Sultan MackJoe Khalifa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2022
- 6,782
- 14,148
Unampa mtu kazi ya pesa na akisepa hujui utampataje!.
Mtafute huyo dogo janja alipe ukimkosa unalipa wewe.
Mtafute huyo dogo janja alipe ukimkosa unalipa wewe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu usijifanye mjuaji kwenye jambo ambalo hulijui na huna uzoefu nalo.Uelewa wako ni duni sana ,unajidai kuuliza maswali ili yaonekane ni logic questions kumbe ni upupu,wewe ndo ulimpa access huyo msimamizi wa Laini Yako na ukampa password,Sasa unadhani voda wana vifaa vya kujua kuwa huyu anayekopa ni mmiliki wa Laini au siye!?
Jichanganye kuwashitaki waje wakufirisi Hadi uhame mtaa,,mfano Mimi Laini yangu ya voda inakopesheka Hadi sh 2M Sasa siku nikikuta mtu kaikopa hiyo Hela ni washitaki vodacom au mtu niliyempa access ya Laini yangu?
Kuna haja ya kuanzisha vyuo vya kukuza uelewa Kwa watanzania
Kuna watu ni hawaridhiki hata uwafanyie nini unaweza kuta alikua anakaa nae vyema anamlipa vizuri ila ndio kaingiwa na tamaa. Hujawahi ona watu wana mishahara mizuri, maisha mazuri ila ni wezi??Tatizo ulishindwa kuishi nae kwa upendo, hivi mtu anakufanyiaje ubaya kama unaishi nae kibinadamu? Ukute mshahara ulikuwa hulipi kwa wakati unajifanya mwamba na kelele nyingi sasa dogo kapiga kwenye mshono. Pambana na hali yako tu 🤣
Kwenye Laini Kuna huduma nyingi sana,ili kuonesha kwamba umeipenda huduma utabonyeza kitufe,kama hujaipenda acha kubonyeza kitufe husika.Mkuu usijifanye mjuaji kwenye jambo ambalo hulijui na huna uzoefu nalo.
Hii huduma kwanza sikujua km ipo.
Pili sijawahi kuiomba.
Tatu kwenye biashara mara nyingi tunashirikiana na watu wa mshahara.
Huwezi kumpa mtu kazi ya simu pesa na usimpe pin za line husika, hataweza kufanya huduma.
Line zote Tigo, Airtel, Hallotel hawana huduma hii kwenye line ya biashara.
Hata voda walipoanzisha huduma hii ilipaswa watujulishe sisi mawakala tunaomiliki hizo line.
Nadhani nimeeleweka.
Pole Boss.Hii huduma ya kukopesha kipindi naanza hii biashara haikuwepo na mimi sikujua km ipo hadi yalipotokea yaliyotokea .
Wamjulishe kwa njia gani? Nadhani hata huduma mpya wanapaongeza wanamjulisha kwa njia ya message (ambayo bado itafika kwenye simu hiyo ambayo anayo msaidizi wake) Hoja ya msaidizi amewezaje kukopa milioni 2 inakosa mashiko kisheria maana hata hapo kazini umempa pesa zaidi ya hizo na anasimamia miamala mikubwa zaidi ya hiyo kwa niaba yako na kwa kutumia saini yako(PIN).Hayo mambo yako ya kukariri darasani weka pembeni. Jamaa ana hoja, hiyo line ni ya biashara, mkataba alioingia nao ni wa huduma ya kutoa na kuweka pesa, huduma hiyo tu. Hoja yake,. Inakuaje, muajiriwa wake ameweza kufanikisha hilo la kukopa bila hao "voda" kumjulisha mmiliki?
Wapo sana wengi tuKuna watu ni hawaridhiki hata uwafanyie nini unaweza kuta alikua anakaa nae vyema anamlipa vizuri ila ndio kaingiwa na tamaa. Hujawahi ona watu wana mishahara mizuri, maisha mazuri ila ni wezi??
Hayo mambo yako ya kukariri darasani weka pembeni. Jamaa ana hoja, hiyo line ni ya biashara, mkataba alioingia nao ni wa huduma ya kutoa na kuweka pesa, huduma hiyo tu. Hoja yake,. Inakuaje, muajiriwa wake ameweza kufanikisha hilo la kukopa bila hao "voda" kumjulisha mmiliki?
Hakuna hoja kwa sababu wachangiaji hamwelewi kuwa huo mkopo ni wa voda kwa mawakala pale wanapokuwa wameishiwa float. Ni huduma waliyoianzisha na walikuwa wakipita kwa mawakala kuwataarifu juu yake. Sio mkopo kama mkopo wa kawaida wa nipige tafu au songesha huu ni kwa mawakala na kiasi wanachokupatia kinaendana na kiasi cha miala unachofanya.Hapa ndipo kwenye hoja yangu.
Ipoanzishwa walikuwa wanapita wanawahimiza watu wa hop in so kijana wako uliyeamuamini, mpaka ukampa password na line atakuwa alijiunga.Hii huduma ya kukopesha kipindi naanza hii biashara haikuwepo na mimi sikujua km ipo hadi yalipotokea yaliyotokea .
