USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

kama ni uwakilishi wa wanawake unatakiwa mi ningeshauri wabunge viti maalum wawepo ila mchakato wa upatikanaji ubadilishwe kila mkoa uwe una idadi flani ya viti maalum kulingana na ukubwa na idadi ya watu afu hizo nafasi zigombewe na wanawake kutoka ktk vyama mbalimbali na wapigiwe kura na wananchi na kama ni zaidi ya mmoja wapangwe kutokana na idadi ya kura . Hii itasaidia ktk uwajibikaji coz watakuwa wamechaguliwa na wananchi sio sasa wanawajibika kwa vyama vyao zaidi kuliko wananchi sababu wamepata ubunge through vyama na wala sio wananchi tusipobadilsha hivyo bungeni wataendelea kuingia mahawara na watoto wa vigogo wa vyama vya siasa ambao hawana uchungu na taifa bali wameenda kuganga njaa na kulinda maslahi ya vyama vyao no wonder wanashabikia tu kipuuzi puuzi tu ka ma***ya wameeona pesa na mzinga wa konyagi

umenena ndugu ni lazima na wao wagombee kwa njii hii naiafiki
 
Wabunge wa viti maalum ni kirima tu, ndio maana tumeshuhudia vigogo wa CCM mume na mke wamekuwa bungeni mume wa kuchaguliwa na mke wa ubunge wa kirima. Wabunge wengine ni mabishow bungeni labda wana mabosi wao waliowaweka pale, maana wanachosubiri ni posho tu na hakuna mchango wanaotoa ila kuzomea tu.
 
Wengi wa wabunge wa viti maalum ni vimada,wake na mashoga wa wakubwa. Hawana maana wafutwe tu.
 
mimi naomba wabunge waliopo humu watupe undani wa hivi viti kama vina manufaa
na kama ndio kwa nini tusifanye kama uingereza kila mbunge anatoka jimboni, maana hivi
nafaa, baadhi ya wanawake wanaozipata wanajulikana kabisa ni chakula cha mabosi kwa baadhi ya
vyama vya siasa,
kama kwenye tunataka kuwawezesha wanawake tuwape ndoano (majimbo) na sio samaki kila siku
kwanza tulifilisi taifa na
pili tunawafanya kujiona viti maalumu hii ina wanyima nguvu kama wabunge wengine, sio hivyo tu
ni ngumu kujua hawa wabunge wamefanya nini kitaifa? ni wabunge wakutetea chama na waliowapeleka bungeni
sisi ni nchi masikini tunatumia pesa ovyo ovyo namna hiyo wakati nchi tajiri wana -save matumizi kwenye tabaka la utawala

Wafutwe. Dk kashirima ameshaona watu wanateua mademu zao kuwaleta Bungeni, haina maana.

hawana maana ...sasa kama Vick kamata eti mbunge sasa anaoingea nini bungeni kama sio kwenye kujipaka mapoda tu na kujibinua binua

Hawa wabunge hawana sababu ya kuwepo na ni mzigo kwa taifa hili maskini.

Hawana maana hao wafutwe.

At least kuna kiongozi wa kutoka CCM naye ameona hilo; ni upuuzi kujaza bunge na watu wa kuteuliwa ambao kazi yao kubwa ni kuzomea badala ya kujadili mambo yanayohusu maendeleo ya wananchi. Watu hawa wanakuwa hawako responsible kwa mtu yeyote bali yule aliyewatua.

Wafutwe ama kupunguzwa, ni wengi mno hawana mchango wowote, angalia bunge la sasa viti maalum ni upupu mtupu.
 
Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) alimshangaa Dk. Kashilila kwa kutoa mashambulizi makali dhidi ya wabunge wa viti maalumu, huku akisema wabunge hao ni watu wenye mchango mkubwa kwa jamii.
SOURCE: MTANZANIA (
Wabunge kikaongoni)

Mna mchango gani mafisadi ninyi kama siyo kuwahudumia baadhi ya wale waliowapa ulaji? Ngojeni dola lichukuliwe na chama makini muone hivyo viti vyenu, viti maalum vitawekwa jikoni.
 
katika kitu ambacho niko tayari kupigwa risasi katika maandamano, ni ili la viti maalumu
tunapoteza hela nyingi sana , kwa kisingizio cha picha za wanawake katika bunge waonaingia kwa
njia za vitu maalumu wakati wanakwenda humo kwa manufaa ya vyama vyao na sio wanawake,
lakini pia kwa nini tulipia zaidi ya bilioni 50 kwa ajiri ya kitu ambacho akina manufaa kwa taifa.

hapa tunalipia hela za vipodozi kwa hawa vimada wa mabosi na vigogo na vigogo wa nchi hii
mimi naomba kama kuna mtu ana historia ya hawa kina mama walivyoingia ingia hapo mjengo hawapasue hapa mmoja moja, ili wananchi wajue wanalipia nini?


 
Sijuhi Kashirira naye ataitwa mchochezi,tusubiri

kimsingi wanaongeza umasikini kwa kufaidi rasilimali zetu,napendekeza tutafuta ratio kwa kila mkoa labda tuweke tu kwamba pale chama kinaposimamisha wagombea wake ama kimajimbo ama kimkoa basi iwe razima kila chama kitenge asilimia kadhaa ya wagombea wake eg.20% wawe ni akina mama

na wao waende wakasimame majukwaani waombe kura watakaochaguliwa waende na watakaoshindwa kwenye kura basi ilimradi vyama vitakuwa vimewasaidia kwamba walipewa nafasi lakini kupitia sanduku wananchi hawajamchagua fulani

nadhani hii itasaidia kuwabeba kichama lakini na wao watakuwa wameonesha wamepigana na wananchi wamewaridhia ...hii vipi wanajamii
 
Kwa nchi zetu za africa wanawake bado wanadharaulika,mi naona ni jambo jema tu wanawake kupewa hivi viti maalum,ili na wao watoe mchango kwenye jamii, ila sasa malengo yanatumika vibaya sijui mchumba wa fulani, mama mkwe, marafiki.
 
Frankly speaking Kashilila amekonga mtima wangu kama kweli kaliona hilo. Hatuhitaji serikali iwe na mzigo wa msusulu wa watu wanaoishi kwa welfare with fictitious leadership posts (e.g wabunge wa kuteuliwa na viti maalum, manaibu waziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa maendeleo wa halmashauri za miji na majiji, you name them) Tanzania inaweza kuendelea kama tutakuwa na serikali ndogo ya watu makini wanaofanya kazi kwa ajili ya nchi yao siyo matumbo yao. Political pay back zinadidimiza taifa.
 
Sitaki kugeneralize kuwa wabune wa kuteuliwa hawafai kwani kuna wabunge wengi wa kuchaguliwa ambao ni bure kabisa kuliko hata hao wa kuteuliwa. Kuna Amina Chifupa (RIP) alikuwa wa kuteuliwa lakini mchango wake bungeni ulikuwa ni wa juu kuliko wabunge wengi wa kuchaguliwa. Jambo ninalotaka ni kuondoa tu huu utaratibu wa kuteua wajumbe kwani kufanya hivyo kunaondoa kabisa dhana ya Bunge kuwa chombo cha uwakilishi. Wabunge wengi wa kuteuliwa wana divided royalty, hasa wale wa kutoka chama tawala kwa vile uteuzi wao hufanywa kwa baraka za viongozi wa serikali kuu, ambayo wanatakiwa kuisimamia wawapo bungeni.
 
