USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

havina mpango wowote hapo ndipo napokubali ya kuwa ukimuona kobe juu mti ujue kawekwa.Toa hivi vt havina mpango wowote
 
kwanini viwepo ngazi ya udiwani na halmashauri na si bunge na executive?? is it because ni wanawake walio kwa viti maalum?give us your reasons.....:A S 13:

Maamuzi mengi yanatakiwa yafanyike ngazi ya chini kabisa yaani "grass root" ambayo ni baraza la madiwani. Kwa maana nyingine Baraza la madiwani linatakiwa liwe na mchango mkubwa sana katika kusimamia na kuleta maendeleo ya sehemu husika kuliko Bunge. Bunge kazi yake ni kugawa rasilimali zilizopo lakini jukumu la kusimamia kule chini ni baraza la madiwani. Tatizo linalofanya kazi za baraza la madiwani zisionekane ni kuingiliwa kiutendaji na Serikali kuu. Hivyo ushirikishwaji wa kina mama ngazi hii ya nchi ni muhimu kuliko hata Bungeni maana huduma zote za jamii - afya, elimu, huduma ya uzazi salama nk zinatolewa katika ngazi ya Halmashauri inayosimamiwa na madiwani
 
Nimeshuhudia wanaume wakisema na wao wapewe nafasi ya viti maalumu! Kazi kweli kweli....
 
Binafsi ningependa nafasi 10 za ubunge wa kuteuliwa na Rais na viti maalumu hizi nafasi zisiwepo!
 
Sio viti maalumu tu, hata Bunge lenyewe lisiwepo kwani halitusaidii chochote sisi walalahoi na ni mzigo kwetu tena kuliko wa dowans!
 
Swala cio viti maalum tatizo ni ufanisi wa mbunge yoyote mi naona idadi ya wabunge ipungue 360 too much,chukulia wengine wapo kwa ajiri ya kuzomea wenzao kama majuha na wengine kazi kusinzia kama yule ko....ba

Nakubaliana na hoja hii.....hakuna ufanisi from both sides,wale wa viti maalum na wasio viti maalum.....
 
Sio viti maalumu tu, hata Bunge lenyewe lisiwepo kwani halitusaidii chochote sisi walalahoi na ni mzigo kwetu tena kuliko wa dowans!

Kazi za bunge zifanywe vipi Matarese?? natamani kufahamu mbadala wa bunge waweza kuwa nini?
 
Ivi pale bungeni tunaona hawa watu kama kina viky kamata ni wabunge wa kina nani maana mbunge ni mwakilishi wa watu wao wana wawakilisha kina nani viti maalumu ifutwe jamani
 
Dk. Kashilila aliwaponda wabunge wa viti maalumu akisema kundi hilo ni mzigo kwa taifa kwa kuwa hawana kazi wanayoifanya zaidi ya kukidhi maslahi ya kisiasa.

Dk. Kashilila alisema ni Tanzania pekee ndiyo yenye wabunge wa aina hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine zinazofuata mfumo wa mabunge ya jumuiya ya madola (Commonwealth).


Mtendaji huyo wa Bunge alihoji sababu za kuwepo kwa kundi hilo la wabunge, wakati wabunge wa majimbo wapo. Wabunge 102 kati ya wabunge 350 waliopo bungeni hivi sasa ni wabunge wa viti maalumu.


"Wabunge wa majimbo wapo 239, ndiyo kusema kwamba katika eneo lote la Tanzania hakuna eneo lisilokuwa na uwakilishi bungeni. Ukisema kila mbunge wa jimbo aende jimboni kwake, utakuta nchi yote ipo covered (ina wabunge).

"Sasa unajiuliza kama hivyo ndivyo hawa wabunge wa viti maalumu wa kazi gani
? Wanafanya kazi ipi special (maalumu) ambayo haifanywi na mbunge wa jimbo?" alihoji.

Alipoulizwa iwapo hoja yake hiyo inalenga kushauri wabunge wa viti maalumu wafutwe
, Dk Kashilila alisema: " Mimi siwezi kushauri moja kwa moja kwamba wabunge hawa wafutwe, ila tunaweza kufanya marekebisho tukaiga affirmative policy ya Uingereza.

"Tukatenga maeneo, kwamba katika kila majimbo kumi ya uchaguzi majimbo manne yawe kwa ajili ya wanawake kama hoja ni kuwa na wanawake bungeni. Hapo vyama visisimamishe wagombea wanaume katika majimbo hayo.

"Kwa kufanya hivyo tutajikuta tumewaondoa hawa wabunge wa viti maalumu ambao kimsingi mimi sioni kazi wanayofanya na badala yake tutakuwa na wanawake bungeni, lakini wanaotokana na majimbo," alisema.


Wakizungumza na Mtanzania kwa nyakati tofauti, baadhi ya wabunge walitoa maoni tofauti kuhusiana na kauli hiyo, huku baadhi yao wakiipinga wazi wazi kauli hiyo.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) alimshangaa Dk. Kashilila kwa kutoa mashambulizi makali dhidi ya wabunge wa viti maalumu, huku akisema wabunge hao ni watu wenye mchango mkubwa kwa jamii.


