Ushauri tafadhali, Vodacom wameniumiza

Swala la uaminifu lina nguvu katika kipengele za kutembea "kuiba" cash.

Kujiunga na kuweza kunufaika na huduma ya mikopo kwa laini ya biashara ni madhaifu ya mfumo wa voda katika kulinda wamiliki wa laini hizo za biashara.

Uaminifu Hapo kwèñye cash tuu hata kwèñye Float.
Mpaka umemuajiri Mtu ukampa password kuendesha biashara yako ya uwakala WA mpesa au tigopesa au Airtelmoney NI kwamba umemuamini.
 
Wewe ndio una uelewa duni sana juu ya wajibu wa makampuni ya simu kuweka "control" zenye tija na nguvu kulinda watu walioamua kuwekeza katika biashara ya kipesa.
 
Mm haya makampuni ya simu tangu yalipotumiwa kumuua Tundu Lissu na kumfuatilia Kabendera, sina hamu nayo tena. Haya makampuni ni zaidi ya magaidi.

Na inawezekana mbwa hawa tayari wameishahusika kuwakamata na kuwateka watu wengi sana wakiwemo ambao wamepotea jumla kama vile Ben Saanane, Azori Gwanda, Dkt Masunga, nk. Aidha, watakuwa wamehusika kuwateka raia walioponea kwenye tundu la sindano kuuawa kama vile Sativa, Roma mkatiliki, nk. Inauma sana.
 
Uaminifu Hapo kwèñye cash tuu hata kwèñye Float.
Mpaka umemuajiri Mtu ukampa password kuendesha biashara yako ya uwakala WA mpesa au tigopesa au Airtelmoney NI kwamba umemuamini.
Kumuamini swala moja, kukosekana kwa control ni swala lingine. Malalamiko ni juu ya kukosekana kwa control.

Fikiria hili Taikoni, unamiliki duka, umeajiri kijana kuendesha shughuli za kila siku. Malipo kwa "vendors" ni kwa cheques, wateja wanalipa cash, wewe ndio signatory wa cheque, unafikiri kijana anaweza nufaika dhidi ya balance yako katika akaunti zaidi ya pesa tu anazopokea akiamua kukuibia? Hata kama akaunti ina huduma ya "overdraft"?
 
Swala la uaminifu lina nguvu katika kipengele za kutembea "kuiba" cash.

Kujiunga na kuweza kunufaika na huduma ya mikopo kwa laini ya biashara ni madhaifu ya mfumo wa voda katika kulinda wamiliki wa laini hizo za biashara.
Huo si mkopo wa kawaida bali ni mkopo kwa mawakala wakiishiwa float. Ni huduma inapatikana kwa mawakala na haipo kwa bahati mbaya ni product yao kwa mawakala
 
Huo si mkopo wa kawaida bali ni mkopo kwa mawakala wakiishiwa float. Ni huduma inapatikana kwa mawakala na haipo kwa bahati mbaya ni product yao kwa mawakala
Vyovyote unavyoielezea haiondoi ukweli kuwa kuna madhaifu katika kutekeleza hilo. Unapokuja na product mpya, lazima waje na suluhu kulinda wamiliki halali wa biashara hizo. Hizo ni laini za biashara, si jambo la kushangaza mtu zaidi ya mmiliki kuendesha laini hiyo. Kinachotakiwa ni mbinu stahiki katika ulinzi.
 
Una uhakika na honga?
 
Kama unamwamini mtu unampa line yenye float ya mamilion na anatuma kwa wateja kwa kuweka pin basi ina maana unamwamini anaweza kukopa float.
Kama unaona kukopa float uwe mchakato basi akija mteja anataka atumiewe milion 2 nao unapasea uwe mchakato hapo
 
Huyo kijana umemkabidhi kila kitu ili akuendeshee biashara yako. Kijana kaona mtaji umeyumba ngoja akope ili biashara iendelee. Japo hujatupa mkataba baina ya mwajiri na mwajiriwa, kwa hiyo tunatoa ushauri kwa kukisia tu. Hivyo Hilo deni ni la office na mwenye office ni wewe.
 
