Ushauri: Simba SC isihofie mabadiliko ikiwa inataka kufika mbali kisoka katika bara la Africa na duniani kwa ujumla

Ushauri: Simba SC isihofie mabadiliko ikiwa inataka kufika mbali kisoka katika bara la Africa na duniani kwa ujumla

Tipstipstor

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
1,528
Reaction score
3,352
Ahlan Ahlan bik

Habari zenu wana Jf, wadau wa soka na wapenzi wa wana lunyasi, giants of Africa, Simba Sc.

Jana nilipata safari kidogo kutoka Bergamo kwenda katika jiji la bandari, Piraeus nchini ugiriki .Jiioni nikiwa naitazama bahari ya meditterenian katika kitongoji cha Freattyda nikawa nawaza kuhusu maendeleo na mabadiliko ya soka ya klabu yangu pendwa barani Afrika nayo si nyingine zaidi ya Simba Sc.

Simba Sc inabidi tufanye mabadiliko ya sera zetu hususani katika suala la kiufundi.Sina shaka hata kidogo juu ya weledi wa watu wanaofanya kazi katika utawala.Nazungumzia mkurugenzi mtendaji ,CEO mheshimiwa Barbara Gonzalez na wanabodi wote wa simba. Suala kubwa la kwanza linalohitaji mabadiliko ni katika Scouting team yetu ,jinsi gani tunasaka wachezaji wa kuweza kuivusha simba kimataifa.

Inanipa wasiwasi sana kuona klabu changa kama Singida big stars inaweza kuleta wachezaji mahiri sana kutoka taifa la brazil kuja kuichezea timu isiyojulikana barani Africa huku sisi tukistruggle kupata wachezaji wa maana. Hili liangaliwe mno.Uwekezaji unaofanyika simba ni mkubwa hivyo lazima kazi ya scouting team ifanywe kwa jicho la mwewe katika kuleta wachezaji watakaoipa thamani simba.

Pili, ni kuhusu usajili wa makocha na wachezaji, tujenge utaratibu wa kuhakikisha pindi tunamtimua kocha na kuleta kocha mpya basi tumpe nafasi ya kuteua benchi lake zima la ufundi.Wengi tunapiga kelele kuwa tunataka chemistry ya wachezaji uwanjani ila tunasahau kuwa makocha pia wanahitaji chemistry!! Muunganiko ambao utawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.

Makocha wakubwa wote wanapopewa kazi katika timu huku barani ulaya huwa na kawaida ya kuchagua timu ya makocha watakaofanya nao kazi na ni jukumu la klabu kuwapa mikataba ili wamsaidie kocha mkuu ila kwa huko Tanzania hali ni kinyume kabisa unakuta kocha anasajiliwa na timu halafu anapangiwa watu wa kufanya kazi nae.Ni sawa umchukue pisi kali ya kigiriki hapa Athens halafu uilete huko tanzania uilishe ugali au makande..it won't work out!! Vyakula vya hapa ugiriki ni tofauti na vya huko bongo ,atalazimika tu kula ikiwa hakuna chakula kingine ili asife njaa ni sawa na hawa makocha tunaowaleta.

Tuhakikishe kuwa tunawapa nafasi ya kuchagua watu wa kufanya nao kazi na pia tuwape muda atleast misimu miwili tuone nini wanaweza kuifanyia klabu yetu pendwa na ikitokea hatujaridhishwa nao basi tunatimua benchi lote la ufundi.

Sio kocha unamtoa serbia halafu msaidizi unampangia ni lazima awe Matola (mtanzania), hawafahamiani hata falsafa zao za ufundishaji n.k halafu unataka kikosi kiwe na chemistry ndani ya wiki mbili ili hali hao makocha wenyewe wanaweza kukaa miezi miwili hawaelewani falsafa zao.

