitu vizuri vingi vya kufurahia ila si vyote tutavipata. Ni swala la mtu binafsi kujizuia. Ukishindwa kujizuia baadhi ya mambo ili utimize majukumu mengine muhimu kwa afya ya maendeleo yako basi hautakuwa binadamu wa kawaida.

Na tukumbuke wanaochambua michezo wako kazini wanatengeza mkate wao watoto wale. Na ili walipwe ni lazima watafute fursa za kuuza vipindi kwa wawezeshaji kifedha ambao ni wadhamini. Hivyo inaweza kuwa asubuhi au jioni yote sawa . Ikiwa unaona wenzio wako kazini halafu unasikiliza story zao wewe huingizi kitu basi jitathmini.

Vipindi vingi vinavyohusu burudani na starehe kwa vijana vinaanza saa 6 mchana mpaka saa 12 jioni, muda ambao vijana wengi walengwa wa hivyo vipindi wako darasani au majukumu mengine. Kwa hiyo navyo vihamishiwe muda gani?
 
Reactions: Auz
Hoja iko sahihi ila wanaojadili naona wameamua kumjadili mtoa hoja na sio hoja yenyewe.
Shida ya Jf mchangiaji wa kwanza akianza na ushuzi tu Tegemea vinyesi huko chini ni uovyo wa Hali ya juu humu.Kuna hoja happy wanamshambulia mtoa Mada.Vipindi vianzie 10 jioni wote tuwe na nafasi ya kusikiliza.Sio kila Mtanzania muuza duka au genge au Dereva daladala kuwa atasikiliza muda wote michezo.
 
Unashangaza sana. Kwani ni lazima mtu kuangalia kipindi Cha michezo. Kwa hiyo unashauri TVs waanzishe vipindi vya kazi????
 
Hata kama itachambuliwa 24hours unatakiwa kutune kila kwa mda wake
 
Huna akili mpumbavu kabisa.
 
Hivi vipindi vya michezo kwa miaka ya leo naona kama vimepoteza sifa na umaana wake,vimekuwa ni vijiwe vya kahawa vilivyochangamka.Havina tofauti kubwa na vijiwe vya kahawa vya mtaani,tofauti labda wao wanalipwa mshahara na hawana kahawa ila wale wa vijiwen wanapata kahawa ila hawana mashahara!! Mtoa mada upo sahihi,wachache watakuelewa!!
 
Kwani wewe mchambuzi gani ambaye humpendi yaani!
 
Iambie serikali izuie mechi za mpira siku na masaa ya kazi.
 
Naona huo ulevi umehamia huko maana kipindi kile ilikua bunge live hali ilitisha,

Unakuta asubuhi bar imefunguliwa vijana wanacheza pool table, hapo pembeni kuna kijiwe cha soga halafu wako wanaotoa lock huku wakitazama bunge live.

Magufuli was right.
 
Kwahiyo wakiweka mziki pia utalalamika wanaplay sana mziki watu hamfanyi kazi Basi vyombo hivyo vifungwe muda wa kazi mkuu

NB. Sio lazima kusikiliza asubui kunacradio stations nyingine vipindi vya uchambuzi wa michezo vipo jioni na usiku kabisa kupanga ni kuchagua
 
Sijaielewa mantiki ya bandiko lako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…