Huo si mkopo wa kawaida bali ni mkopo kwa mawakala wakiishiwa float. Ni huduma inapatikana kwa mawakala na haipo kwa bahati mbaya ni product yao kwa mawakala
Ina maana kwenye hiyo huduma
Kwenye kuconfirm hakuna taarifa mhusika anapata kwamba ameomba mkopo
 
Hiyo biashara ulikuwa unaiendesha wewe mwenyewe binafsi au ulikuwa msimamizi mmiliki wakati aliyekuibia akichakata madili ya kuzalisha mali?
 
Na wewe kwanini unaweza kumuamini mfanyakazi wako pasipo kuchukua tahadhari na bila kuwa na closer monitoring
 
Ina maana kwenye hiyo huduma
Kwenye kuconfirm hakuna taarifa mhusika anapata kwamba ameomba mkopo
Mkuu hiyo huduma iko hivi. Kuna wakati kama wakala unaweza kujikuta una cash lakini huna float, sasa mawakala huwa wanabadilishana float unakuta una wakala unamjua labda unamtumia tigo yeye anakutumia ya voda na ndio maana wana magroup yao. Hii si official ni njia watu waligundua kuweza kuepuka kwenda kudeposite pesa kila mara.
Sasa voda wao wakaja kuwa ukiishiwa float kama wakala unaweza kukopa float kwa hiyo line yako. ukirudisha ndani ya saa 10, makato ni madogo sana ila yakizidi makato ndo yanakuwa makubwa kidogo na wanaikata pale unapoweka floaat, au mtu akija akatoa pesa.
Sasa zamani line zilikuwa mbili, ya kuendesha biashara nyingine ya kufuatilia biashara na kupokea comission. Siku hizi huo mfumo haupo line ni moja ile ile till. So messages na kila kitu ni humo humo kwenye line.
Hivyo, ukiweka mtu hakikisha unamwamini, unafuatilia maana kitendo cha kumpa mtu line, fedha in cash, float ni sawa umempa power of attorney kufanya yale yote wewe mwenye line uliyostahili kufanya.
Na hii huduma ipo kufanya mtu anayehitaji float kwa dharura aipate haraka labda mtu anataka kuweka ila kapungukiwa, sasa ikiwa itachukua muda huo itakuwa haina maana kwa kuwa mtu si angeenda deposite tu kama kawaida.
 
Wasajili line mbili za mhusika
Ili ikitokea kitu kama hiki mhusika apate taarifa au ni ngumu kuweka mfumo kama huo
 
Wasajili line mbili za mhusika
Ili ikitokea kitu kama hiki mhusika apate taarifa au ni ngumu kuweka mfumo kama huo
Hivyo ndivyo walianza voda line za till za mwanzo zilikuwa mbili mbili, ila mitandao mingine wakaja na moja, na voda wakaachana na huduma ya line mbili mbili ikawa line moja moja.
Ni jukumu la mhusika kuweka namna ya kutoibiwa unamkabidhi mamilioni mtu bila kufuatilia mkuu.
Halafu huenda si mara ya kwanza kukopa, ila ni sababu kapoteza fedha ndipo anamaindi. Hiyo huduma kwa emergence za float mawakala wanaipenda shida ni pale ucheleweshe kurudisha fedha waanze kukulima riba.
 
Hapo mkuu mtafute mtuhumiwa..... Voda hawahusiki kwa sababu hawakukwambia umwajiri mtu.

Songea pia ulikubali vigezo na masharti kwa kubonyeza 1.


Pole sana

Ova
Hayo uliyoyaandika yananihusu?
 
Mbaya wako ni huyo kijakazi wako, kusumbuka na voda ni kujipotezea muda tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…