Kifupi huo ndio ushauri wangu. Tusifanye mikataba mirefu ya kujifunga kwa miaka 100 kwani mambo hubadilika sana na tutafika mahali tutakuwa hatuna la kufanya na mikataba mibovu.
Tufanye nini? Najua shida yetu kubwa katika kila kitu hapa nchini ni uendeshaji mmbaya na sio kukosekana kwa fedha. Tumewahi kupokea fedha nyingi za misaada lakini tukaishia kuzitumia hovyo kwa kukosa good management au weledi.
Tunashindwa kwenye technical aspects na management. Timu hii ifanye shughuli za kiufundi na kiuendeshaji ikifanya kazi sambamba na wazawa hadi pale utendaji utakapoboreka.
Ni rahisi na salama zaidi kufanya hivyo kuliko kibinafsisha muundombinu wa bandari ambao ni mlango wa nchi yetu.