"Hayo ni maoni yake, lakini kusema wabunge wa viti maalumu ni mzigo kwa taifa mimi nadhani siyo sahihi. Wabunge wa viti maalumu wana mchango mkubwa kwa jamii na hata hao walioweka mfumo huu walijua wabunge wa viti maalumu wana mchango.

"Tunafanya shughuli nyingi za kijamii, tumekuwa tukisaidiana na wabunge wa majimbo katika mambo mbalimbali. Pale ambapo wabunge wa majimbo hawatimizi sisi tumekuwa tukiziba mapengo. Kwa hiyo si kweli kusema wabunge wa viti maalumu hawana kazi ya kufanya," alisema



Maoni yangu:
tunapoteza zaidi ya bilioni 50 kwa miaka mitano kughalimia hawa wabunge wasio na tija kwa taifa wala kwa hao wanawake wanao wawakilisha nadhani tukifuata mfumo wa kiingereza kwa sababu tunafuta huo itakuwa makini zaidi, au kama vipi tuwe na utaratibu ambao wabunge wanatoka kajimboni tu na uwakilishi na ushawishi wao utaoneka wazi wazi, hizo pesa tunaweza kuzitumia kuleta maendeleo makubwa sana, na hawa wakuu wa mikoa na wilaya watolewe pia hakuna kitu cha maana wanachofanya.

SOURCE: MTANZANIA (
Wabunge kikaongoni)
 
hata mimi sijui kazi kubwa ambayo wanafanya hawa wabunge wa vitimaalum. mimi maoni nyangu nahisi zipunguzwe nafasi za wabunge wa vitimaalum. na kuendelea kuwa hawa wanawake nafasi ya viti maalum bungeni ni kuwadekeza . cha msingi kila chama kiwe na mikakati yake ya kuwawezesha wanawake ktk nafasi za uongozi badala ya kusubiri kuwapa nafasi za wabunge wa vitimaalum.
 
Hawa wabunge hawana sababu ya kuwepo na ni mzigo kwa taifa hili maskini.
 
At least kuna kiongozi wa kutoka CCM naye ameona hilo; ni upuuzi kujaza bunge na watu wa kuteuliwa ambao kazi yao kubwa ni kuzomea badala ya kujadili mambo yanayohusu maendeleo ya wananchi. Watu hawa wanakuwa hawako responsible kwa mtu yeyote bali yule aliyewatua.
 
kama ni uwakilishi wa wanawake unatakiwa mi ningeshauri wabunge viti maalum wawepo ila mchakato wa upatikanaji ubadilishwe kila mkoa uwe una idadi flani ya viti maalum kulingana na ukubwa na idadi ya watu afu hizo nafasi zigombewe na wanawake kutoka ktk vyama mbalimbali na wapigiwe kura na wananchi na kama ni zaidi ya mmoja wapangwe kutokana na idadi ya kura . Hii itasaidia ktk uwajibikaji coz watakuwa wamechaguliwa na wananchi sio sasa wanawajibika kwa vyama vyao zaidi kuliko wananchi sababu wamepata ubunge through vyama na wala sio wananchi tusipobadilsha hivyo bungeni wataendelea kuingia mahawara na watoto wa vigogo wa vyama vya siasa ambao hawana uchungu na taifa bali wameenda kuganga njaa na kulinda maslahi ya vyama vyao no wonder wanashabikia tu kipuuzi puuzi tu ka ma***ya wameeona pesa na mzinga wa konyagi
 
Siku ya wanawake duniani nilialikwa star tv nikiwa daktari ili nifafanue nafasi za wanawake katika sector ya afya, nilianza kwa kuwauliza maswali;-
1. je mnaamini kuwa mnaweza bila kuwezeshwa
-wakajibu, ndiyo tunaweza.
2. je viti maalum ni aina gani ya uwezo, je inaepuka dhana yenu ya kuwezeshwa?
- no huko unaenda kusiko kuhusu kabisaaa
3. je hamuoni kuwa kauli mbiu yenu ya ''tukiwezeshwa tunaweza'', inawakosesha uhalali wenu wa kuweza bila back up
-kwa hilo walikuwa wakali sana,ila niliwaomba wadhihilishe kudai haki yao ya kutodharaulika kwa kufanya maandamano nchi nzima wapinge viti maalum,kwani vinawadhalilisha,na wawe tayari kuingia ulingoni kama wabunge wengine wa kucchaguliwa,si wanasema haki sawa,na pia mwanamke anaweza kama mwanaume!!!!!
BASI NI HAYO TU ILA KWA HIVI VITI MAALUM HAKUNA ANAYEJUA KAZI YAO NA FAIDA YAO ZAIDI YA KUTAFUTA BALANCE TU YA KIJINSIA,AMBAYO WAO WANASEMA MUDA WA MWANAMKE KUBEBWA UMEISHA...SO LET THEM TOIL FOR WHAT THEY THINK,TO JUSTIFY THEIR DIGINITY.
 
Back
Top Bottom