Ushauri tafadhali, Vodacom wameniumiza

Hayo mambo yako ya kukariri darasani weka pembeni. Jamaa ana hoja, hiyo line ni ya biashara, mkataba alioingia nao ni wa huduma ya kutoa na kuweka pesa, huduma hiyo tu. Hoja yake,. Inakuaje, muajiriwa wake ameweza kufanikisha hilo la kukopa bila hao "voda" kumjulisha mmiliki?
 
Sasa kama kuna options za kukopa kwenye line inashindikana vipi mtu kukopa. Unless voda waweke secondary level security code ambayo ni ya admin tu hio ya mpesa uwakala iwe na pin tofauti.
 
Hapo mkuu mtafute mtuhumiwa..... Voda hawahusiki kwa sababu hawakukwambia umwajiri mtu.

Songea pia ulikubali vigezo na masharti kwa kubonyeza 1.


Pole sana

Ova
Hahahah na huu ndio ukweli, yeye kaingia mkataba na Voda. Vodacom hawamtambui huyo kijana wake wa kazi so wanaamini wanafanya kazi na yeye katika huduma zote.
 
Duh hio riba kiboko, mimi ningetupa line kummmk kama mbwai na iwe mbwai tu😁 bora kesi iungurume.
20500 kwa mwezi ni laki 415,000 kudadadeq! Af ukiangalia hela kachukua mtu baki tu kaenda kufanyia mambo yake.
 
Tatizo ulishindwa kuishi nae kwa upendo, hivi mtu anakufanyiaje ubaya kama unaishi nae kibinadamu? Ukute mshahara ulikuwa hulipi kwa wakati unajifanya mwamba na kelele nyingi sasa dogo kapiga kwenye mshono. Pambana na hali yako tu 🤣
 
Ukimaliza ubabe wako nenda kalipe deni za watu.

Hili ni lako asilimia mia. Wewe ndio uliingia mkataba na Vodacom kwahiyo ni jukumu lako kutunza line zako na kila kitu. Vodacom wanakujua wewe kupitia hizo line, kwahiyo nafasi yako inawakilishwa na hizo line. Line ikiingia mkataba wowote ni wewe ndio umeingia

Ulipaswa kuripoti upotevu wa hizo line immediately ili Vodacom wasiendelee kuwasiliana nazo
 
Si ukomae na kesi ya wizi iliyowazi kuliko kuendesha kesi nyingine usiyojua hata kanuni zake, Kadiri muda unavyozidi dogo anazidi kuitafuna na kuhonga, anazidi kutafuta mbinu za kukukwepa.
Upepo utageuka, una kesi yako ya madai, voda nao wana kesi na wewe ya utapeli.
 
Kabla ya kukopa au kujiunga na huduma fulani huwa kuna vitu hivi tunachukulia poa.
Bonyeza moja kubali vigezo na Masharti <url> au link ya vigezo na masharti unapewa[hatusomagi] ✅️
Weka namba yako ya siri kuthibitisha (Hapa umeweka saini ya kidigitali kuwa ni wewe unakopa, kumbuka namba ya siri ni saini yako kimkataba)✅️

Haya hiyo kesi Voda unawasumbua kwa lipi?
Mikataba babu hatusomi ndo tatizo letu. Terms and Conditions a.k.a Vigezo na Masharti....hapo pambana na huyo uliyemwachia line zako na ofisi
 
sasa mkuu mfanyakazi umempa uwakala wa ofisi ya miamala ya M PESA na Tigo pesa tena ana NIDA yako,LESENI,TIN namba na PASSWORD alafu isitoshe wakala anaruhusiwa kukopa kuongeza Float..na kijana amekopa kwa jina lako sababu umempa accss ya taarifa zako zote za biashara.. kwakuwa biashara inamesajliwa kwa majina yako hao voda hawajui nani anaendesha biashara bali wanamtambua mmiliki tu..
 
Tatizo ulishindwa kuishi nae kwa upendo, hivi mtu anakufanyiaje ubaya kama unaishi nae kibinadamu? Ukute mshahara ulikuwa hulipi kwa wakati unajifanya mwamba na kelele nyingi sasa dogo kapiga kwenye mshono. Pambana na hali yako tu 🤣
Mkuu hujui usemalo.
Tatizo ulishindwa kuishi nae kwa upendo, hivi mtu anakufanyiaje ubaya kama unaishi nae kibinadamu? Ukute mshahara ulikuwa hulipi kwa wakati unajifanya mwamba na kelele nyingi sasa dogo kapiga kwenye mshono. Pambana na hali yako tu 🤣
Dogo nimekaa nae miaka 5 hadi sasa.
Nimepata chumba analala bure, anakula bure, anatibiwa bure na mshahara wake haijawahi tokea hata siku moja asipate kwa wakati.
Watoto wangu wanamuita kaka. Ni vile ubaya haupigi hodi!
 
Sasa mtafute huyo mwizi wako yeye ndio atalipa Hilo deni laah sivyo sidhani kama Voda watakuelewa maana wao wamekukopesha wewe ndio mwenye lain so kwa kifupi hapo UMEIBIWA tu ndugu so mtafute mwizi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…