Mkuu hebu angalia upande wa magamba tukianza kumention hapa ni balaa, hapa tunaangalia wabunge wote wa viti maalum, kuna kina Catherine Magige, Vicky Kamata n.k. Acha ushabiki angalia reality.

nawewe unaweza jaribu kidogo kutupa vicheko kwa kuwataja wale wa chama cha magambaa ambao walipewa viti maalum kwa sababu kama alizozitaja ritz
 
Mimi siwezi kushauri moja kwa moja kwamba wabunge hawa wafutwe, ila tunaweza kufanya marekebisho tukaigaaffirmative policy ya Uingereza[/B].[/SIZE][/FONT]

"Tukatenga maeneo, kwamba katika kila majimbo kumi ya uchaguzi majimbo manne yawe kwa ajili ya wanawake kama hoja ni kuwa na wanawake bungeni. Hapo vyama visisimamishe wagombea wanaume katika majimbo hayo.


red: napinga vikali sanaaaaaa, ushindwe....kafulila na pepo mchafu mwenye rangi ya kijivu. hii itakuwa ni kutowatendea haki watu wa majimbo fulani na ndio mwanzo wa kuzorata majimbo tunahitaji wawakilishi hatuangalii jinsia, mbona dada halima ameweza tena dhidi ya mwenyekiti mbatia, rose kamili, dada regia walileta kashikashi october mpk wakachakachuliwa.

Jamii imestaarabika sana sema ccm ndio inatukuza huu upuuzi wa kuwa wanawake wanaonewa kitu ambacho 2011 hakipo
 
hiyo mbona sio siri mkuu, kila mtu anajua, mkuu wa kaya kawajaza humo kibao
nawewe unaweza jaribu kidogo kutupa vicheko kwa kuwataja wale wa chama cha magambaa ambao walipewa viti maalum kwa sababu kama alizozitaja ritz
 
tatizo wanawake wamejilegeza mno, badala ya kupambana kama wanavyodai 50 kwa 50 sasa wanakuwa wanategemea jeck za wanaume, na mbaya wanaume wasiomuogopa Mungu ukijipendekeza kuwa karibu yake lazima akuchakachue kwa kukuahidi viti maalum. wanawake andamaneni kupinga kupewa viti maalumu. Mnadharilishwa kwa hilo
 
husinivunje mbavu mkuu, lakini hawa lazima tuwatoe,
kunapoteza pesa nyingi sana kama taifa kwa masilahi ya siasa
hizo pisa mpaka sasa tungekuwa na hospitali kubwa zaidi ya kumi
na tano
Mimi siwezi kushauri moja kwa moja kwamba wabunge hawa wafutwe, ila tunaweza kufanya marekebisho tukaigaaffirmative policy ya Uingereza[/B].[/SIZE][/FONT]

“Tukatenga maeneo, kwamba katika kila majimbo kumi ya uchaguzi majimbo manne yawe kwa ajili ya wanawake kama hoja ni kuwa na wanawake bungeni. Hapo vyama visisimamishe wagombea wanaume katika majimbo hayo.


red: napinga vikali sanaaaaaa, ushindwe....kafulila na pepo mchafu mwenye rangi ya kijivu. hii itakuwa ni kutowatendea haki watu wa majimbo fulani na ndio mwanzo wa kuzorata majimbo tunahitaji wawakilishi hatuangalii jinsia, mbona dada halima ameweza tena dhidi ya mwenyekiti mbatia, rose kamili, dada regia walileta kashikashi october mpk wakachakachuliwa.

Jamii imestaarabika sana sema ccm ndio inatukuza huu upuuzi wa kuwa wanawake wanaonewa kitu ambacho 2011 hakipo
 
Nadhani kwenye jambo la kitaifa kama hili,tuweke pembeni mambo ya vyama, na tujadili kwa manufaa ya taifa, viti maalum ilikuwa kuleta balance, harakati za kuwapa wanawake nguvu/nafasi na usawa zilipoanza,ziliingia kila nyanja, hivyo hata siasa bungeni ililazimika ifanyike kwa namna ya kuwateua ili wahusike kwenye kutoa mamuzi kwa jamii zao, ila sasa hawa wanawake wameamuka sana leo hii wanaamini kuwa wanaweza na elimu ya haki sawa ilikwisha enea kote, na hakuna sababu ya kuwateua tena kwa naman hii,kwanza wanasababisha chuki miongoni mwao kati ya waliopata na waliokosa, na pengine wanasababisha migogoro isiyoleta tija kwa vyama vya siasa.....nafasi hii ifutwe na isionekane katika katiba mpya ijayo.
 
mkuu hebu angalia upande wa magamba tukianza kumention hapa ni balaa, hapa tunaangalia wabunge wote wa viti maalum, kuna kina catherine magige, vicky kamata n.k. Acha ushabiki angalia reality.

ni kweli wabunge wa viti maalum wanajaza ukumbi tu, kama akina chiku abwao, lucy owenya na ms lissu mchango wao sifuri!
 
