Mkuu hiyo huduma iko hivi. Kuna wakati kama wakala unaweza kujikuta una cash lakini huna float, sasa mawakala huwa wanabadilishana float unakuta una wakala unamjua labda unamtumia tigo yeye anakutumia ya voda na ndio maana wana magroup yao. Hii si official ni njia watu waligundua kuweza kuepuka kwenda kudeposite pesa kila mara.
Sasa voda wao wakaja kuwa ukiishiwa float kama wakala unaweza kukopa float kwa hiyo line yako. ukirudisha ndani ya saa 10, makato ni madogo sana ila yakizidi makato ndo yanakuwa makubwa kidogo na wanaikata pale unapoweka floaat, au mtu akija akatoa pesa.
Sasa zamani line zilikuwa mbili, ya kuendesha biashara nyingine ya kufuatilia biashara na kupokea comission. Siku hizi huo mfumo haupo line ni moja ile ile till. So messages na kila kitu ni humo humo kwenye line.
Hivyo, ukiweka mtu hakikisha unamwamini, unafuatilia maana kitendo cha kumpa mtu line, fedha in cash, float ni sawa umempa power of attorney kufanya yale yote wewe mwenye line uliyostahili kufanya.
Na hii huduma ipo kufanya mtu anayehitaji float kwa dharura aipate haraka labda mtu anataka kuweka ila kapungukiwa, sasa ikiwa itachukua muda huo itakuwa haina maana kwa kuwa mtu si angeenda deposite tu kama kawaida.