Tatu, ni lazima kocha apewe nafasi ya kurecommend ni wachezaji gani anawahitaji katika kikosi chake, haiyumikiniki unamleta kocha halafu wachezaji unasajili tu bila ya matakwa ya kocha.Unakuta kocha anahitaji mshambuliaji mrefu ili aendane na falsafa yake ..kwa maana anaweza kumsaidia hata kwenye kudefend set pieces ila timu inasajili striker mfupi kama kichuya ambaye hata hawezi kuruka juu ku-win aerial duels. Management ya klabu iache kusajili kwa mihemko ,inabidi impe nafasi kocha ajiridhishe kwanza iwapo huyo mchezaji anayetaka kusajiliwa ataisaidia klabu ama laa.

Mwisho kabisa napenda kutanguliza shukrani zangu kwa uongozi wa simba ,benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla kwa ushindi wa kwanza katika ligi kuu ya NBC. Tumpe ushirikiano kocha Zoran Maki na wachezaji wajitume waache makundi.

Sio kwasababu Kocha Zoran kakataa baadhi ya wachezaji ndio hao waliobaki wacheze chini ya kiwango ili tu wamtengenezee kocha mazingira ya kufukuzwa.
 
Kwanza simba hatuna menejementi nzuri ili liko wazi wale wahindi mo na demu wake wanapenda sifa za mitandao kazi sifuri na waongo waongo tu, pili klabu zetu ikiwemo simba hawataki akili ya kibunifu ije yaaani kocha akija anapangiwa kila kitu sio yeye apange tatu hakuna uwazi kwenye mapato ba matumizi financial statement zake ziko Kifichoni hazionekani hata kwa kuomba sasa na sisi mshabiki akili tusivyo kywa nayo tunashangilia taasisi kubwa mapato yake kuingia kwenye account binafsi, wawekezaji wote GSM na MO hawa wote hawana nia ya kuvikuza hivi vilabu bali wanavitumia pasi na kuweka kitu baadae wata ondoka na kuviacha kuanza sifuri tena
 
"..sawa, tushajua uko Ugiriki". Alisikika mwanaJF mmoja akinanga!!
 
Victor Akpan alivyosajiliwa kwa mbwembwe leo hii hawamtaki? Daah mimi kama shabiki kindakindaki inaniuma sana
Hii kauli kuwa Akpan hatakiwi pale Simba imetolewa na kiongozi gani? Binafsi sijamsikia kocha wala kiongozi yoyote wa Simba akiongea hivyo. Tuache majungu tufanye kazi. Kama kutocheza wachezaji wengi tu hawajacheza, je na wao pia hawatakiwi? Mtaweka wapi sura zenu siku mkimuona Akpan uwanjani? Tuache kuingilia kazi za kocha.
 
Hii kauli kuwa Akpan hatakiwi pale Simba imetolewa na kiongozi gani? Binafsi sijamsikia kocha wala kiongozi yoyote wa Simba akiongea hivyo. Tuache majungu tufanye kazi. Kama kutocheza wachezaji wengi tu hawajacheza, je na wao pia hawatakiwi? Mtaweka wapi sura zenu siku mkimuona Akpan uwanjani? Tuache kuingilia kazi za kocha.
Taarifa kutoka kwa kocha zinasema kuwa Akpan haendani na falsafa ya kocha mkuu na ndio maana inatakiwa auzwe au atolewe kwa mkopo

kama huamini, muda utasema
 
Taarifa kutoka kwa kocha zinasema kuwa Akpan haendani na falsafa ya kocha mkuu na ndio maana inatakiwa auzwe au atolewe kwa mkopo

kama huamini, muda utasema
Hiyo taarifa kutoka kwa kocha ipo wapi? Mbona hatuioni? Je, ipo kwenye Simba App? Hii ni taarifa rasmi au ya vijiwe vya kahawa?
 
ushauri mzuri sana.
Manzoki anakwama kuchezea Simba caf kisa eti kabakiza miezi miwili,Simba wamegoma kutoa hela wanasubiri kitonga cha free agent.
 
Back
Top Bottom