Dhana nzima ya viti maalum IFUTWE KABISA. Miaka 50 ya Uhuru watu hawajakomaa mpaka wabebwe na viti maalum? Hao wanaosema kuwa wabunge wa viti maalum wana mchango mkubwa ni upi huo? na hawawezi kuutoa huo mchango mpaka wawe bungeni? mambo ya kujiuliza;

1. Kuna wabunge viti maalum-vijana je vijana wamefaidika nini kupitia kwa uwakilishi wao? ajira? elimu bora?

2. Wabunge wa wanawake - ni kitu gani wamesaidia wamama? watoto wa kike wanabakwa kila kukicha hawa wabunge wanawakilisha nini hasa? Mbona TAMWA wanatoa mchango mkubwa tu kwa wanawake bila uwepo wao bungeni?

3. Na hawa wabunge viti maalum - vyama vya wafanyakazi wanateteaje maslahi ya wafanyakazi? Bunge lililopita Mh. Mnyika alikuwa anatetea uwakilishi wa wafanyakazi idara fulani hakuna mbunge kupitia vyama vya wafanyakazi aliyejitokeza kumuunga mkono! Mishahara ya wafanyakazi mgogoro wako wapi hao wabunge wa viti maalum?

4. Ndugu zetu maalbino wanapata shida sana na wengine wameuliwa kinyama. Mh. Shymaa (sorry my spelling) kafanya nini tangu alipoteuliwa? Alishaleta hata hoja binafsi kutetea haki za maalbino? Hivi Mh.Shymaa anaweza kusema ni kesi ngapi zinazousiana na maalbino ziko mahakamani? na ajenda yake ni nini hasa kuhusu haki za maalbino?

5. Mama Ana Abdallah amekuwa bungeni kwa kipindi kirefu kuliko wabunge wote walioko bungeni kwa sasa. Na tunajua kipindi hiki kapitia viti maalum -NGOs. (yeye pamoja na Rita Mlaki). Sasa NGOs zinafaidika vipi na uwakilishi wa hawa watu?. Kuna nini hasa kimebadilika tangu wawili hawa waingie bungeni kwa tiketi hiyo ya NGOs?

Hivi vijana, wanawake, wafanyakazi, NGOs vikundi vyote hivi haviko kwenye majimbo? Mfano kwenye jimbo la Temeke mbunge atakuwa anahudumia watu walio nje ya hivyo vikundi?

Note: Yapo majimbo mengi yenye wakazi wengi. Kwa mfano, jimbo la Ubungo lina watu zaidi ya laki moja (100,000). wakati huo huo kuna majimbo yana watu wachache i.e chini ya 8,000. Kama Serikali ina uwezo kwa kulipa wabunge wa majimbo ya kinadharia kwa nini basi wasigawe/kupunguza ukubwa wa majimbo yenye watu wengi ili kila mbunge apata pa kugembea na zaidi awajibike kwa wananchi na sio kwa vyama vya siasa.

KATIBA MPYA inakuja. ni vizuri TUFUTE KABISA viti maalum. Hivi viti ni maalum kulinda sheria za kinyonyaji, maalum kusifia serikali hata pale inapozembea kutimiza wajibu wake kwa wananchi, maalum kupumbuza watu kuwa maslahi yao yanawakilishwa wakati sio kweli, maalum kuendeleza nidhamu ya woga na unafiki. Hivi viti ni maalum kuangamiza umma ili mradi wakubwa waneemeke. Viti maalum wafutwe. Kabisa.
 
Back
Top Bottom