Hapa ndipo wachangiaji wengi hawajaelewa. Huduma ya kutoa na kuweka pesa n huduma moja inayojitegemea, kadharika huduma ya kukopa "float" ni huduma nyingine inayojitegemea. Kwa usahihi, inafaa mitandao ya simu waongeze control kuzuia asiyehisika na usajili wa laini kuwa na uwezo wa kukopa / kuingia mkataba katika huduma hiyo pasipo ruhusa ya muhusika.Hii huduma haukuwepo kabla hata mimi sikujua km voda wameanzisha huduma ya kukopesha.
Msingi wa lalamiko la mleta uzi ni kukosekana kwa "control" ama kuwepo kwa "control" hafifu zinazonufaisha "third party" bila muhusika mkuu kuwa na taarifa. "Control" inayozuia mtu wa tatu kuweza kijiunga ama kuingia makubaliano kwa huduma mpya kama hizo za mkopo.Voda hawahusiki Hapo.
Mkataba wa mwenye biashara na mfanyakazi wake hauna uhûsiano na Vodacom.
Voda inajua anayefanya biashara ni mtoa Mada kama ameajiri au hajaajiri hiyo haihusiani
Taikoni jaribu kufikiria katika mlengo wa biashara na uwekezaji. Hayo uliyoandika hapa yana tija na yana nguvu katika laini binafis, na hata mitandao ya simu wameweka mahitaji tofauti baina ya usajili wa laini binafsi kwa ajili ya huduma za mawasiliano binafsi.Utaambiwa wewe ndiye umekopa Kwa sababu zifuatazo;
1. Laini imesajiliwa Kwa Jina Lako.
2. Sheria za Tanzania hazitambui kuwa laini yako inaweza Kutumiwa na Mtu Mwingine ndîo maana Hilo NI Kosa Kisheria.
Kîla Mtu anatakiwa atumie laini Yake.
3. Namba ya Siri ya laini na akaunti za Pesa niza MTU binafsi yàani wewe. Hauruhusiwi Kutoa Namba yako ya Siri Kwa Mtu yeyote hata kama ni Mkeo au mtoto au Mzazi.
Hivyo Hapo wewe ndîo utawajibika.
Huyo kijana aliyekopa anaweza pia kukuruka.
Hapa ndipo wachangiaji wengi hawajaelewa. Huduma ya kutoa na kuweka pesa n huduma moja inayojitegemea, kadharika huduma ya kukopa "float" ni huduma nyingine inayojitegemea. Kwa usahihi, inafaa mitandao ya simu waongeze control kuzuia asiyehisika na usajili wa laini kuwa na uwezo wa kukopa / kuingia mkataba katika huduma hiyo pasipo ruhusa ya muhusika.
Msingi wa lalamiko la mleta uzi ni kukosekana kwa "control" ama kuwepo kwa "control" hafifu zinazonufaisha "third party" bila muhusika mkuu kuwa na taarifa. "Control" inayozuia mtu wa tatu kuweza kijiunga ama kuingia makubaliano kwa huduma mpya kama hizo za mkopo.
Taikoni jaribu kufikiria katika mlengo wa biashara na uwekezaji. Hayo uliyoandika hapa yana tija na yana nguvu katika laini binafis, na hata mitandao ya simu wameweka mahitaji tofauti baina ya usajili wa laini binafsi kwa ajili ya huduma za mawasiliano binafsi.
Laini za uwakala ni laini za biashara na hata mahitaji yake katika kusajili ni tofauti, utahitaji taarifa za kitambulisho kwa utambulisho, leseni ya biashara na tin. Kama wametambua haya katika usajili, ni lazima waje na "control" zenye nguvu kulingana na asili ya matumizi za laini hizo.
Hapa nimekupata. Laini za uwakala ni laizi za biashara, ni wazi na hata wao wanatambua kuwa kuna "waajiriwa" wanatumia laini hizo kwa niaba ya wamiliki. Ni jukumu lao voda kuweka mipaka katika kuzuia "third party" kujiunga na huduma mpya pasipo muhusika kutoa idhini.Labda kwa Ushauri wa Voda na Mawakala nadhani huwa kuna mbinu unaweza ukawa na line Mbili Master na nyingine ya ziada (ingawa sina uhakika) ili wafanyakazi wapewe line ambazo hazina options nyingi ambazo zinaweza kumletea Shida mwenye mali (Ukizingatia Watanzania wameshakuwa Vibaka na hakuna Uaminifu)
Mambo unayachukulia kirahisi sana wewe!Inamana umeajiri mtu ambae hujui details zake vizur, kama unajua kwanin usimtafute mpambane one against one
Swala la uaminifu lina nguvu katika kipengele za kutembea "kuiba" cash.Ulichoandika NI Sahihi lakini hata biashara ni binafsi.
Hapo ni suala la uaminifu tuu.
Lakini pia Vodacom wanaweza ichukua hiyo kama changamoto waongeze akaunti Mbili ndàni ya laini Moja àmbayo ina password tofauti