Ushauri: Serikali ongozeni kidigitali Kuna mambo ukisikia bado yanafanywa yanashangaza sana

Ushauri: Serikali ongozeni kidigitali Kuna mambo ukisikia bado yanafanywa yanashangaza sana

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Miaka imesonga sasa badilisheni baadhi ya mambo muendane na ulimwengu wa kidigitali mambo kama;

1. Mwenge wa uhuru na kuwatoa wanafunzi mashuleni na kuwapanga msululu yamepitwa na wakati

2. Wanafunzi kukimbia mchakamchaka na kuimba nyimbo za kambona na idd amini

3. Siku ya wafanyakazi walimu na watumishi kuvaa (ma) t-shirt na kuungua juani kwa kutembea

4. Kubeba watu kwenye malori kwenda kwenye mikutano na kampeni

5. Kuzindua miradi na misululu ya magari na ving'ora

Mengine wadau mtaongeza, lakini ninachojaribu kusema hayo mambo yanahitaji mamboresho katika ufanyikaji wake ili tuendane na Kasi ya Dunia ili tusionekane washamba mbele ya Dunia. Mengine ni ya kufutwa kabisa maana ufanyikaji wake unatia aibu Taifa kama mwenge wa uhuru
 
Kuna mambo wananchi wenyewe wanapaswa kuachana nayo, hili la kupakiwa kwenye malori lipo ndani ya uwezo wa wananchi wenyewe
 
Kuna mambo wananchi wenyewe wanapaswa kuachana nayo, hili la kupakiwa kwenye malori lipo ndani ya uwezo wa wananchi wenyewe
Wanachukua watu walio kwenye miliki Yao hasa wafanyakazi na wanafunzi raia wa kawaida ni wachache wanaoweza kupewa kamshiko

Hili ili likome watu wa serikali kuu waache huu ukale mambo yamebadirika kwa sasa
 
Hao ndio wanaofanya mfumo huu uendelee
 
Back
Top Bottom